Uraia pacha si wa kuchagua, ni wa kupewa na nchi ya pili kwa masharti yao

LGF

JF-Expert Member
Dec 6, 2020
1,389
781
URAIA PACHA SI WA KUCHAGUA, NI WA KUPEWA NA NCHI YA PILI KWA MASHARTI YAO. MARA NYINGI MASHARTI HAYO YANAKUTAKA UIKANE NCHI YAKO YA KUZALIWA, MATHAKANI UUKANE UTANZANIA WAKO.

Kabla hujapewa uraia wa USA, ni lazima ule kiapo kifuatacho, hadharani:

Full Oath of Allegiance to the United States

“I hereby declare, on oath, that I absolutely and entirely renounce and abjure all allegiance and fidelity to any foreign prince, potentate, state, or sovereignty, of whom or which I have heretofore been a subject or citizen; that I will support and defend the Constitution and laws of the United States of America against all enemies, foreign and domestic; that I will bear true faith and allegiance to the same; that I will bear arms on behalf of the United States when required by the law; that I will perform noncombatant service in the Armed Forces of the United States when required by the law; that I will perform work of national importance under civilian direction when required by the law; and that I take this obligation freely, without any mental reservation or purpose of evasion; so help me God.”

TUWAOMBE DIASPORA WETU WAWE WAZALENDO, WASITUTUPE. NENDA UBELGIJI, NENDA CANADA, NENDA USA, SOMA, CHAPAKAZI, TAJIRIKA, TUSAIDIE NDUGUZO TULIO HAPA, NA MJOMBA NA SHANGAZI, TUTUMIE HELA KADIRI UKIWEZA. HALAFU RUDI NYUMBANI. UKIONA HAPAKUFAI, BASI KAA HUKOHUKO LAKINI USITUSALITI NDUGUZO BADO TUPO HUKU.
 
Hiki hapa:

I hereby declare, on oath, that I ABSOLUTELY and ENTIRELY renounce and abjure all allegiance and fidelity to any FOREIGN prince, potentate, STATE, or SOVEREIGNTY, of whom or which I have HERETOFORE BEEN A SUBJECT OR CITIZEN.....

Imagine ulizaliwa Mnyiramba halafu useme hivi.
 
Ccm inaogopa vitu viwili katiba mpya na uraia pacha.Haya ni adui Mkubwa sana wa maagano na mazindiko ya kuzaliwa kwa ccm.Ccm na umasikini ni pacha sawa na masharti ya mganga.

Katiba mpya na uraia pacha uondoa umasikini, umasikini ukitoweka CCM lazima itakufa. Case study check ngome za CCM ni maeneo gani.
Na Ili uwe masikini ni lazima upitie hatua ya ujinga.Ujinga na umasikini ni kulwa na doto.

Huwezi kuwa masikini kama sio mjinga.
 
Uraia pacha na kuukana uraia ni vitu viwili tofauti.
Uraia pacha mtu mmoja kuwa na uraia nchi zaidi ya moja.Na kuuna uraia ni kitendo cha kuukana kuukataa utaifa ulionao.
 
Wawatumie hela ili muone maisha rahisi, muendelee kushabikia matapeli ya CCM sio?
 
Nchi nyingi za ulaya kama uingereza unaulizwa kama unataka kubaki na uraia wako au unataka uukane,na hap ijulikane kuwa kuukana uraia ni process nyingine.Kuchukua uraia HAKUENDANI na kuukana uraiawatu wengi wenye uraia ulaya bado kwa walipo(ulaya) wanatambulika kuwa na uraia miwili.
Ivyo uliyoandika si kweli,umeandika bila ufahamu wa kutosha.
 
Hiyo sawa kuwa wa-ulaya wanawatambua kuwa ni raia wa nchi mbili! je hizo nchi zao nazo zinatambua hivyo? kama ndivyo hili timbwili latoka wapi? mie nadhani nchi zao (Tanzania) haina kitu hicho, nipo tayari kupokea mawazo mbadala
 
URAIA PACHA SI WA KUCHAGUA, NI WA KUPEWA NA NCHI YA PILI KWA MASHARTI YAO. MARA NYINGI MASHARTI HAYO YANAKUTAKA UIKANE NCHI YAKO YA KUZALIWA, MATHAKANI UUKANE UTANZANIA WAKO.
Hii topic ya uraia pacha kila Tom and Jerry anaandika kwa kujifanya anaielewa, na hata Wabunge wengi wanaongea pumba kwa kujifanya wanailewa, kumbe hawana kitu.

Ngoja na wewe nikuonyeshe usivyoelewa mambo unayadandia kama lolri la mkaa. Unasema kwamba,

"URAIA PACHA.....MASHARTI HAYO YANAKUTAKA UIKANE NCHI YAKO YA KUZALIWA, MATHAKANI UUKANE UTANZANIA WAKO"

Sasa kama kama nchi ya uraia wa pili inakupa masharti ya kuukana uraia wako, unakuwaje tena uraia pacha?

Kama mimi Mtanzania, naomba uraia wa pili USA, na USA wanasema niukane uraia wa Tanzania nikakubali, nitakuwaje raia pacha wakati nimebaki na uraia mmoja wa USA?

Unajiona ulivyo kihiyo wa hii topic?
 
Uraia pacha na kuukana uraia ni vitu viwili tofauti.
Uraia pacha mtu mmoja kuwa na uraia nchi zaidi ya moja.Na kuuna uraia ni kitendo cha kuukana kuukataa utaifa ulionao.

Hiko Kiapo ni Cha wale walioomba Uraia wa Marekani.

Siyo Uraia Pacha.

Mulamula Akapekue vizuri aje tena
 
Hiyo sawa kuwa wa-ulaya wanawatambua kuwa ni raia wa nchi mbili! je hizo nchi zao nazo zinatambua hivyo? kama ndivyo hili timbwili latoka wapi? mie nadhani nchi zao (Tanzania) haina kitu hicho, nipo tayari kupokea mawazo mbadala
Unavyosema ni kweli Tanzania tunajua haikubali uraia pacha,lakini comment yangu ilikuwa na nia ya kumkosoa alioandika uzi huu kwani alisema kuwa masharti ya kupewa uraia mwengine ni lazima uukane uraia wako wa nchi ulikozaliwa,hii si kweli.
 
Back
Top Bottom