Uraia wetu na dhana ya mweusi ndio Mtanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uraia wetu na dhana ya mweusi ndio Mtanzania.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mohammed Shossi, Jul 26, 2012.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Habari zenu ndugu zangu wanajf,

  Ni matumaini yangu waraka huu utawakuta mkiwa wazima wa afya ninyi na familia zenu.

  Nianze na mkasa ulionikuta.

  Jana majira ya saa tatu nilipita kituo cha kuandikisha vitambulisho vya uraia katika shule ya msingi Temeke jirani kabisa na msikiti wa Tungi. Nilionana na karani nikamuuliza mimi nina passport je wanataka copy nitoe kurasa zipi? yule bwana alinielekeza kuwa nitoe ukurasa wa kwanza kabisa ule ukurasa wenye maelezo mengi mengi na picha ya adam na amina/hawa/eva. Na ukurasa wenye details nilimuuliza kwanini nitoe ukurasa ule wa mwanzo ilhali ukurasa wenye picha una details zote? akaniambia ni lazima. Basi kwa kuwa ni lazima ilinilazimu nifanye vile nilivyoelekezwa.

  Nikaenda kutoa kopi na kurudi kupanga foleni, ilipofika zamu yangu akawa ameingia bwana mmoja kutoka NIDA akasema watu wengine waende kwakwe kwaajili ya kuandikisha. Mimi nikaenda kwa yule yamaa nikasalimiana nae kisha nikampa kopi ta pasi yangu ya kusafiria akaniuliza huna kitambulisho chochote zaidi ya pasi ya kusafiria? nikamwambia ninavyo ila kwa kuwa tangazo linasema ukiwa na kimojawapo unaruhusiwa kujiandikisha ndio maana nikaenda na ile kopi ya pasi ya kusafiria. Akanijibu hapana sio kweli nenda kalete TIN, kadi ya mpiga kura na cheti cha kumaliza shule ya sekondari. Nikatoka na kwenda kuvichukua na kwakuwa nyumbani si mbali haikunichukua muda nikarudi tena.

  Nilihakikisha nina vyeti mpaka vya chuo na transcripts ili nisije kukwazwa tena yaani nilijtahidi nina vyeti vya ziada na kopi zake.

  Baada ya kurudi kuna mama mmoja akanstaajabu kuwa nimeweza kuwasilisha nyaraka zote kwa muda mfupi namna ile nakusema.

  Mama: Yaani wewe mwelewa sana umeleta vyeti vyote sio kama hao wenzako wenye rangi kama wewe.
  Mimi: Kwani mama wenye rangi kama mimi wanatakiwa kuja na vyeti vyote vilivyoorodheshwa kwenye fomu?
  Mama: Ndio
  Mimi: Kwanini? kwani sisi ni raia wa daraja la pili?
  Mama: Sisi hatujui ila ndio maelekezo tulioelekezwa na bosi wetu.
  Mimi: Nikamgeukia huyo bosi wao nikamuuliza kwanini anafanya vitu doble standards? kwanini anafanya mambo yanayomfanya ahisi kunyanyapaliwa na kutengwa kutokana na rangi ya ngozi yake? kwani kama ni mahitaji yawe ya siri wasitangaze kuwa Watanzania wenye asili ya asia waje na vyeti moja, mbili, tatu?

  Nikamwambia hivi humu ndani mnaaminije kuwa hawa weusi hakuna wanaotoka msumbiji, rwanda, burundi, kongo na kenya? ukiwa mweusi hata ukienda na barua ya mwenyekiti wa serikali za mitaa unaandikishwa ukiwa mweupe unatakiwa uende na mlolongo wa vyeti.

  Nadhani kuwa mweusi hakuamanishi wewe ni Mtanzania kwani Tanzania imezungukwa na nchi nyingi zenye watu wenye ngozi nyeusi ambao wanaweza kuchukua fursa hii adhimu kuupata uraia wa Tanzania kwa chee! Na nina sikia kuna vijana wengi wa kimsumbiji wapo hapa Dar wanafanya kazi za umachinga si ajabu hawa vijana kwa weusi wao wakaandikishwa na kuwa Watanzania lakini kuna weupe "wakuchovya" wakakataliwa kupata fursa hii kwa kuwa tu vyeti vilivyohitajika havikutimia.

  Kwakuwa JF ni mahali wanapopita watu wa kadi mbalimbali naamini mtatoa ushauri na kuchukulia hili swala kwa uzito stahiki!


  Mwisho ni ushauri mdogo kwa NIDA.

  Msihangaike sana na Watanzania wenye asili ya asia wasiofika hata laki tano! Hangaikeni na Weusi wanaoweza kufikia nusu yetu aprox 40 mil. Pengine Watanzania tupo wachache sana ila hii kasumba ya kila mweusi ni Mtanzania ndio inayoongeza idadi inabidi kila mmoja afanyiwe upembuzi yakinifu wa vyeti vyake apewe uraia stahiki.

  Wasalam.

  Mohammed H. Shossi
  P.O.Box 19181
  Dar es Salaam, Tanzania.
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mohammed Shossi

  Mkuu wangu mbona sijaona tatizo mpaka hapo.Nina hakika zoezi likifikia maeneo ya mkoa wa Kigoma hata weusi watakumbana na urasimu mkubwa kwakuwa mikoa ya pembezoni ina idadi kubwa ya wakimbizi.Dar ina wahindi,Pakistan,waChina ndiyo maana weupe lazima wachunguzwe sana.

  Natumaini umenielewa bila chenga.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #3
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nimekuelewa vizuri sana mkuu,

  Lakini ninachosema mimi hata hapa Dar kuna wamsumbiji wengi sana wanafanya kazi za umachinga! Kuna wanyarwanda na wacongoman wengi tu lakini kwa weusi wao wanahesabika wao ni watanzania!
   
 4. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Wafaransa wanasema C est la vie yaani kikwetu "ndio maisha". Fanya wanavyotaka chukua kitambulisho na endelea na maisha yako usiulize sana!


   
 5. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kweli hilo ni tatizo kubwa yaani kuna wanamitizamo ya hovyo kabisa ,ili hili zoezi liwe na maana wote inabidi tupitie kwenye chujio lile sio kuweka makundi.
   
 6. h

  hargeisa JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  utanzania kwa maana ya ngozi haupo hapo ni urasimu .
   
 7. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyo boss si ajabu alishajua kitaa cha hapo mupo wengi(wenye asili ya asia)akaamua kuzua njia ya kupewa chochote,huo ni mchongo tu,kama ungekuwa makini mapema hiyo pass+5000/=tsh ingetosha kufanikisha uliloliendea.
  kwa kifupi waarabu na wahindi ni wepesi kuliwa pesa kwa kuwa haki zenu wengi hamzijui,na hata mkibebeshwa kesi mahakamani mnaogopa kwenda hata kama mnajua 100% ni wadhulumiwa na haki ipo pamoja na nyinyi.
   
 8. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #8
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160

  Mkuu nimependa sana maoni yako! Uraia hautolewi kama karanga maana karanga hata kama huna pesa utaonjeshwa! Hili zoezi lingeleta maana kama wangetumia taratibu zinazofanyika kwenye kazi serikalini na elimu ya juu. Mimi nilipokuwa najiunga chuo kwa elimu ya juu sikuulizwa vyeti tofauti na wenzangu waliokuwa weusi hakukuwa na double standard same applied to all na hili la Uraia lengekuwa hivyo.

  Binafsi sikubalani kuwa ukiwa na kadi ya mpiga kura basi upewe Uraia, sote tunajua hivi vipande watu walikuwa wanaenda wanajaza fomu na kupigwa picha wanachukua vipande hakukuwa na mahitaji ya supporting document yoyote! Kenge na mamba wote waliingia humo! Lilipokuja hili zoezi tukasema sasa chujio lemekuja na pengine lingetusaidia kujua idadi yetu ya kweli na kujua kumbe umasikini unasababishwa na wageni wengi wanaojiita watanzania kumbe bado sana.
   
 9. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  zingatia hilo pass+5000/=tsh inatosheleza,na ungeona kuwa wewe ni mwananchi daraja la kwanza kwa jinsi unakavyopewa huduma ya fasta,hapa ndio tanzania na hizo ndio njia za kupita(karibu sana)
   
 10. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #10
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kaka sio mimi kwanza mimi sijihesabu kama ni hao watu coz zaidi ya kigogo, Kinyiramba kidogo na Kinyaturu jumlisha na kiswahili sijui lugha nyingine especial za upande wa asia.

  Nikutoe wasiwasi tu nimesoma Uhuru Primary Dodoma, kisha Dodoma Secondary na kumalizia Chuo Cha Biashara Dsm. Humo mote nimekutana na wabongo 120% hakuna wahindi wala waarabu na mimi nimekua kwenye attitude hizo hizo mkuu! Naijua haki yangu na jana nilibwata sana mpaka bosi akanywea!
   
 11. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Hilo chujio ndg yangu watakuwa wamechelewa sana'kuna maswali ambayo walitakiwa watumie tu yanatosha kumthibitisha kama huyu mtu ni mtz,Siku 1 nimekutana na kijana flani wa kihindi akiwa na mchumba wake kwa sababu tulikutana kwenye border ya UAE emirate,basi yeye alikuwa anatoka Oman anakwenda Dubai,pale tulikutana dukani bahat mbaya huyu kijana hakuwa na pesa za nchi zile yaani Rial au Diraham'basi katika maongezi tukawa tunaongea english lakini alikuwa kavaa Tshirt imeeandikwa kenya,nikamuuliza vp waijua kenya?akaniambia ni mkenya lakini mimi nafaham kenya kuingia Oman ni vigumu sn nikamuuliza unatumia Pass ya kenya?akasema hapana anatumia Passpt ya Tz yeye na mchumba wake wote wakenya lakini wote wanatumia Pass za Tz,sasa ndugu zangu hebu tujiulize ni watu wangapi ambao sio wa Tz kama huyu na wanatumia paspt za Tz?uhamiaji wanahusika kwa asilimia zote
   
 12. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mohammed Shossi Naona na mimi nitaingia kwenye mkumbo wako na ninawasubiria kwa hamu. Hata mdogo wangu amesumbuliwa ingawa alikuwa na vyeti vyote kuanzia cha kuzaliwa, std 7 mpaka kitambulisho cha chuo lakini walimsumbua sana kwa sababu ya rangi yake.

  Am waiting for them
  .

  Pole Mohammed Shossi, i feel your pain.
   
 13. The Eagle2012

  The Eagle2012 Senior Member

  #13
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole kwa Kunyanyapaliwa Mkuu,Kila sehemu lazima kutakuwa na Mgonjwa wa Akili,Tuvumiliane tu!!!
   
 14. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #14
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Shukran sana kaka ila kwa mwendo huu naona jinsi nchi itakavyogawa uraia kwa wasio stahiki kisa ni weusi
   
Loading...