Uraia wa Zitto Kabwe sasa kuamuliwa Mahakamani

Aliyekuwa Katibu wa (UVCCM) mkoa wa Kigoma ambaye kwasasa amehamishiwa wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, Agustino Matefu amesema kuwa atamburuza mahakamani mbunge wa Kigoma mjini kupitia chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe kwa madai kuwa sio raia wa Tanzania,

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amedai kuwa ushahidi wote anao.

“Kwasasa nimeamua kwenda mahakamani kumfungulia kesi Zitto Kabwe, sababu sio raia wa Tanzania, nimesafirisha wazee wanne kutoka Kigoma kwa ajili ya kutoa ushahidi,”amesema Matefu
Kila la heri
 
Che Nkapa ndie alianza hayo maujinga. Alipoletewa cheti chake cha kuzaliwa kilichoandikwa kwa kireno. Na pia Baba yake Nze Makota alihamia toka Nchumbiji, Ben akiwa na miaka 3/4. Kuanzia hapo ndio akaacha maujinga hayo, akanyamaza.
Viongozi wakuu wa CCM wa sasa wote uraia wao na hata kwa sura zao vinatia shaka.
Sawa UVCCM, ENTER the dragon.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haha jamiiforum raha kwa kweli. Nmecheka mpaka machozi yamenitoka
 
Aliyekuwa Katibu wa (UVCCM) mkoa wa Kigoma ambaye kwasasa amehamishiwa wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, Agustino Matefu amesema kuwa atamburuza mahakamani mbunge wa Kigoma mjini kupitia chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe kwa madai kuwa sio raia wa Tanzania,

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amedai kuwa ushahidi wote anao.

“Kwasasa nimeamua kwenda mahakamani kumfungulia kesi Zitto Kabwe, sababu sio raia wa Tanzania, nimesafirisha wazee wanne kutoka Kigoma kwa ajili ya kutoa ushahidi,”amesema Matefu
Watoto wa CCM wamerithishwa sera za visasi za babazao, mtoto wa nyoka ni nyoka.
 
Kwa hiyo wanataka kumrudisha Rwanda au Burundi!CCM tuache hizo ,sisi tupige kazi,tunajichora tu na uraia wa Zitto .Ok sema sasa Zitto sio raia ,then mtamyamazisha?hata mkimpeleka nchi aliyozaliwa au kwenye uraia wake ndio kwanza ataongea Zaidi.ACHENI KUJICHORA,TUFANYE KAZI.Yeye Zitto achene aendelee kuongea kwani anawanyima usingizi?wakati kila kitu mnacho?ndege ya sita inaingia leo what is your problem?
Maajabu weji naye alikuja kabebwa mgongoni kutoka Rwanda watampeleka naye mahakamani au watamrudisha Rwanda.
 
Huyu Jamaa ni kitasa na dishi lake halijakaza huwa linayumba mara kwa mara.

Namfahamu tokea tukiwa N.I.T 2007/2008 huko
 
Aliyekuwa Katibu wa (UVCCM) mkoa wa Kigoma ambaye kwasasa amehamishiwa wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, Agustino Matefu amesema kuwa atamburuza mahakamani mbunge wa Kigoma mjini kupitia chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe kwa madai kuwa sio raia wa Tanzania,

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amedai kuwa ushahidi wote anao.

“Kwasasa nimeamua kwenda mahakamani kumfungulia kesi Zitto Kabwe, sababu sio raia wa Tanzania, nimesafirisha wazee wanne kutoka Kigoma kwa ajili ya kutoa ushahidi,”amesema Matefu
Huu ndo ujinga ambao kila nikiuuona unanikera sana kwakweli, Tuache upuuzi kama huu kuna mambo mengi ya kufanya nchi hii.Asilimia hata zaidi ya 50 waTz siyo wazawa halisi wa Tz hasa mikoa ya mipakani,unakuta Babu alihamia Tz na wajukuu ndo sisi, tuna mengi ya kushughulikia ila siyo huo upuuzi
 
sure mkuu tunapoteza muda sana kwenye mambo ya kijinga jinga kana kwamba dunia inatusubiria
 
Vigezo vya kumjua raia wa Tz ni rahisi sana. Kwanza, ajue kuimba wimbo wa taifa, pili awe na kovu la sindano ya ndui kwenye mkono wa kulia.
Sababu zako ni mfu, hivi wimbo wa Taifa ni mgumu sana kiasi kwamba asiye raia hawezi kuimba? Suala la ndui sio wote walichanjwa kuna watu huku interior hawa kupeleka watoto wao, na tunaoishi mipakani kliniki tulikuwa tunapelekwa nchi jirani.

Suala la uraia lina vigezo na taratibu zake ikiwemo kuangalia asili ya wazazi wako, mzazi mmoja anaweza kuku fanya ukawa raia wa Tanzania, mfano babaake mtoto akawa mnyarwanda na mamaake mtanzania akazaliwa Tanzania basi mtoto atakuwa mtanzania kupitia mamaake.
 
sure mkuu tunapoteza muda sana kwenye mambo ya kijinga jinga kana kwamba dunia inatusubiria
Mi linanichukiza sana,huwa najiuliza na kushangaa mtu mishipa inamtoka kuhoji uraia wa mtu,Mm binafsi mfano marehemu Baba yetu aliandika documents moja ambayo inaonyesha asili ya nchi tuliyotoka,hapa Tz mkoa fulani alihamia Baba yake Babu miaka ya nyuma sana,babu akazaliwa Tz, Baba akazaliwa Tz, nasisi tumezaliwa Tz halafu jinga litoke huko liseme mm siyo mtz😁😁😁
 
Kabisa Mkuu hawa watu ni dhalimu sana. Ukiwashinda kwenye hoja na kukataa maovu yao yanayoididimiza nchi pia kuyapinga hadharani basi watakutoa uhai, kukubambikia kesi mbaya au kudai kwamba huna uraia.

Zitto amfungulie kesi huyu mburula kwa madai yake ya uongo.

Kete yao ya mwisho ukionesha ni akili kubwa ndio hiyo, sasa ngoja mahakama nayo iwateme aibu mpaka kwenye nywele
 
Walituahidi viwanda tuliambiwa nchi itakua na viwanda kama Canada naona unjenzi wa viwanda umekamilika
Viwanda vya kuzalisha maujinga ya kuwaondoa waTZ KUTOKA kwenye mambo ya msingi ya kuleta maendeleo, hivyo vimekamilika na vinaajiri wajinga wengi tu.
Sasa hivi kwa makusudi kabisa watu wajinga wanajivunia kabisa kusigina siasa safi ya kuheshimu Haki za waTz wenzao kwa kufuata katiba na sheria za nchi walizoapa kuzilinda.
Wategemea watoto wao UVCCM watakuwafurahishaje 'wazazi' wao. "......Maji ni yaleyale, yaliyochotwa kwenye ndoo na yaliyobaki ziwani...." JKNyerere. AMEN.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo nchi yetu ilipofikia Mkuu. Upumbavu wa hali ya juu kila kona tena unaanzia Ikulu.

Watu wengine bhana badala ya ku deal na mambo ya maana ya ujenzi wa taifa ana kazana na zitto kabwe...! Eti nimetuma wazee wanne waende wakatoe ushahidi...hizo nazo akili?

Sent from my SM-J530F using Tapatalk
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom