Saidi Yakubu
Member
- Mar 6, 2006
- 33
- 27
Naam wanajukwaa
Nafurahi kujiunga na JF, nachukulia jukwaa hili kama ni sehemu ya kujifunza.
Takwimu za tanzania zinaonyesha kuwa kuna watanzania zaidi ya 1.2m wanaoishi nje ya nchi [rejea ripoti ya Tanzania Law Review Commission]. Naam hii ni karibu 3% ya taifa zima.
Nadhani wakati umefika sasa serikali ikapitisha sheria kuruhusu raia hawa kuweza kufaidi matunda ya uraia wa nchi mbili kwani kwa sasa wengi wanakwazwa na kuwa wakiamua kuchukua uraia mwingine inabidi waamue kuachia uzalendo wao.
Swali hili niliwahi kumuuliza mheshimiwa Sumaye alipokuja hapa Uingereza mwaka jana akakiri kuwa ni muhimu kuruhusu lakini hakuweza kutoa sababu kwa nini hasa mpaka sasa Tanzania imeshindwa kuwa sheria ya kuruhusu uraia wa nchi mbili.
Sasa hivi watanzania wengi wanaoishi Uingereza na nchi nyinginezo za Magharibi wanaweza kupata misaada kadhaa ya kuwekeza nchini mwao lakini kwa vile wengi wameamua kuwa na uraia wa nchi mbili bila kuachia uraia wao wa TZ basi inakuwa hawawezi kuwekeza nyumbani na kama watawekeza wataweka katika mfumo usio rasmi kama vile kuwatumia ndugu na jamaa pesa ili waweze kuwekeza,matokeo yake ni kuwa kwa vile ndugu hana uwezo wa biashara au kutokuwa muaminifu inakuwa ndio hivyo tena hela zinakwenda na hakuna linalofanyika,hii ina athari zaidi kwani mtu huyu hutotegemea akamhimiza mwenzie wa tanzania kuwa kawekeze nyumbani.
Naam mniwie radhi wanajukwaa nadhani ngwe yangu hapa mtandaoni italelemea zaidi katika kuwawezesha na kuwajali raia wote wa tanzania na kwa vile tuna asilimia 3% ya hawa wapo nje basi nao inabidi waainishe hoja zao ikiwemo na matatizo wayapatao,mwishowe waweze kuwa nao ni washiriki wazuri wa shughuli za kiuchumi Tanzania.
Mfano wa China ututoshe:
Kuna wachina 48 milioni nje ya nchi yao.Kuna wizara ya kushughulikia wachina waliopo nje ambayo inakuwa ni kama kiambatanishi cha wizara ya mambo ya nje ambapo wana jukumu la kuhakikisha kila mchina mwenye uwezo wa kutoa mchango kwao anawezeshwa bila vikwazo na pia wachina waliopo nje waweze kuwa wanapata habari na taarifa sahihi kuhusu hali ya uchumi,siasa,jamii nk wakati wote.
Angalia kwetu:
Balozi zetu zipo mbali na watanzania au tusema baadhi zimejitenga sana,ni kwa sababu kuwa karibu au mbali kunategemea na hulka ya balozi husika,kama ni mtu wa watu basi watu 'watajichanganya' kama sivyo basi watu hola! Nukta ni nini hapa? ni kuwa inabidi kuwe na ainisho maalum kwenye kazi za balozi katika kuwashughulikia watanzania.
Inatokea Rais anakuja kwenye nchi husika balozi anamkimbiza asionane na watanzania!
Natumai Ari mpya haitokuwa hivi na mabalozi nao watawajali watanzania hawa. Maoni yanakaribishwa, ''i stand to be corrected''
----------------------------------------------------
----------------------------------------------------
Waziri Member juu ya Uraia wa Nchi mbili
----------------------------------------------------
--------------------------------------------------------
Serikali yashauriwa kuwa makini juu ya Uraia wa nchi mbili
---------------------------------------------------------

Waraka wa uraia wa nchi mbili wakamilika
Na Boniface Meena
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Joseph Mungai amesema waraka wa mapendekezo ya mwananchi kuwa na uraia wa nchi mbili umekamilika na kufikishwa kwenye Baraka Baraza la Mawaziri.
Hata hivyo, waraka huo utapelekwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ili kupata muafaka wa pande zote mbili za Muungano.
Mugai alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya wizara hiyo na vitengo vyake kwa miaka miwili ya serikali ya awamu ya nne.
"Suala la uraia wa nchi mbili mchakato wake unaendelea na suala la vitambulisho vya uraia pia mchakato wake unaendelea na kwamba mchakato huo utagharimu kiasi cha dola Marekani milioni 152 (karibu 15.2 bilioni )," alisema Mungai.
Akizungumzia suala la wakimbizi, Mungai alisema idadi ya wakimbizi nchini imepungua kutoka 615,000 mwaka 2005 hadi wakimbizi 432,583 mwezi Novemba, mwaka huu baada ya zoezi la kuwarejesha makwao wakimbizi kuendelea vizuri.
Hata hivyo, alisema utafiti uliofanyika kuangalia ni asilimia ngapi ya wakimbizi hao wangependa kurudi nchini mwao hasa wale wa Burundi, imeonekana kuwa asilimia 21ya wakimbizi wa Burundi wangependa kurudi kwao na asilimia 79 wangependa kubaki nchini na hatimaye kuomba uraia.
Kwa upande wa magereza, alisema uwezo wa kisheria wa kutunza wafungwa umeongezeka kutoka wafungwa 22,6699 hadi 27,653 pia wafungwa na mahabusu wamepungua kutoka 46,416 hadi 43,262, lakini hata hivyo bado kuna tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu gerezani.
Alisema sababu za msongamano katika magereza ni ongezeko la uhalifu nchini ambalo husababisha ongezeko la idadi ya wafungwa lisilowiana na ongezeko la nafasi za kuwahifadhi pamoja kesi zao kuchelewa kusikilizwa mahakamani.
Kuhusu zimamoto Mungai alisema wizara inajitahidi kuboresha miundombinu ya kikosi hicho ili kiweze kukabilia na na majanga ya moto na mengine.
Chanzo: Mwananchi
----------------------------------------------------
Waziri Member juu ya Uraia wa Nchi mbili
----------------------------------------------------
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa KimataifaWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, amesema serikali itahakikisha sheria ya uraia wa nchi mbili inapitishwa kwa manufaa ya Watanzania na taifa na si vinginevyo.
Mh. Bernard Membe
Akizungumza na baadhi ya Watanzania waliokutana naye mjini New York wiki iliyopita katika hoteli ya Grand Hyatt, Waziri Membe alisema lengo la serikali ni kuwasaidia Watanzania na si kugawa uraia wa Tanzania kwa wageni wenye uraia wa nchi zao.
Alisema haingii akilini ni kwa nini Mtanzania wa kuzaliwa anyang'anywe uraia wa Tanzania kwa kuwa amechukua uraia wa nchi nyingine kutafuta faida za kielimu, ajira au hata matibabu.
"Ni kwa nini tumuadhibu huyu Mtanzania wa kuzaliwa kwa kuwa tu amechukua uraia wa nchi nyingine ili apate elimu ama ajira na kusaidia ndugu zake waliobaki Tanzania?" alihoji Waziri Membe.
Waziri alisisitiza kuwa sheria hiyo itakapopitishwa haitatoa mwanya kwa kila mtu kuuvamia uraia wa Tanzania bali itawalinda Watanzania wanaotaka kuchukua uraia wa nchi za nje kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.
Akitoa mfano mmojawapo bila kutaja majina ya wahusika, Waziri Membe alisema anaifahamu familia moja ya Watanzania ambayo ililazimika kuchukua uraia wa Kanada kwa sababu za matibabu, na kwamba kuwanyang'anya uraia watu hawa ni kuwaadhibu bila kujali uhai wao.
Alieleza kuwa familia hiyo ina watoto wawili ambao matibabu yao hugharimu dola 2,000 kwa kila mmoja kwa mwezi, na kwamba kwa kuchukua uraia wa Kanada, matibabu hayo yanakuwa bure. Alihoji je, ni haki kuwanyang'anya uraia wao wa Tanzania?
Akitoa mfano wa manufaa yanayopatikana Ghana, Waziri Membe aliwaambia Watanzania hao kwamba ni muhimu kwa Tanzania kutumia raia wake walioko nje kwa manufaa ya taifa na siyo kuwabagua.
"Mwaka jana pekee wananchi wa Ghana walioko nje waliingiza dola bilioni 2.5 kwa njia mbalimbali halali," na akaongeza: "Taifa dogo kama Komoro, mwaka jana lilipata dola milioni 89 kutoka kwa wananchi wake walioko Ufaransa pekee.
Akifafanua zaidi, Waziri Membe alisema wakati akiwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kipindi kisichofikia miaka miwili, Tanzania ilitoa uraia kwa wageni 101 na kushangaa ni kwa nini Watanzania wa kuzaliwa wapoteze uraia wao.
Waziri Membe aliwataka Watanzania kujenga umoja thabiti na kuwahakikishia kwamba serikali itakuwa pamoja nao ili kuleta maendeleo kwa taifa, na kwamba mawazo kuwa usalama wa taifa utakuwa hatarini si la jambo kuhofia iwapo sheria itatungwa vizuri.
Tanzania ina raia wake waliosambaa nchi mbalimbali duniani huku idadi kubwa ikiwa katika nchi za Kiarabu za Ghuba ambako wakati serikali ikiongeza ofisi moja ya Ubalozi nchini Oman miaka michache iliyopita ilikadiria kuwa kuna Watanzania laki tano.
Nchi nyingine ambazo Watanzania wanakadiriwa kuwa wengi ni za Marekani Kaskazini na Ulaya Magharibi ambako wako kwa maelfu, ambao wengi wao hukabiliwa pia na utata wa uraia wa watoto wao wanaozaliwa ugenini.
Mjadala wa suala la uraia wa nchi mbili umekuwa ukiendelea nchini katika siku za karibuni ambako kumeibuka kambi za wanaopinga kwa madai ya kulinda maslahi ya nchi na wanaounga mkono kwa madai hayo hayo ya kulinda maslahi ya nchi.
Serikali yashauriwa kuwa makini juu ya Uraia wa nchi mbili
---------------------------------------------------------
Tread carefully on dual citizenship, govt urged
By The Citizen Reporter
Jan 21, 2010
The government should be extremely careful when drafting a bill on dual citizenship to avoid abuse if it is enacted.
Though allowing dual citizenship will be such a relief for people who do not want to forsake patriotism at the expense of their survival abroad, some might use it for wrong purposes, observed Mr Freddy Macha, a Tanzanian living in Britain.
"Dual nationality is best for law-abiding citizens, for people wanting to bridge gaps between countries, for those working towards a better understanding of societies," he told The Citizen yesterday.
Mr M. M. Mwanakijiji, a Tanzanian living in Detroit, US, is against such as, saying reasons given to have it are weak.
He said arguing that the law would enable Tanzanians living abroad to invest back home did not hold water as citizenship was not among conditions to invest in the country.
"Many investors in Tanzania are foreigners and not indigenous Tanzanians. This shows that things might be easier for someone living abroad to invest in Tanzania as a foreigner," he said.
He also said it was disturbing that when discussing dual citizenship, many people had been countries such as the US, Canada and the UK in mind and seldom talked about Kenya, Uganda, Rwanda, Malawi and other countries.
"How will a person holding dual citizenship of Tanzania and Somalia help Tanzania?" he said.
He also warned against possible economic crimes and espionage especially if the citizenship involves economic giants. He gave an example of Chinese nationals holding American citizenship who sold some US secrets to China.
Mr Mobhare Matinyi, a Tanzanian consultant based in Washington DC, US, said dual citizenship had disadvantages and advantages "depending on how we enact the law and formulate our policy."
"The problem is that our country has serious weaknesses in safeguarding its interests as it happened in the Mining Act, Bank of Tanzania operations, government houses and other things," he said.
However, he said it was embarrassing for a child born of bona fide Tanzanian to be required to renounce one citizenship by the time he/she reaches 18.
The Tanzania Professionals Network (TPN) recently observed that lack of a law allowing dual citizenship was a stumbling block to Tanzanians in the Diaspora.
TPN president Sanctus Mtsimbe told The Citizen yesterday in Dar es Salaam that the network was campaigning for the enactment of the law on dual citizenship.
"We observed, for instance, that there are no good strategies and policies for facilitating easy investment by those who have decided to return back home. Such policies would encourage Tanzanians living abroad to return home and invest," he said.
On Tuesday, Foreign Affairs and International Cooperation minister Bernard Membe announced that the government would enact the dual citizenship law before the end of this year.
Law on dual citizenship coming
2008-07-15 10:16:03
By Bilal Abdul-Aziz, Dodoma
The government yesterday said it was in the process of drafting a new law that would allow Tanzanians to have dual citizenship.
Home Affairs deputy minister Khamis Kagasheki told the House that the Union and Zanzibar governments were jointly looking into the matter.
The deputy minister was responding to a question posed by Mwadini Jecha (Wete, CUF) who had wanted to know when the government would table a bill proposing the enacting of a new law on the matter.
``The Union government and that of Zanzibar are carefully looking into the matter. When the process has been completed, my ministry will bring the bill in the House for approval,`` said Kagasheki.
Earlier on, the deputy minister told Parliament that under the Union constitution, dual citizenship was illegal.
He said the law denied the people of Tanzania a chance to possess dual citizenship, and their Tanzanian citizenship ceased once they opted for other citizenship.
Kagasheki said the current laws particularly affected Tanzanian children born outside the country, who on reaching 18 years, were required to denounce the citizenship of one of their parents if they wanted to keep the Tanzanian citizenship.
``The system is not much known by our people. For that reason, at times, children encounter problems when they apply for passports or seek sponsorship for higher education,`` he said.
SOURCE: Guardian