Uraia wa Zitto Kabwe sasa kuamuliwa Mahakamani

Watu wengine bhana badala ya ku deal na mambo ya maana ya ujenzi wa taifa ana kazana na zitto kabwe...! Eti nimetuma wazee wanne waende wakatoe ushahidi...hizo nazo akili?

Sent from my SM-J530F using Tapatalk
 
Aliyekuwa Katibu wa (UVCCM) mkoa wa Kigoma ambaye kwasasa amehamishiwa wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, Agustino Matefu amesema kuwa atamburuza mahakamani mbunge wa Kigoma mjini kupitia chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe kwa madai kuwa sio raia wa Tanzania,

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amedai kuwa ushahidi wote anao.

“Kwasasa nimeamua kwenda mahakamani kumfungulia kesi Zitto Kabwe, sababu sio raia wa Tanzania, nimesafirisha wazee wanne kutoka Kigoma kwa ajili ya kutoa ushahidi,”amesema Matefu

Kwa ushauri wangu katika kesi hiyo awaunganishe na Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, pamoja na idara ya uhamiaji kwa kushindwa kufanya majukumu yao ya kumbaini mtu ambaye sio raia. Sijajua vizuri elimu ya mtu aliyeibua tuhuma hizi, ila naamini sio ya kiwango cha kusoma na kuandika.
 
Kwanini asianze kumshitaki kwanza baba yake
tapatalk_1547193549954.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo wanataka kumrudisha Rwanda au Burundi!CCM tuache hizo ,sisi tupige kazi,tunajichora tu na uraia wa Zitto .Ok sema sasa Zitto sio raia ,then mtamyamazisha?hata mkimpeleka nchi aliyozaliwa au kwenye uraia wake ndio kwanza ataongea Zaidi.ACHENI KUJICHORA,TUFANYE KAZI.Yeye Zitto achene aendelee kuongea kwani anawanyima usingizi?wakati kila kitu mnacho?ndege ya sita inaingia leo what is your problem?
Walituahidi viwanda tuliambiwa nchi itakua na viwanda kama Canada naona unjenzi wa viwanda umekamilika
 
Kwa ushauri wangu katika kesi hiyo awaunganishe na Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, pamoja na idara ya uhamiaji kwa kushindwa kufanya majukumu yao ya kumbaini mtu ambaye sio raia. Sijajua vizuri elimu ya mtu aliyeibua tuhuma hizi, ila naamini sio ya kiwango cha kusoma na kuandika.
nazani atakuwa amefikia kiwangi cha mwisho kabisa cha kufikiri
 
Nina mashaka kama kuna kazi kwa sasa katika ofisi zetu za kiutawala katika ngazi za Wilaya hasa kwa hawa vijana. Huyu baada ya kuwa mbunifu kuwasaidia vijana wetu wa CCM wanaoteswa na ukosefu wa ajira yeye anapigana na akina Zito Kabwe as if ndio agenda yetu ya Chama. Kijana amepata ajira CCM ya Ukatibu wa Wilaya baada afanye yenye manufaa anaanza ujinga. Hasara kabisa huyu kijana maana uraia wa Zito unawezaje kutatua matatizo tuliyo nayo kwa vijana wetu wa CCM.
Mkuu mtoto nyumbani huwa anaangalia baba yake au mama yake huwa anafanya nini, kama baba ni seremala na mtoto kidogo kidogo ataanza kushika nyundo au msumeno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mheshimiwa Katibu inawezekana una hoja, ila chama cha mapinduzi kinaamini katika umoja na undugu kiasi kwamba mwalimu Nyerere alitamani sana kuona kuwa Afrika ni moja. Hoja ya kutaja na kuona kuwa uraia wa Zito ni tatizo ni hoja inayotolewa na wabaguzi tu ambayo Tanzania kutokana na misingi yake inategemewa na kila mtu iwe ya mwisho katika ubaguzi wa namna hiyo. Wapo viongozi wengi ambao walishawahi kutumikia madaraka makubwa ambapo hata kuwatazama tu unaweza kugundua kuwa sio raia wa nchi hii, ila Tanzania iliyoachwa na Mwalimu haikujali hilo kikubwa ni kufanya kazi kwa bidii na kuwatumikia wananchi. Tuhuma hizi ziwe ni zakweli au uongo hatufikirii kabisa kwamba mwana CCM anaweza kutamka ubaguzi huu. CCM ni chama chenye historia iliyotukuka ila ikivumilia hawa vijana wenye kupenda kiki imeisha.

Na kama unakumbuka mwenye kuleta hoja za uraia ni huyu huyu mhutu
 
Che Nkapa ndie alianza hayo maujinga. LAKINI Alipoletewa cheti chake cha kuzaliwa kilichoandikwa kwa kireno. Na pia KUKUMBUSHWA kuwa Baba yake Nze Makota alihamia toka Nchumbiji, wakati Ben akiwa na miaka 3/4, kuanzia hapo ndio akaacha maujinga hayo, na akanyamaza.
Viongozi wakuu wa CCM wa sasa wote uraia wao na hata kwa sura zao vinatia shaka.
Sawa UVCCM, ENTER the dragon.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Che Nkapa ndie alianza hayo maujinga. Alipoletewa cheti chake cha kuzaliwa kilichoandikwa kwa kireno. Na pia Baba yake Nze Makota alihamia toka Nchumbiji, Ben akiwa na miaka 3/4. Kuanzia hapo ndio akaacha maujinga hayo, akanyamaza.
Viongozi wakuu wa CCM wa sasa wote uraia wao na hata kwa sura zao vinatia shaka.
Sawa UVCCM, ENTER the dragon.

Sent using Jamii Forums mobile app
kwahiyo mzee nkapa cheti yake ya kuzariwa imeandikwa kwa kireno
 
Aliyekuwa Katibu wa (UVCCM) mkoa wa Kigoma ambaye kwasasa amehamishiwa wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, Agustino Matefu amesema kuwa atamburuza mahakamani mbunge wa Kigoma mjini kupitia chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe kwa madai kuwa sio raia wa Tanzania,

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amedai kuwa ushahidi wote anao.

“Kwasasa nimeamua kwenda mahakamani kumfungulia kesi Zitto Kabwe, sababu sio raia wa Tanzania, nimesafirisha wazee wanne kutoka Kigoma kwa ajili ya kutoa ushahidi,”amesema Matefu
Angeanza na mwenyekiti wa chama chake, kuna ushahidi wa kutosha kuwa ni mhutu kutoka nchi jirani
 
Back
Top Bottom