TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Habari za Uchunguzi wa mambo ya siasa zinasema kuwa ukaribu wa Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe na aliyewahi kuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antipas Lissu umezua hofu ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA. Taarifa hizo zinasema kuna uwezekano mkubwa wa Tundu Lissu kuhamia ACT-Wazalendo na kutengeneza Muunganiko imara wa kukabiliana Chanma tawala CCM katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwaka 2020. Sababu hasa za LIssu kufikia uamuzi wa kukitosa Chama chake bado hazijafahamika ingawaje ukaribu wa Zitto Kabwe kwa Lissu kuliko mtu yeyote hasa katika kipindi hiki ambacho Lissu amekuwa kwenye matatizo makubwa ya kiafya inatajwa kuwa moja ya sababu. Lissu anaamua kuuenzi msemo usemao "Äkufaaye wakati wa dhiki ndiye rafiki wa kweli".
Hali hiyo imepelekea Viongozi wa Chadema kuchukua hatua kadhaa ili kujaribu kunusuru Lissu kuhamia ACT-wazalendo.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe amelazimika kusafiri kwenda Ubelgiji anakotibiwa Mhe. Lissu kwa kile kinachodaiwa ni kwenda kuuzima moto aliouwasha Zitto wa kumshawishi Lissu ahamie kwenye chama chake. Inasemekana Zitto amekuwa na safari za mara kwa mara Ubelgiji ambapo baadhi ya safari hizo zimekuwa ni siri na hazikuripotiwa na vyombo vya habari.
Mwanachama kindakindaki kijana Yeriko Nyerere kupitia akaunti yake ya Twitter , ameponda kile kinachoitwa ni Muungano Mkubwa 2020 (GrandCoalition2020) unaoenenzwa na Zitto. Yeriko amemshutumu Zitto kuacha kushughulikia kesi iliyopekeka Diwani wake wa Kata Mwanga Kaskazini Manispaa ya Kigoma Ujiji Clayton Chipanda maarufu kama Baba Levo kushindwa rufaa iliyokuwa ikipinga kufungwa jela miezi mitano na kuongezewa muda wa kifungo hadi mwaka mmoja. Duru za kisiasa zinasema Yeriko na Kundi la vijana wenzake ambao ni wakongwe ndani ya Chadema wanaona kumruhusu Zitto ajihusishe na Chadema ni kusaliti Vijana wenzao waliokuwa wapambanaji wa kweli ambao leo hii hawaonekani akiwemo Ben Saanane.
ba