BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,849
Kwa taarifa tu, mimi naunga mkono uraia wa nchi mbili kwa sababu faida za uraia wa nchi mbili especially kwa Watanzania waliohamia nchi za nje na watoto wao ili kutafuta maslahi zaidi ya kimaisha ni kubwa mno kuliko hasara. Wanaochukua uraia nchi nyingine hawafanyi hivyo kwa kuuchukia Utanzania bali kujiweka katika nafasi nzuri ili kupata kazi mbali mbali ambazo nyingine ni kwa ajili ya raia wa nchi tu na pia kuepuka kuathirika na sheria za uhamiaji wa nchi hizo ambazo zinabadilika kila kukicha.
Uraia wa nchi mbili utaangamiza nchi, uzalendo
Joseph Mihangwa Julai 30, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo
MNAOJALI kusoma historia na kazi za uandishi za watu wenye uchungu na nchi yao, msikieni Shaaban Robert katika shairi lake, "Fahari ya mtu", akisema:
"Fahari ya kila mtu, kwanza ni taifa lake,
Kutimiza wake utu, afe au aokoe,
Pasipo hofu ya kitu, halipendi liondoke
Fahari ya kila mtu, ya pili nchi yake,
Mtu hakubali katu, kutawaliwa pake,
Hilo haliwi kantu, halina heshima kwake.
Fahari ya kila mtu, ya tatu ni nchi yake,
Kuwaye chini ya watu, wageni wa nchi yake,
Ni jambo gumu kwa mtu, japo vipi aridhikie,
Pasipo hofu ya kitu, hulipenda liondoke".
Ni jambo la kuhuzunisha na kugadhabisha pia, kuona zama hizi, baadhi ya Watanzania wenzetu, hasa wanasiasa, wametekwa nyara na ubepari na mitaji ya kimataifa kiasi cha kupoteza uzalendo na moyo wa kuona fahari kwa taifa lao na kuabudu vya nje.
Na kwa kuwa Watanzania walio wengi hawana kiwewe na vya nje, wala fikra kwamba siku moja watafika au kuishi Ughaibuni; wananchi sasa wanaanza kuona ufa uliopo unavyozidi kupanuka kati yao na viongozi wao wenye kuabudu vya nje, badala ya kushikamana na wanaowaongoza kwa matatizo, mafanikio na kwa kila kilicho cha nchi hii.
Wananchi wanaanza kutambua kwamba, wao na viongozi wao hawaabudu kwenye madhabahu moja, wala hawachangii sala. Wakati sala ya wananchi kwa mama Tanzania ni kuona maendeleo ya nchi yao waliyoitolea jasho wakati wa kupigania uhuru na ustawi wa jamii, sala ya viongozi wao ni tofauti, inasema hivi:
"Baba yetu uliyeko Ulaya na Amerika,
Jina lako litukuzwe, ufalme wako uje,
Utakalo lifanyike katika Tanzania yetu tajiri kama huko uliko,
Mapenzi yetu ya kukukaribisha nchini yatimie,
Kama tulivyokukaribisha wakati wa ukoloni,
Tupatie riziki yetu ya kila siku,Mapesa ya dola,
kwa kuwa vishilingi vyetu si thamani tena.
Tusamehe kwa mapungufu na udhaifu wetu kiuchumi na kisiasa.
Tusaidie kuwanyuka, kuwashinda wote wanaokusakama
Kwa kupora utajiri wa nchi yetu, eti huo ni ukoloni maboleo.
Tusaidie kuwanyuka ipasavyo wanahabari wa nchi yetu,
Kwa makeke na kidomo domo chao.
Fadhili kutungwa Sheria ya kuwabana, wakome.
Tupe nguvu, utukufu na misaada tele;
Utujalie moyo wa kukupenda wewe tegemeo letu,
Tufanye wanyeyekevu na wenye shukrani;
Milele na milele, Amina.
Watanzania wengi wamestushwa na kugadhabishwa na taarifa ya Serikali kwamba inakusudia kuwasilisha bungeni muswada wa sheria kuruhusu uraia wa nchi mbili (dual citizenship). Akijibu swali la Mbunge Mwadini Abbas Jecha wa Wete, wakati wa kikao cha 12 cha Bunge, mjini Dodoma, hivi karibuni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Khamis Kagasheki, alisema, anawahurumia "Watanzania wengi walioko nje waliopoteza uraia wao kwa kutokuwapo sheria hii", hivyo lazima wasaidiwe.
Watetezi wa muswada huu wanadai kuwa, Sheria hiyo itawasaidia mabilionea wa Kitanzania waliochukua uraia wa kigeni kurejea nchini na "vijisenti" vyao na kutoa msisimko kwa uchumi wa nchi; na pia kwamba raia wa kigeni wenye mitaji wataweza kuchukua uraia hapa nchini bila kutakiwa kufuta uraia wa nchi zao, wakiishi nchini, bila wasi wasi kuliko ilivyo sasa.
Kuna maswali mengi yanayotaka majibu juu ya muswada huu: Uraia wa nchi mbili utamsaidiaje Mtanzania wa kawaida kwa kugawana uraia na wageni? Kwa nini muswada huu unaletwa leo na si miaka iliyopita?
Tanzania imebarikiwa kwa utajiri mkubwa wa maliasili za aina mbali mbali; imefungua milango kwa wawekezaji hadi upana wote wa bawaba. Je muswada huu si kuruhusu "Wageni kupigana vikumbo" (scramble) kugombea rasilimali za Tanzania, kama enzi za kina Karl Peters, Cecil Rhodes na wengine, mwanzoni mwa ukoloni barani Afrika? Nini hatima ya yote haya?
Tunaambiwa, dunia sasa ni kama kijiji ambapo watu wanaweza kuwekeza na kufanyakazi popote. Je, kwa muswada huu si kujikanganya na dhana hiyo ya "utandawazi" ambayo tayari tumeipokea kwa pupa bila kuelewa madhara yake? Wanaotetea utandawazi na kututaka turuhusu uraia wa nchi mbili kwa manufaa ya wenye mitaji, wanaitakia nini nchi yetu na uzalendo uliosimikwa na waasisi wa Taifa hili?
Haya ni maswali magumu yanayotaka ukomavu wa kisiasa kuyatolea majibu sahihi kuweza kuwaridhisha wazalendo wa nchi hii. Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha na Naibu wake Kagasheki, wanaweza wasilijue hili, na hivyo kuonekana wepesi wa kusali bila kuhoji, "Baba yetu uliyeko Ulaya na Amerika…..", lakini wasubiri hisia za wananchi wazalendo, pale watakapowasilisha muswada huo tata bungeni. Kusema kweli wanajitengenezea baruti.
Tunaamini muswada huo haukubuniwa na wazalendo wenye kutetea na kujivunia fahari ya taifa na kwa maslahi ya walio wengi, bali chimbuko lake ni watu wenye matanuzi, wenye kuchumia kivulini na kulia kivulini, wakiwamo wazalendo mamluki wasioweka mbele maslahi ya taifa, wakishirikiana na kina Karl Peters wa zama hizi, kila mmoja akiwania kwa staili yake kujinufaisha na maliasili za nchi hii.
Ni matokeo ya fungate ya "uwili mtakatifu" kati ya ubeperi wa kimatifa kwa kufunga ndoa na siasa za nchi hii na kwa viongozi kutumika kama mkondo (conduit) wa kuingiza ukoloni mpya (na kwa historia kujirudia) kwa kujali zaidi maendeleo ya miradi kuliko maendeleo ya watu. Huu ni uhaini ulio dhahiri.
Sheria hii itawawezesha wageni kupata haki zote za kiraia sawa na Wazalendo; lakini wao (wageni) kwa shabaha ya kuifanya nchi kuwa kituo cha "kuwekeza" na kupora uchumi wa nchi, wakirandaranda kati ya nchi na nchi wasiweze kukamatika kwa urahisi iwapo watahusishwa na hujuma nchini.
Wako wapi akina Jeetu Patel (kashfa ya EPA), Saileth Vithlani (kashfa ya rada), Chavda na wengine, ambao tuliwakubali kama raia wenzetu, na mwisho wa yote wakatupora wasikamatike? Tuambieni, ni raia gani wa aina hiyo ameonyesha fahari kwa taifa, na aliye tayari kuitetea nchi kwa lolote, kama hawa si mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo? Tuambieni, nani kati yao, au watoto wao ameshiriki kujenga nchi kama afisa kilimo, polisi au mwanajeshi?
Baadhi ya wazalendo wachache wanaotetea muswada huu ni wale waliowatelekeza Watanzania, wakakimbilia nje na kuwaacha wakipambana na ujenzi wa nchi yao wanayoipenda; au ni wale waliojiunga na ufisadi wa kimataifa na kutumika kama mawakala wa ufisadi nchini.
Hawa hawana Watanzania na nchi moyoni mwao. Wanaona bora sheria hii ipite, ili wanachopora na watakachopora kwa kushirikiana na wageni (ambao nao sasa watapewa uraia) waweze kuwekeza nje na kukimbilia huko mambo yanapowaharibikia. Ni uasi, uzandiki na umamluki ulioje kwa Mtanzania wa aina hii. Wasaliti hawa.
Hivi Watanzania tumelogwa? Kwamba wakati hatujatatua "mgogoro" wa kuwapo kwa "Wazanzibari na Watanzania, au Wazanzibari na Wazanzibara, tunajibebesha hima mzigo mwingine mkubwa zaidi wa "uraia wa nchi mbili"!
Fahari ya mzalendo wa kweli ni taifa lake, na ambalo kwake anapaswa kutimiza wajibu wake; yupo tayari kulitetea na kulifia. Tuambieni, mtu mwenye uraia wa nchi mbili ataimbaje "Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote?", wakati moyo wake umegawanyika kwa "mapenzi" ya nchi mbili? Atawezaje kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja?
Tunasema wanaotetea muswada huu hawana lengo la kutumikia taifa na watu wake, bali agenda yao ni kupora utajiri na maliasili za taifa hili.
Na kwa kuwa sheria hii itawapa wageni haki sawa za kiraia na wazalendo, tusishangae siku moja nchi hii ikatawaliwa na Rais "Mtanzania" kutoka Japan, Waziri Mkuu "Mtanzania" kutoka China, au Spika wa Bunge "Mtanzania" kutoka Iran, Irak au Canada. Utawazuiaje kutawala wakati nao watakuwa ni Watanzania bila kutuhumiwa kuvunja Katiba ya nchi kwa ubaguzi wa rangi na wa asili ya mtu? (Angalia ibara 13(2) na (5) ya Katiba , 1977).
Kwa wanaosoma historia ya nchi hii, watakubali kwamba suala la uraia ni jambo nyeti tangu enzi za uhuru na ambalo lilitaka kumgharimu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere nafasi ya urais wa nchi hii, mwaka 1962. Mwaka 1961 Serikali, chini ya Waziri Mkuu Nyerere, iliwasilisha muswada wa uraia kwa watu wote bila kubagua rangi au asili ya mtu, mradi tu awe amezaliwa au mmoja wa wazazi wake awe amezaliwa Tanganyika.
Muswada huo ulipita kwa upinzani mkali wa wabunge na wananchi, waliotaka uraia uwe kwa Waafrika tu ambao ndio wenye nchi na wenye kustahili kufaidi matunda ya uhuru.
Kwa kukerwa na sheria hiyo, chama tawala cha "Tanganyika African National Union" (TANU) kiliitisha Mkutano Mkuu, Januari 16, 1962 ambapo wajumbe walimshambulia na kumlaumu Nyerere, wakishinikiza kuona maendeleo ya haraka, kuanzishwa kwa Jamhuri ya Tanganyika, kufutwa kwa viti 20 maalumu kwa weupe Bungeni (minority races) wenye uraia wa nchi mbili, na kutoa madaraka kwa Waafrika katika utumishi wa umma na vyama vya Ushirika.
Wakati mkutano huo ukiitishwa, tayari TANU ilikuwa imeanza kugawanyika na wanachama wengine kuunda Chama cha "The Nationalist Enterprises Party" (NEP).
Kwa kutetea msimamo wake, na hasa kutokana na kile kilichoitwa "kukosa ujasiri wa kuwatimua Waingereza kwa kasi iliyotakikana", ilibidi Mwalimu aachie ngazi na kuwaachia Rashid Kawawa na Oscar Kambona kuwaondoa Wazungu kwenye vyeo walivyokuwa wakishikilia.
Uraia wa nchi mbili ni chukizo linalolenga kuigeuza Tanzania kuwa "Shamba la Bibi"; ni hatari pia kwa uchumi wa nchi, uzalendo; na umoja wa kitaifa. Ni sheria ya kudhalilisha wazalendo na uzalendo. Mwenye masikio na asikie, Watanzania wanaisubiri siku ya muswada huo.
0713-526972
jmihangwa@yahoo.com