Uraia wa Zitto Kabwe sasa kuamuliwa Mahakamani

Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
4,512
6,856
Aliyekuwa Katibu wa (UVCCM) mkoa wa Kigoma ambaye kwasasa amehamishiwa wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, Agustino Matefu amesema kuwa atamburuza mahakamani mbunge wa Kigoma mjini kupitia chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe kwa madai kuwa sio raia wa Tanzania,

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amedai kuwa ushahidi wote anao.

“Kwasasa nimeamua kwenda mahakamani kumfungulia kesi Zitto Kabwe, sababu sio raia wa Tanzania, nimesafirisha wazee wanne kutoka Kigoma kwa ajili ya kutoa ushahidi,”amesema Matefu
 
Nina mashaka kama kuna kazi kwa sasa katika ofisi zetu za kiutawala katika ngazi za Wilaya hasa kwa hawa vijana. Huyu baada ya kuwa mbunifu kuwasaidia vijana wetu wa CCM wanaoteswa na ukosefu wa ajira yeye anapigana na akina Zito Kabwe as if ndio agenda yetu ya Chama. Kijana amepata ajira CCM ya Ukatibu wa Wilaya baada afanye yenye manufaa anaanza ujinga. Hasara kabisa huyu kijana maana uraia wa Zito unawezaje kutatua matatizo tuliyo nayo kwa vijana wetu wa CCM.
 
Kwa hiyo wanataka kumrudisha Rwanda au Burundi!CCM tuache hizo ,sisi tupige kazi,tunajichora tu na uraia wa Zitto .Ok sema sasa Zitto sio raia ,then mtamyamazisha?hata mkimpeleka nchi aliyozaliwa au kwenye uraia wake ndio kwanza ataongea Zaidi.ACHENI KUJICHORA,TUFANYE KAZI.Yeye Zitto achene aendelee kuongea kwani anawanyima usingizi?wakati kila kitu mnacho?ndege ya sita inaingia leo what is your problem?
 
Hivi ccm hamna kazi za kufanya? kila mtu akiwa na msimamo hasi na ccm sio Raia kwani hata wewe tutaaminije kuwa ni raia? shughulikiani mambo ya msingi kwa watanzania wana matatizo mengi sana
Aliyekuwa Katibu wa (UVCCM) mkoa wa Kigoma ambaye kwasasa amehamishiwa wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, Agustino Matefu amesema kuwa atamburuza mahakamani mbunge wa Kigoma mjini kupitia chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe kwa madai kuwa sio raia wa Tanzania,

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amedai kuwa ushahidi wote anao.

“Kwasasa nimeamua kwenda mahakamani kumfungulia kesi Zitto Kabwe, sababu sio raia wa Tanzania, nimesafirisha wazee wanne kutoka Kigoma kwa ajili ya kutoa ushahidi,”amesema Matefu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Augustino Matefu na mzee Likwepa ndio hadi sasa hawajapata juteuzi wa Rais Magufuli kati ya wale vijana wa CCM waliokuwa hawakosi kuhudhuria kipindi cha malumbano ya hoja pale ITV.

Yawezekana Matefu anautafuta udc wa Arusha kwa kutumia mbeleko ya Zitto Kabwe.

Lakini hata jina la Matefu ni Wanyasa wa Malawi hawa aangalie yasije kuwa ya " mchimba kisima"
 
Vigezo vya kumjua raia wa Tz ni rahisi sana. Kwanza, ajue kuimba wimbo wa taifa, pili awe na kovu la sindano ya ndui kwenye mkono wa kulia.
 
Mheshimiwa Katibu inawezekana una hoja, ila chama cha mapinduzi kinaamini katika umoja na undugu kiasi kwamba mwalimu Nyerere alitamani sana kuona kuwa Afrika ni moja. Hoja ya kutaja na kuona kuwa uraia wa Zito ni tatizo ni hoja inayotolewa na wabaguzi tu ambayo Tanzania kutokana na misingi yake inategemewa na kila mtu iwe ya mwisho katika ubaguzi wa namna hiyo. Wapo viongozi wengi ambao walishawahi kutumikia madaraka makubwa ambapo hata kuwatazama tu unaweza kugundua kuwa sio raia wa nchi hii, ila Tanzania iliyoachwa na Mwalimu haikujali hilo kikubwa ni kufanya kazi kwa bidii na kuwatumikia wananchi. Tuhuma hizi ziwe ni zakweli au uongo hatufikirii kabisa kwamba mwana CCM anaweza kutamka ubaguzi huu. CCM ni chama chenye historia iliyotukuka ila ikivumilia hawa vijana wenye kupenda kiki imeisha.
 
Aliyekuwa Katibu wa (UVCCM) mkoa wa Kigoma ambaye kwasasa amehamishiwa wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, Agustino Matefu amesema kuwa atamburuza mahakamani mbunge wa Kigoma mjini kupitia chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe kwa madai kuwa sio raia wa Tanzania,

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amedai kuwa ushahidi wote anao.

“Kwasasa nimeamua kwenda mahakamani kumfungulia kesi Zitto Kabwe, sababu sio raia wa Tanzania, nimesafirisha wazee wanne kutoka Kigoma kwa ajili ya kutoa ushahidi,”amesema Matefu
huyu atakuwa mwita wa kidengereko maana hakuna mwita wa mara muoga na mjinga hivi au baba mkurya na mama mdengereko naye amelelewa sana upande wa ukeni,hakuna wakurya wala wakizu wajinga wajinga hivi
 
sasa kosa langu nini hapo mbona munawaaibisha walimu wenu mimi sijaenda mahakamani kumshtaki zitto
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom