SoC01 Uraibu wa Ponografia

Stories of Change - 2021 Competition

Jade_

Senior Member
Apr 19, 2015
122
214
`Kuna mtu hapa Jamii Forum alielezea kisa chake na kwamba anaweza kujifungia ndani akiangalia video za ngono huku akipiga punyeto kwa masaa hata 12. Kuna watu walifikiri hii ni “chai” (uongo) lakini watu wanapata sana hizi shida ila hawawezi kuongea kwa kuwa ni aibu kwenye jamii. Unaweza kukuta kundi la vijana limeinamia simu ukafikiri wanafanya kitu cha maana kumbe wanaangalia ponografia. Siku hizi hata watoto wanakutana na hizi video mtandaoni na zinawaharibu mapema sana. Rejea uzi wangu wa jinsi mtoto anavyoathiriwa na elimu anayopata akiwa mdogo sana.

Watu wengi sana wameingia katika dimbwi la uraibu wa video za ngono za mtandaoni, na wanatafunwa taratibu bila wao wenyewe kujijua. Uraibu huu ni mbaya sana kuliko uraibu wa madawa au pombe na madhara yake ni kama ya kulevya. Familia zinaangamia, vizazi na vizazi hurithishana tabia hizi na watu wanabaki na maumivu makali sana kwenye nafsi zao. Rejea uzi wangu kuhusu uraibu wa ngono kiujumla. Uraibu huu unasababisha magonjwa mengi ya kisaikolojia kama vile sonona, kuharibu ubongo kibayolojia, kuumwa mwili na kwa wanaume zinapunguza nguvu za kiume na hata kupelekea uhanisi. Mtu atalalamika sana, atazunguka hospitali zote na kwa waganga wote kutafuta tiba ya ugonjwa wa nguvu za kiume lakini tiba inaweza kuwa kuacha kuangalia video za ngono. Uraibu huu unaambatana na uraibu wa kupiga punyeto.

Dalili za uraibu wa video za ngono ni kukaa muda mwingi sana mtandaoni unatafuta video hizi. Yaani kama upo nyumbani unaanza kwanza taratibu kusaka video ambazo zinaweza kukidhi mahitaji yako huku unapiga punyeto na ukikaribia kufikia mshindo unaacha kwanza unaendelea kutafuta video nyingine tena. Mwingine akiona tu tarakinishi tayari anapata hamu anatamani aende tu kwenye video hizo. Mtu kama huyu, kwa sababu waigizaji kwenye sinema hizi wanafanyia plastic surgery sehemu zao za siri (wanawake) na wanachukuliwa wale wenye maungo makubwa (wanaume) basi anatamani tu kulala na watu wa aina hii. Anakuwa hana hamu na watu wa kawaida, na kwa wanaume atajiona amepungukiwa nguvu za kiume.

Dalili nyingine ni kwamba mtu huyu anaanza kuwa na tamaa nyingine ambazo hakuwahi kuwa nazo kama vile mapenzi ya jinsia moja, kupitia mtaroni, mapenzi na watoto, mapenzi na wanyama au mapenzi na ndugu. Anataka kufanya staili za kila namna akiona kwenye video hizi na kifo cha mende kinaonekana ni ushamba. Hii ni kwa sababu ponografia hushtusha na hisia za kushtuka na za kupata hamu zinafanana sana (moyo unadunda kwa haraka zaidi, unaanza kusikia joto nk). Hivyo basi unaufundisha ubongo kwamba ili upate raha inabidi uangalie na kufanya makubwa zaidi vitakavyokushtua. Utaanza na video za ngono za kawaida lakini kadiri unavyoendelea kuzoea utatafuta zinazokushtua ambazo si za kawaida na mwishowe utajikuta ambako ukuwahi kutarajia kuwepo. Dalili zipo nyingi na chache za kuongezea ni mtu kupoteza mahusiano mazuri aliyowahi kuwa nayo kama ya ndugu jamaa na marafiki, kutokufanya vizuri shuleni na kazini, kubadilika hulka ghafla bila sababu ya msingi nk.

Video za ngono za mtandaoni kiukweli ni aina ya udhalilishaji kwa wanawake. Hata wanawake wanaocheza hizi video wanakuwa tayari wana matatizo ya kisaikolojia (aidha waliwahi kudhalilishwa kingono au walilelewa kwenye mazingira hatarishi) kwa hiyo wanakuwa na chuki binafsi. Mwanamke mwenye uraibu wa kuangalia video hizi atataka kufanyiwa kama wanawake kwenye hizi video wanavyofanyiwa (matendo ya aibu) na bila ya yeye kudhalilishwa anaona kama hajapata raha.

Kwa wanaume wao ni mwendo wakudhalilisha. Asilimia kubwa ya video kwenye tovuti za ponografia zinahamasisha kutoka na watoto, kutoka na ndugu, kufanya mapenzi ya jinsia moja, kubaka, kufanya unyanyasaji wa kingono nk. Hii inajionyesha moja kwa moja kwenye jamii, mtu anaona kama kumvunjia au kuvunjiwa heshima ndio mapenzi yenyewe. Kitu ambacho si kweli na husababishia watu vidonda visivyotibika.

Kama una uraibu huu lazima ufanye kila namna uache kuangalia video za ngono. Kufanya hivi ni ngumu mno lakini ni kitu kinachowezekana. Kama mtu anavyoanza kuacha madawa ni lazima kwanza uanze kupunguza kuangalia video hizi. Siku za mwanzoni utajisikia vibaya sana, unaweza hata kuumwa lakini ni muhimu ujikaze na usikate tamaa. Unatakiwa kupunguza taratibu mpaka uje kuacha kabisa.

Wewe mwenyewe utashangaa jinsi maisha yako yatakavyobadilika na pia hata matatizo madogo (kuumwa, uchovu, kukosa hamu ya kula, kutoweza kufikiri au kutumia ubongo kwa kina nk.) yatapotea kwenye maisha yako. Watu wengi wanafikiria kwamba wamelogwa lakini yote haya ni madhara ya ponografia. Video za ngono si za kuangalia mara mojamoja, bali ni kitu cha kutoangalia kabisa.

Kitabu cha Your Brain on Porn: Internet Pornography and the Emerging Science of Addiction cha Gary Wilson kinaongelea kwa ukubwa na kwa undani zaidi kuhusu uraibu huu.
 
Porn na Punyeto huwa zina roho chafu ya kishetani, ukishafnya kitendo hiki pepo hao huuanza kufanya kazi yao na dalili ni kukosa amani, kukosa hamu ya kuishi, kujihisi hauna thamani . Kuna video nyingi Youtube zinaonesha pepo hao wakitolewa kwa maombi.
Jinsi ya Kuacha ni kumfanya Yesu kuwa role model wako. Kumbuka hakuna kitu chochote kinaweza kukupa furaha katika hii dunia - Furaha ya kweli ipo kwenye kusali na kujazwa Roho Mtakatifu rohoni mwako. Pombe , Uzinifu zina furaha ya muda na maumivu makali ya muda mrefu. STAY PURE. - MWILI NI BOKSI LA ROHO, NA WEWE NI ROHO
hivi mnajua kuwa jini halikai sehemu chafu? sasa mimi nkipia zangu nyeto hilo jini litaenda kukaa wapi kwenye huu mwili wenye janaba? nimesema jini sababu unayemwita pepo huwa sio kiumbe ni hali/vibe ila jini ndio kiumbe mwenyewe.

anyway Mkuu nilikuwa kwenye moja na mbilli za kutetea chama chetu chaputa
 
Hongera sana tena sana, Mungu mkubwa.
Unaweza kutupa picha jinsi hali yako ilivyokuwa?
Siku zote nilikua mtu wa kujitenga. Nikaona Mungu hanipendi. Nikakata tamaa ya maisha. Nlikua extrovert nikajikuta introvert. Nikajichukia sana.

Nikawa niko addicted kiasi cha kwamba naweza fanya everytym. Iliniumiza. Nilitamani kuacha lakini inahappen siku mbili after ninarudi. Nikateseka sana.

Nilijua fika kuwa hili ndo linalonitenganisha na Mungu wangu. Najua Mungu alikua anataka kunibariki anitendee makubwa but i couldnt make the choice. I was always stuck.

Siku moja ilifika nikasema enuf is enuf..naacha leo...nikajizuia sana. Eh bwana niliteseka nikasema addiction ni nyoko. Lakini kwa msaada wake huyu aliye jua akaniwezesha. Ile kumaliza wiki..mara mwezi..mara miezi..mara mwaka...mara miaka...jamani namtukuza Mungu sana.

So inawezekana sana. Ni kweli ni ngumu sana kuacha tena vita kwelikweli. Lakini inawezekana. Mungu akusaidie wewe unayehitaji msaada wake. Dont give up. Trust, Believe in God.
 
Hii kitu kwa sasa ni a very sensitive topic. Yaani unapozungumzia hili janga unagusa kada tofauti yaani kuanzia vijana na mabinti wadogo na watu wazima.

Lakini pia inawagusa waliopo ndani ya ndoa na wasio ndani ya ndoa pia.

Wanaume kwa asilimia kubwa ndio wahanga wa hili swala. Sababu mwanaume ndie mwenye njaa ya ngono masaa 24 tofauti na mabinti. Mabinti pia wapo ambao wameanza hii tabia ila wao si kama wanaume katika kuathirika especially kimaumbile.

Katika kuachana na huu ulevi wa kingono kiukweli inahitaji 90% ya personal efforts.....

Ila kwa mimi nilichokiona nadhani mabadiliko ya kimaadili na mifumo ya upangaji wa maisha pamoja na maswala ya kifedha kuhusishwa sana katika mahusiano imefanya huu uraibu kushika kasi.

Vijana na wanaume wanaingia sana huku kama shortcut kujiridhisha akili zao zipate utulivu. Kama uraibu mwingine wowote wa madawa ya kulevya na mihadarati, pombe, au kamali, hii ya ponografia pia wahanga hutumia kama njia ya kuescape stress za maisha na kupata utulivu wa akili ili wapate focus mpya.

So Kimsingi nadhani na hali ya uchumi wa sasa wa CCM unachangia sana vijana na mabinti kuingia huko pahala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu anisaidie hii vita bandiko zuri sana nimeshapigana sana na hii kitu ila angalau saiv naona inaisha angalau najicotrol mpka mwezi najikuta nimeshitua ila naiman ntaacha kabisa maana hayo ulioandika ni ukweli mtupu ubarrikiwe sana brother
 
Porn inapunguza sana concentration.
Mzazi ukiona kijana ako wa kiume hafanyi vizuri darasani ebu mchunguze vizuri inawezekana anapiga nyeto kwa porn.
Mimi ni muanga mkubwa wa porn+punyeto+betting.
Bet nimefanikiwa kuacha lakini porn+nyeto mpaka sasa nina mwezi + sijaangalia porn wala kupiga nyeto.
Najua ni ngumu lakini lazima nishinde vita.
 
Porn inapunguza sana concentration.
Mzazi ukiona kijana ako wa kiume hafanyi vizuri darasani ebu mchunguze vizuri inawezekana anapiga nyeto kwa porn.
Mimi ni muanga mkubwa wa porn+punyeto+betting.
Bet nimefanikiwa kuacha lakini porn+nyeto mpaka sasa nina mwezi + sijaangalia porn wala kupiga nyeto.
Najua ni ngumu lakini lazima nishinde vita.
Uko ka mimi bro
 
Hii kitu kwa sasa ni a very sensitive topic. Yaani unapozungumzia hili janga unagusa kada tofauti yaani kuanzia vijana na mabinti wadogo na watu wazima.

Lakini pia inawagusa waliopo ndani ya ndoa na wasio ndani ya ndoa pia.

Wanaume kwa asilimia kubwa ndio wahanga wa hili swala. Sababu mwanaume ndie mwenye njaa ya ngono masaa 24 tofauti na mabinti. Mabinti pia wapo ambao wameanza hii tabia ila wao si kama wanaume katika kuathirika especially kimaumbile.

Katika kuachana na huu ulevi wa kingono kiukweli inahitaji 90% ya personal efforts.....

Ila kwa mimi nilichokiona nadhani mabadiliko ya kimaadili na mifumo ya upangaji wa maisha pamoja na maswala ya kifedha kuhusishwa sana katika mahusiano imefanya huu uraibu kushika kasi.

Vijana na wanaume wanaingia sana huku kama shortcut kujiridhisha akili zao zipate utulivu. Kama uraibu mwingine wowote wa madawa ya kulevya na mihadarati, pombe, au kamali, hii ya ponografia pia wahanga hutumia kama njia ya kuescape stress za maisha na kupata utulivu wa akili ili wapate focus mpya.

So Kimsingi nadhani na hali ya uchumi wa sasa wa CCM unachangia sana vijana na mabinti kuingia huko pahala.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuna duka moja linauza nguo za ndani za kike pale palm village, lile duka now days limeingia kwenye biashara ya SEX TOYS kwa wadada aisee huwa nikitafakari hiyo biashara, naimani kabisa wateja wengi ni addicts wa pornographs ambao hawaridhishwi na binadamu wa kawaida.

Na wafanyabiashara wana lugha nzuri sana sikuizi na madhara ya product wanazouza wao hata haiwahusu.

Na hii impact yake naamin divorce zita double kama sio kutriple in a long run
 
Ubongo unaharibika kwa kupungua "grey matter". Watu wakiangalia porn grey matter inapungua na wakiacha grey matter inarudi.
Wanaume wanapungukiwa nguvu za kiume kwasababu kuangalia porn inawapunguzia sana hamu ya kufanya ngono na wanawake wa kawaida.
Pia kupiga sana punyeto kuna chosha sana mifumo ya uzazi ya wanaume hivo kupunguza kabisa uwezo wao wakuproduce sperm kwa ufanisi.
Huo ni uongo dhahiri
 
Punyeto is safe sex. It contributes highly to your success since it reduces money expenditure. It facilitates performance especially in single sex schools especially in advanced level (pcb). It makes a person comfortable and easily focus on his careers.
It becomes best only if it's done twice or once a week .
What a good timetable!
 
Ni hivi watu wanapungukiwa na grey matter wakiwa waraibu wa porn. (Hata wakiangalia kidogo tu wanapungukiwa).
Wakiacha kabisa grey matter inarudi kama ilivyokuwa. Je hapo hakuna kabisa uhusiano wowote?
Lots of studies have been conducted to prove this.
Nipe full mechanism with well labeled digram if possible otherwise iyo ni story kama story zingine.
 
Ahsante mkuu kwa mchango wako.
Nimeweka jina la kitabu mwishoni mwa andiko langu, ukipenda kujua zaidi kuhusu haya majaribio unaweza kukipitia.
Kama utashindwa kusoma hicho kitabu unaweza kupata maelezo mengi na yenye uhakika zaidi kutoka kwa wanasayansi wenyewe waliofanya haya majaribio mtandaoni.
Does watching porn cause brain damage?
Ha ha ha LOL no.

Pseudoscience site called Your Brain On Porn. That site distorts and in some cases lies about scientific research to try to persuade people that porn harms your brain.

There is a study that, according to YBOP, “proves” that watching porn causes neuron loss. The study looked at two groups of people: college students who said they watch a lot of porn (more than 20 hours a week), and college students who said they don't watch porn. It looked at their brains with an MRI machine and the people who said they watch a lot of porn had noticeable deficits in parts of their brain.

So that proves it, right? People who watch a lot of porn have smaller brains. Porn makes your brain shrink!!!!!!!!

Well, hold on there, hoss. Actually, that's not what the study said at all. Two things that are correlated (porn and brain deficits) aren't necessarily causative. This is one of the most basic parts of science.

If you look at ice cream sale and look at death by drowning, when ice cream sales go up, more people drown. Ice cream causes drowning!!!!!

Well, no, it doesn't.

There is a third factor; sunshine. More people eat ice cream on hot sunny days. More people go swimming on hot sunny days. Ice cream does not cause drowning. Heat causes people to eat more ice cream. Heat causes people to go swimming more.

When the researchers looked at the pattern of brain deficit, they observed that it looked like the brain damage caused by untreated clinical depression. And guess what? Depressed people watch more porn.

Porn doesn't cause your brain to shrink. Depression causes your brain to shrink. Depression also causes people to watch more porn.

This is a great illustration of how pseudoscience works. Pseudoscience assumes that if two things are correlated, one of them must cause the other.
 
I think you don't quite fully understand what the addiction to porn does to the brain.
What you're saying is like saying addiction to drugs doesn't harm the brain because a lot of drug users are already depressed (Which is not true at all drugs absolutely rewire your brain just like porn).
But that's the thing, porn addiction DOES cause depression and other ailments that one might think have nothing to do with porn itself AND damages the brain on top of that.
I think you're the pseudoscientist here trying to twist scientific facts in favour of the very lucrative porn industry just like most "scientists do".
But even more so, tell that to the people who've had their minds and bodies ruined by porn addiction that they're wrong, or that they haven't "understood" the study or whatever notion you're trying to push.
Read more.
 
No you read and study more. And on top of that brainstorm and start thinking for yourself. Maybe even try to find people with a porn addiction (if you don't have one) to get their experience.
The problem is not your mind, it's your mindset!.
 
Kuacha kuangalia porn ni rahisi sana. Ni kubadili tu mfumo wako wa maisha. Punguza mda wa kukaa sana mwenyewe. Punguza kufatilia picha za kusisimua. Mbona utakomboka
 
Kuacha kuangalia porn ni rahisi sana. Ni kubadili tu mfumo wako wa maisha. Punguza mda wa kukaa sana mwenyewe. Punguza kufatilia picha za kusisimua. Mbona utakomboka
Ndio, inabidi kuwa busy.
 
Back
Top Bottom