Uraia wa Siyoi: Joshua Nassari akata Rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Baada ya CHADEMA kupiti kwa mgombea wake Joshua Nassari kumpinga Siyoi kuwa siyo raia wa Tanzania, Mkurugenzi wa Uchaguzi jimbo la Arumeru ametupilia mbali pingamizi iliyowekwa na wagombea wa upinzani. Hata hivyo Nassari amekata rufaa tume ya uchaguzi ngazi ya taifa. Amesisitiza vielelezo vyote vipo wazi kuwa Siyoi Sumari siyo Raia wa Tanzania. Source TBC1
 
Ni ajabu na aibu ya serikali ya ccm. Mkurugenzi ametupilia mbali pingamizi bila kufafanua au kuridhisha umma kwamba Siyoi Sumari ni Raia wa Tanzania. Itafikia mahali wageni wanakuja kujichotea uongozi bila kuhojiwa. Ninachokiona kwa ccm ni kuwa kama una pesa zako wewe ni kiongozi. Sijui ilikuwaje akina Azim Premji wakahojiwa uraia wakati mtu kama Siyoi hata ardhi ya Arumeru haijui.
 
uraia wa siyoi wa Tanzania ulikwisha mara alipofikisha miaka 18. hili ni kosa wanalolifanya watu wengi kuishi kwa mazoea endapo hakwenda kuukana uraia wa kenya mara alipotimiza miaka 18 basi atakuwa bado na uraia wa kenya kwani Tanzania bado haijaridhia dual citizenship.
 
Mh haya maisha bwana na je asingetangaza nia si kusingekuwako na hizi purukushani,serikali ina jukumu la kuelimisha raia wake juu ya haya,anyway time is the answer,
 
Mh haya maisha bwana na je asingetangaza nia si kusingekuwako na hizi purukushani,serikali ina jukumu la kuelimisha raia wake juu ya haya,anyway time is the answer,

suala siyo angetangaza ama asingetangaza. Suala ni katiba yetu inaeleza sifa gani anatakiwa kuwa nazo mtu anayeomba ridhaa ya kuwa kiongozi, hususana ubunge.
 
Hata ccm wakimtetea jamani haitutishi ccm meru haipiti labda kwa kuiba kura

hapa suala la msingi siyo kushinda au kushindwa. Suala ni je katiba ya jamhuri ya muungano imefuatwa inavyotakiwa?
 
Sioni mantiki ya hiyo rufaa! Box la kura litaamua jamani.

ni kweli box la kura litaamua. Lakini litakuwa limeamua huku katiba yetu ikipindishwa. Hapa ndipo ninapokumbuka signature ya member inayosomeka "don't break the law, just bend it"
 
Wameru muwe makini ktk uchaguzi huu mdogo msichague mzamiaji,chagueni mtu mwenge uzalendo na raia halisi.Mkichagua Mkenya mtakuja kujuta wenyewe.
 
kwa hiyo huyo aliyetupilia mbali hilo pingamizi anataka kutueleza kuwa watu wana uhuru wa kumchagua mkikuyu kutoka kenya pande za nyeri
 
Cyoi hoi , mawazo, analiwazwa na wazee kadhaa anambiwa ucwaze, ukikosa ujakosa maisha. Utakoma kujaribu. (source- mgangawangu mmoja mweusi kinoma)
 
Ni ajabu na aibu ya serikali ya ccm. Mkurugenzi ametupilia mbali pingamizi bila kufafanua au kuridhisha umma kwamba Siyoi Sumari ni Raia wa Tanzania. Itafikia mahali wageni wanakuja kujichotea uongozi bila kuhojiwa. Ninachokiona kwa ccm ni kuwa kama una pesa zako wewe ni kiongozi. Sijui ilikuwaje akina Azim Premji wakahojiwa uraia wakati mtu kama Siyoi hata ardhi ya Arumeru haijui.

Kama hakuwa na maelezo ya kuridhisha kwahiyo kachoma mafuta na posho bure huku akiwa na jibu tayari.
 
upo sahihi kabisa lakini siku zote serikali walikuwa wapi?sio mpaka mtu atangaze anagombea nafasi fulani ndiyo historia iibuke wanatakiwa wajue tena kinachoonyesha kabisa uzembe ni pale serikali inayoongoza nchi hii haina habari juu ya hili hadi waambiwe au ni kuwapima wananchi?mi nafikiri ulegevu katika serikali ndio chanzo cha haya yote.
 
ilikuwa siri kubwa sana ya serikali. Walitaka kunyamazia. Shukrani kwa RC wetu mpendwa. Alitusaidia kuuweka uhuni wa ccm ya Lowassa hadharani.
 
Siyoi ni raia wa Tanzania.

labda leo ndiyo kaukana uraia wa kenya. Na kama ndiyo kaukana leo sheria inasemaje kuhusu mtu aliyepewa uraia leo? Anatakiwa akae muda gani ndiyo aombe ridhaa ya wananchi?
 
Ndugu zangu wa arumeru muwe macho sana, ntawashangaa kama mtapanga foleni na kuspend mda mrefu kwa ajili ya kupiga kura halafu mumchague mkenya, huyu sioi hajawai kuukana uraia wa kenya, duh mtalishangaza taifa
 
labda leo ndiyo kaukana uraia wa kenya. Na kama ndiyo kaukana leo sheria inasemaje kuhusu mtu aliyepewa uraia leo? Anatakiwa akae muda gani ndiyo aombe ridhaa ya wananchi?
Hana mzazi mkenya... je aliupataje huo uraia?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom