Uraia wa nchi mbili waipatia ushindi Ghana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uraia wa nchi mbili waipatia ushindi Ghana

Discussion in 'Sports' started by Zawadi Ngoda, Jun 27, 2010.

 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Kevin-Prince Boateng ni raia wa Ghana na Ujerurumani, kwa vile baba yake ni Mghana na Mama yake ni Mjerumani. Mchezaji huyu alikuwa akiichezea timu ya vijana ya Ujerumani na alikuwa tegemeo kubwa sana kwa timu hiyo.

  Ni tarehe 5 mwezi wa 6 mwaka huu ndio Uzalendo wa Ghana ulipomzidi na kuamua kuifungia pasport ya Ujerumani katika sanduku na Kuiinua mbele ile pasport ya Ghana na kuamua kuichezea Ghana katika kombe la Dunia. Uamuzi wake ulimkatisha tamaa sana kocha wa ujerumani ambaye alikuwa na mipango mahsusi juu ya maisha ya soka ya mchezaji huyu ndani ya Ujerumani. Lakini kwa vile ana haki ya kisheria ya kuchagua ni nchi gani achezee, bado uamuzi unakuwa ni wa kwake mwenyewe.

  Leo Ghana ndio nchi pekee miongoni mwa nchi za Afrika ambayo imefanikiwa kufikia 1/8 na hatimaye 1/4 fainali kwa msaada wa goli la kwanza la Mjerumani/Mghana Kevin-Prince Boateng. Faida kama hizi zitokanazo na uraia wa nchi mbili ni nyingi katika maeneo tofauti hasa katika wakati huu wa utandawazi. Na kwa maana hii ndio maana nchi nyingi za Afrika kwa miaka mingi zilisharuhusu uraia wa nchi mbili.

  Kama Ghana ingefunga milango kwa waghana waishio nje kama Tanzania, basi kamwe isingeweza kuitumia nafasi hiyo. Hii ni fundisho kubwa kwa Tanzania ambaye suala la Uraia wa nchi mbili limekiuwa likizungumziwa kwa takriban zaidi ya miaka 10, na kupoteza faida nyingi ambazo nchi yetu ingepata. Uamuzi wa Serikali uliotangazwa na Waziri wa mambo ya nje, Mheshimiwa Membe ni uamuzi wa busara. Lakini ni lazima tuendelee kuwaelimisha watanzania waliokuwa wakifikiri eti ni Watanzania wenye asili ya kihindi tu ndio wataofaidika zaidi. Hii si kweli, na mfano halisi ni kama tulivyoona Nchini Ghana.

  Ninachoiomba serikali isipoteze muda mrefu katika kutia maamuzi muhimu kama haya na mengineyo ambayo seriali haihitaji kutumia pesa nyingi kufikia maamuzihayo. Ni vikao kadhaa tu vya bunge vinatosha kupitisha mswaada kama huo kwa kipindi cha mwaka mmoja tu na sio zaidi ya miaka kumi. Lazima tujue kuwa wakati wenzetu wanatembea yabidi sisi tukimbie ili angalau kuwakaribia.

  Ushindi wa Ghana ni ushindi kwa Afrika na ni mfano kwa Tanzania. Ili tuendelee kwa kasi ni muhimu tujifunze toka kwa wenzetu vile vile. Hii ndio faida ya Utandawazi.
   
 2. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Sijakupata yaani unataka Tanzania ihamasike na Dual Citizenship kwa ushindi wa Ghana through Kevin?
   
 3. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Kevin-Prince Boateng alisaidia ushindi ila Asamoah Gyan ndiye aliyekamilisha karamu ya ushindi!..halafu mechi zote za Ghana kwenye hii WC nilikuwa namwangalia sana Prince sasa nimemuelewa,katulia!..ana mapenzi zaidi na Ghana kuliko Germany,whaao!!
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  ..Not that copy-cat meaning mkuu, lakini huo ni mfano mdogo tu wa faida za dual citizenship...Kwamba mtu anachagua ni nchi gani patamfanya atumike kwa faida zaidi kwa wakati huo...Mfano nchi za baridi kali nadhani economy ina'slow down kwsa kiasi kikubwa wakati wa baridi, so one could go to another country(not necessarily as a tourist) for continuation of his career!
   
 5. n

  nndondo JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  Nadhani kwenye mambo ya msingi kama ya uraia wa nchi mbili tunahitaji analysis za ndani zaidi ya ushindi wa Ghana. Sikubaliani na hoja iliyotolewa na Zawadi kwamba ndio inatosha kufanya nchi kama Tz kuingia katika maamuzi makubwa kama uraia wa nchi mbili. Kwa sasa sijaona mtanzania yoyote aliyeshindwa kuja nyumbani kufanya mambo makubwa kwa sababu hana uraia wa nchi mbili. Ninachoona ni pengo la kuzidi kuwakandamiza watanzania mamilioni wa kawaida ambao tayari rushwa inawatosha kuwamaliza kwa kutoa fursa chache za kwao kwa watu ambao hawazihitiji na hawataweza kushindana nao kama wataondolewa hiyo protection ya kuwa raia. Bado mpaka sasa hatujaambiwa ni watanzania gani wanaoshindwa kuifanyia makubwa nchi yao kwa kuwa wamelazima kujivua utanzania kwa sababu ya maslahi na sasa wanataka kuyeleta maslahi hayo nyumbani. Mtanzania mwenye nafasi kimataifa hahitaji uraia wa nchi hizo anazofanyia maajabu, kwa kuwa kama wanajua thamani yake watahalalisha ukazi wake kwa namna stahiki. Hawa tunaowatetea leo wala sio watakaofaidika kama huu umamuzi utafanyika kwa analysis za namna hii. Hivi kwa nini hamfikirii ni wahindi wangapi watakoogelea kuiningia huku kwa uraia wa nchi kumi, na kutumaliza kabisa kiuchumi? Mimi nadhani swala la diaspora liangaliwe kwa upana na watu wenye akili zaidi ya hiki cha roadshow cha sasa. Na sisi pia tumepata bahati ya kuwa nje ya nchi je mmeangalia profile ya mashabiki wa diaspora huku nje? ni wale wanoishia kufungua matawi ya CCM huku na kule wala sijaona bado taarifa ya majina ya watanzania wanaofanya mambo makubwa katika hizi nchi yakipangwa kwenye hizo diasspora. Pili tuache kuwa cheap ushindi wa Ghana ni wa Ghana na sio wa Afrika. Gone are the days za siasa zisizokua za maana. Waacheni wa Ghana wapete nyie endeleeni na maamuzi yenu ya kisiasa ya kuleta team ya brazil na leo hii hata unyoya wafaida ya hicho kitendo hatuuoni. Haya ndio ya kuyaangalia kwenye soccer leo hii sio maswala ya kutaka share ya ushindi wa watu waliofanya maamuzi magumu katika investment wakati sisi tunacheza
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,708
  Trophy Points: 280
  Watanzania wanaofanya mambo makubwa katika nchi mbali mbali wapo lakini hawapendi publicist hivyo ndiyo maana hawasikiki. Nadhani Membe au maofisa wa Foreign Affairs (w)alitembelea baadhi ya nchi za Africa na Carribean ambazo zinaruhusu uraia wa nchi mbili na huko walijaribu kuulizia faida na hasara za uraia wa nchi mbili. Katika nchi zote hizo (w)alifahamishwa kwamba faida ni nyingi mno kuliko hasara na hizi info zilitumika katika kufikia uamuzi wa kuruhusu uraia wa nchi mbili. Sasa sijui kama uraia wa nchi mbili utaruhusiwa kweli kama ilivyotangazwa au la, maana bado kuna waheshimiwa wengi bado wanapinga sana hili la uraia wa nchi mbili.
   
 7. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Gunia la pipi kamwe halinunuliwi na mtu mmoja. Hapa ninamaanisha kuwa ukuzaji wa uchumi wa nchi yetu unategemea kwa kila mtanzania na kwa kila sekta kushiriki katika kudondosha tone moja moja la shilingi ndani ya nchi yake. Michezo ni moja kati ya sekta nyingi ambazo zimejitokeza kutoa ajira kwa vijana leo hii na ukiwa na kiwango kizuri kipato chake si haba.

  Hivyo nimeandika hapa faida dhahili iliyoonekana na watanzania wote kwa upande wa Ghana kama mfano. Na kwa vile nimeandika upande wa Michezo sikutaka kutoka nje ya eneo hilo kwa kuandika faida nyingine kama elimu, kilimo, tamaduni, biashara n.k. Ukihitaji hiyo nitaifungulia thread katika eneo la Uchumi. Kwa mfano raia wa Ghana walio nje ya nchi wanaingiza nchini Ghana 2.5 bilioni za dola kila mwaka.

  Unasema watanzania wenye uraia wa nchi nyingine wanaweza kufanya shughuli yeyote Tanzania bila kubughudhiwa. Hivi unazijua sheria za uhamiaji Tanzania au unasema tu? Usije ukafikiri kuwa kama jana uliiba na hakuna aliyekushtaki basi Tanzania unaweza kuiba na ukaendelea kuishi kwa usalama tu. Hivi Mtanzania mwenye uraia wa Uingereza, ikiwa ana kiwango cha kimataifa cha soka anaweza kuchezea timu ya Taifa ya Tanzania? Au anaweza kwenda kugombea ubunge SAME? Zifuatilie vizuri sheria za UHAMIAJI ZA Tanzania kabla hujajibu.

  Vinginevyo nakusihi u-google na kuangalia jinsi nchi za Afrika zinavyofaidi na uraia wa nchi mbili.
   
 8. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Ujinga mtupu swala la uraia wa nchi mbili na ushindi wa ghana havihusiani hata kidogo msilete shobo hapa
   
 9. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Yaaa! Nakuelewa kabisa, kwani watanzania ni wagumu kuelewa kuwa mtu mmoja anaweza akabadilisha kabisa hali ya maisha ya watu duniani.

  Kuna watu wanafikiri kwamba bila hata Einshtein na Isack Newton Dunia ingefika hapa tulipo kiteknolojia. Ukiwauliza wenzetu kama Wamarekani watakwambia nafasi ya Abraham lincoln kama Abraham Lincoln ni Nani na nafasi yake katika Amerika ni ipi? Na kama asingekuwa yeye pengine Amerika isingekuwa hivi ilivyo sasa.

  Rom, latin Amerika, Uturuki zilisikikaka nyakati zake sasa hivi ziko wapi.

  Mwisho napenda kukueleza kuwa maendeleo ya Ghana yameanzia na reforms za Jerry Rowlings (mtu mmoja), upende usipende huo ndio ukweli. Tuna hitaji akina Jerry Rowlings Tanzania katika kila sekta ili tusonge mbele.

  Kama huamini kuwa Goli la kwanza ndio liloleta jumla ya magoli mawili, na kuifanya Ghana Mshindi basi nimeishiwa na hoja. Kwaheri.
   
Loading...