Urafiki wa Members Jf umekaa KIUNAFIKI zaidi, kuliko uhalisia.

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Wana wa Bodi, awali ya yote niseme poleni na mishemishe za kutwa ya leo.

Nikiwa nasoma shule ya wavulana miaka ile, nilikua na rafiki yangu tuliekua twasoma shule moja. Mara kadhaa wakati wa kurejea hom tulikua tukifatana nae, kwetu mimi palikua karibu na shule, na mwenzangu kwao palikua mbali , (kwa mujibu wa maelezo yake.)
Hivyo mara nyingi ilikua tukitoka skuli tunafika nae kwetu kama kuna karizki tunafinya nae, siku nyingine anapitiliza n.k. Ikatokea wakati rafiki yangu akawa mgonjwa na hakuweza kufika shule. Na hadi kufikia kuumwa mi sikua nikipajua kwao.

Siku moja Mama yangu akaniuliza "Mbona yule mwenzio kitambo haonekani ?"
nikamjibu kua anaumwa.
Mama akaniuliza "Umeshawahi kwenda kumjua hali ?"
nikamjibu mama kua kwao sipajui.
Maa akaniambia "Basi huo urafiki wenu ni wa kinafiki"
nikamuuliza maa kwa vipi ?
Akanijibu "Kawaida urafiki wa kuishia barabarani, si urafiki wa ukweli, je? Ukisikia amekufa ndiyo ukapatafute kwao siku ya msiba?"
Sikua na majibu ya kumpa maa.

Hapa Jf members wengi ni marafiki, bt majority wao ni urafiki unaoishia majukwaani.
Hivi mimi Judgement leo nimekufa hapa mtajuaje? Hata zile R.I.P zenu nitazipataje ?
Mf. mdogo hapa kuna members kitambo hawaonekani kama,

> Nitonye
>Maprsoo
> Figaniga
> F. Foxy
> AshaDii - afadhali kidogo Ashadii twaweza pata habari zake kwa Bro. Kaizer je? Hao wengine ? Nani ana data zao?

Aidha hao Members niliowatanya hapo ni baadhi tu, bt wako kibao. Mimi sipendezwi sana na urafiki wa kihivi. Napenda nikisikia member flani anaumwa nikamuone, ana shida nimsaidie, nami nna tatizo tunasaidiana hata kwa mawazo. Basi si mbaya mkaacha kujuana Members mnaoishi mikoa mbalimbali. Lakini unakuta mko mkoa mmoja hamjuani. Member anakufa si ajabu pengine mnaishi jirani , lakini hutomzika coz hamjuani, lakini Jf mlikua marafiki mnachart mnafurahi n.k Hii inaskitisha sana.

Naomba kutoa hoja.

Judgement.
 
Urafiki wa humu si wa kinafiki kabisa.......... huu ndio urafiki halisi, mambo ya kutembeleana na kununuliana soda nani atayaweza....... marafiki zangu wakae huko huko, siwahitaji mie......................LOL
 
bsi weka picha yako halisi,
weka number yako ya sim
na weka address yao signature
 
Urafiki wa humu si wa kinafiki kabisa.......... huu ndio urafiki halisi, mambo ya kutembeleana na kununuliana soda nani atayaweza....... marafiki zangu wakae huko huko, siwahitaji mie......................LOL

Nipe picha member unaechart nae kafa, mko mji mmoja, fare ya kufika msibani haizidi mia 5 tu, na usifike mazishini kwake , sababu humjui !
Hiyo pia poa tu?
 
umeongea point. wenye akili tumekuelewa na tutaifanyia kazi.
 
mi natamani nikutane na Kabakabana but alinitolea nje. naomba mnisaidie kunikutanisha. mwingine Kipipi.
 
Last edited by a moderator:
Na huo ndo utamu wa jamvi! Kama unataka pata mtu wa kula naye mtori na makange wapo wengi pale fesibuku. Lakin hakuna aliyekatazwa kuweka taarifa zake hapa
 
Judgement uko sahihi kabisa.
Ila tatizo linakuja je,mkishafahamiana...!!! Maana yatazuka ya kuzuka.
Kuna mmoja alipendekeza member wajitaje kwa majina yao halisi lakini alipingwa mbaya.
Je,tutafika?
Ok me naanza.
ME NIKO DSM,KINONDONI, wewe Judgement,Mamndenyi,Bishanga MKO WAPI?
 
mi natamani nikutane na Kabakabana but alinitolea nje. naomba mnisaidie kunikutanisha. mwingine Kipipi.

Mhe, Dubu nimekusoma!
Hao unaotaka kukutana nao naimani watapita hapa, wataona na nawashauri mjuane if posible! Ispokuwa mimi binafsi yangu sihitaji kujuana na wake za watu.
 
Last edited by a moderator:
Mhe, Dubu nimekusoma!
Hao unaotaka kukutana nao naimani watapita hapa, wataona na nawashauri mjuane if posible! Ispokuwa mimi binafsi yangu sihitaji kujuana na wake za watu.

Nhhe!
Makubwa haya.
Judgement mbona unawatisha watu?
Ila utamjuaje kama flani Ni Mke wa Mtu nawe unachat through Com & Phne?
 
Judgement uko sahihi kabisa.
Ila tatizo linakuja je,mkishafahamiana...!!! Maana yatazuka ya kuzuka.
Kuna mmoja alipendekeza member wajitaje kwa majina yao halisi lakini alipingwa mbaya.
Je,tutafika?
Ok me naanza.
ME NIKO DSM,KINONDONI, wewe Judgement,Mamndenyi,Bishanga MKO WAPI?

Bi Harusi mtarajiwa, kifupi mimi mikoa mi3 inanihusu sana, Dar
Dom
Mwz
but kwa sasa nimekita Mwz zaidi, shughuli zangu sekta binafsi , sijaajiriwa.
 
Bi Harusi mtarajiwa, kifupi mimi mikoa mi3 inanihusu sana, Dar
Dom
Mwz
but kwa sasa nimekita Mwz zaidi, shughuli zangu sekta binafsi , sijaajiriwa.

Abee..!!
Ila hujamaliza utambulisho wako.
Rejea Mwali alivyosema hapo juu.
Jimwage.
 
Nhhe!
Makubwa haya.
Judgement mbona unawatisha watu?
Ila utamjuaje kama flani Ni Mke wa Mtu nawe unachat through Com & Phne?

Walaa Bibie hamna tisho hapo!
Ni kweli huwezimjua huyu ni mke wa mtu au vipi, ndiyo maana nikaanika hadhara kweupee!
Ili atakaejijua ni mke wa mwenyewe tusizoeane kupitiliza na Pm na nini, sitaki.
Kama kuchart na mke wa mtu iwe public not privacy, Note : nikisema mke wa mtu nna maana real wife, not wife on line.
 
Hiyo itafata soon! Mbona bariida tu.

Eti ee!
We umesema hutaki Pm na wake za watu.
Na hao wakisema hawataki Pm na waume za watu,
atabaki nani jamvini?
Maana naona idadi kubwa ya member ka wapo ktk ndoa hv,
japo cna uhakika.
 
Back
Top Bottom