Urafiki wa Lowassa, JK usiingilie urais-Wabunge

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,009
*Selelii, Kimaro wataka afikishwe kortini
*Walaumu serikali kwa kutoa majibu ya ovyo
*Lowassa: Sizungumzi na vyombo vya habari

Waandishi Wetu, Dar, Dodoma
Majira
26 October 2009

WAKATI mkutano wa bunge unaanza leo, mzimu wa mkataba tata wa Richmond umeendelea kumwandama aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa baada ya baadhi ya wabunge kudai kuwa anastahili kuchukuliwa hatua zaidi ya ile ya kujiuzulu kutokana na kutajwa kwake katika kashfa hiyo.

Wabunge hao kwa nyakati tofauti wamesema kuwa urafiki ambao Bw. Lowassa alisema upo baina yake na Rais Jakaya Kikiwete usiingilie urais, serikali na uiachwe ifanye kazi yake kwa kumchukulia hatua kutokana na kuliingizia taifa hasara.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana, Mbunge wa Nzega, Bw. Lucas Seleli Bw. Selelii alisema kutochukuliwa hatua za kisheria kwa Bw. Lowassa kunatokana na urafiki uliopo kati rais Kikwete na mbunge huyo wa Monduli.

Alisema Rais Kikwete anapaswa kuamua kusuka au kunyoa kwa kuacha urafiki na kufuata sheria za nchi kwa kumfikisha Bw. Lowassa katika vyombo vya sheria, kwani alionekana wazi kushiriki kupitisha mkataba huo tata.

"Tulipokuwa tikijadili taarifa ya Kamati Teule ya Bunge tulibaini kuwa bila shaka alishiriki katika uamuzi huo, hivyo tulimwambia apime akapima, akaamua kujiuzulu. Huu ulikuwa ni uamuzi wake binafsi lakini sisi hatukuishia hapo.

"Tuliacha na serikali nayo iamue nini cha kufanya lakini hadi sasa imekuwa ikitupatia majibu ya ovyo ovyo tu, tunajua hawa watu ni marafiki tangu muda mrefu lakini urafiki na urais ni kitu tofauti. Hapa ni kazi wanatakiwa kuweka urafiki pembeni na kuwatumikia wananchi," alisema Bw. Selelii.

Alisema kama kweli nchi inafuata sheria na utawala bora, serikali inatakiwa kumshtaki Bw. Lowassa kutokana na kosa alilofanya kwani limekuwa likiipotezea nchi pato kubwa hadi sasa.

Alisema kuwa sheria ni sawa na moto, kwa kuwa moto unaweza kuundaa mwenywe lakini ukakuunguza.

Alisema katika mkutano wa 17 unaoanza leo mjini Dodoma wamekamia kumaliza suala hilo na kuhakikisha kuwa sheria inachukuwa mkondo wake kwa kuwachukiliwa hatua watu wote walihusika katika mkataba huo tata.

Kauli ya Selilii imekuja siku moja baada ya gazeti moja kutoa vielelezo vinavyoonesha jinsi Bw. Lowassa alivyohusika kushinikiza kusainiwa kwa Mkataba wa Richnond.

Lakini Bw. Lowassa alipoulizwa hakuwa tayari kuzungumza na gazeti hili. "Sikusikia vizuri swali lako kwa kuwa simu inakatakata, lakini siko tayari kuzungumza na vyombo vya habari kwa sasa hadi hapo nitakapopanga," alisema Bw. Lowassa na kukata simu.

Mapema, Mbunge wa Vunjo, Bw. Aloyce Kimaro naye aliungana na Bw. Selelii, akisema kuwa Rais Kikiwete anatakiwa kuuweka pembeni urafiki wao na kuchukua uamuzi utakaowafurahisha wananchi waliomweka madarakani.


Alisema Rais anatakiwa kukumbuka kuwa madaraka aliyonayo ni ya milele na yanagharimiwa na wananchi, hivyo hatakiwi kufanya machezo kwa kuchanganya urafiki na madaraka hayo, kwani kutomchukulia hatua Bw. Lowassa ni sawa na kuwadharau wananchi anaowangoza.

"Iwapo atachukua uamuzi mzito wa kumfikisha Bw. Lowassa katika vyombo vya sheria utakuwa si uamuzi wake bali ni wa wananchi kwa kuwa cheo hicho si mali ya Lowassa au ya Kikwete bali ni mali ya wananchi," alisema Bw. Kimaro.

Alisema hadi sasa hajui ni kwa nini rais anakuwa mzito katika kutoa maamuzi katika jambo hilo kwani mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge na maoni ya wabunge yako wazi.

Mwansheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Tindu Lisu, alihoji, "Lowassa mwenye alishasema kuwa urafiki wake na Rais Kikwete haukuanzia barabarani, sasa kwenye mazingira ya aina hiyo anaweza kumshitaki?

"Mtu wa kumshitaki mahakamani ni DPP (Mwendesha Mashitaka wa Serikali) ambaye anachaguliwa na Rais, na rais ni rafiki yake Bw. Lowassa, sasa hatawezaje kumshitaki katika mazingira hayo." alihoji Bw Lissu.

Alisisitiza kuwa Rais akitaka anaweza kumfikisha, Bw. Lowassa, katika vyombo vya sheria kujibu mashitaka ya kutumia vibaya ofisi yake.

"Kuna ushahidi mkubwa unaoonesha jinsi Bw. Lowassa alivyohusika, ukisoma ripoti yote ya Dkt. Mwakyembe (Harrison) utaona inavyoeleza wazi jinsi alivyohusika...barua zipo nyingi zinazothibitisha alivyoshiriki," alisema na kuongeza kuwa;

"Lowassa ni rafiki wa karibu wa Rais Kikwete, bado ana nguvu serikalini ndiyo maana haguswi."

Alisema hata makosa aliyofanya Bw. Lowassa yakifumbiwa macho lakini baadaye anaweza kushitakiwa. "Makosa yanayomkabili ni ya jinai ambayo hayafi hadi baada ya miaka 60," alisema na kufafanua kuwa hata serikali zijazo zinaweza kumfikisha mahakamani.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza kashfa ya Richmond, Dkt. Mwakyembe alisema yeye kama mwenyekiti hawezi kusema lolote kuhusu taarifa hiyo bali anasubiri kile kitakachowasilishwa na serikali.

“Unajua mimi nilikuwa mwenyekiti wa kamati sasa siwezi kusema lolote, waache Wabunge wengine waseme, mimi nikisema inaweza kutafsiriwa vibaya kwa kuwa nilikuwa mwenyekiti,” alisema Dkt. Mwakyembe.

Kauli hizo za wabunge zimekuja wakati serikali inatarajia kuwasilisha taarifa yake ya utekelezaji ya maazimio 23 ya Bunge kuhusu Richmond muda wowote kuanzia leo.
 
mhhhh.
yaani huku tunakoelekea....
sipati picha...

selelii ameanza kumtaja lowassa live...
tusubiri tuone ........
 
mhhhh.
yaani huku tunakoelekea....
sipati picha...

selelii ameanza kumtaja lowassa live...
tusubiri tuone ........

Mkuu watu wamechoka wanaona nchi inafilisiwa TANESCO watu wanafanya sehemu ya mradi wao. Fisadi Mkapa aliwaingiza wale Nethuru Group kwa mtutu wa bunduki ambao walikuwa hawajui chochote kuhusu umeme wakalipwa mabilioni ya shilingi lakini hawakufanya chochote kuboresha upatikanaji wa umeme nchini. Wakasaini mkataba na IPTL ambao ulikuwa ni WIZI MTUPU!

Pamoja na ushauri toka kwa wataalamu wa TANESCO kwamba Serikali isisaini nao mkataba lakini hawakusikia, hao IPTL wakalipwa mabilioni ya shilingi. Nchi ikaingia gizani 2006 wakasaini mkataba na kampuni ya papa fisadi RA na kulipwa $172 millioni na kushindwa kuzalisha hata tone moja la umeme. Wahusika wote bado wanapeta pamoja na kuwa TANESCO iko hoi bina taabani. Waache waseme mkuu liwalo na liwe hali hii haiwezi kuachiwa iendelee daima. Kikwete akulizwa atajibu, "Najivunia rekodi ya uongozi wangu na upatikanaji wa umeme nchini." Astaghafirullah!

...kweli ukistaajabu ya Mussa....halafu bila hata aibu anataka kugombea tena 2010 ili kulinda utamaduni wa chama chao! wa kukaa madarakani kwa awamu mbili, pamoja na kuvurunda kote huku! Ama kweli Tanzania ni kichwa cha Mwendawazimu.
 
pamoja na hayo..
nafikiri seleli kashaona
kampeni dhidi yake ya ubunge ..
na sasa kamua kumwaga mboga....
 
Kama umesahau kuwa mwakani ni uchaguzi wa Rais,Wabunge na madiwa unaweza ukafikiria kuwa hawa wabunge wanamapenzi mema na wananchi na kwa upande mwingine ukilikumbuka hilo utagundua kuwa kuna watu wanameanza kuzitafuta kura kupitia migongo ya wengine.Wabunge wengi wana zaidi ya miaka kumi bungeni na wengi walishiriki kwa namna moja au nyine ktk maamuzi ambayo kwa kiasi kikubwa yameligarimu taifu na hao hao leo wanakuja na kukemea vitu ambavyo vimefanyika na wao wakiwa wemeshiriki.
Am proud to be Tanzanian but not the way things are going on..let's talk and act!
 
Naona kambi ya JK inajibu mapigo ya kambi ya EL...Bottomline tunautaka ukweli,hopefully this time utawekwa wazi.
 
Naona kambi ya JK inajibu mapigo ya kambi ya EL...Bottomline tunautaka ukweli,hopefully this time utawekwa wazi.

Mkuu Jmushi1, mimi nadhani kama ukweli ukianikwa hadharani basi labda JK itabidi aachie ngazi. Nadhani unakumbuka Mwakyembe alidai kwamba kuna mengine ambayo hakuyaweka kweye ripoti yao ambayo yalikuwa ni mazito zaidi. Sasa kama yaliyoandikwa yaliweza kumuathiri Lowassa basi labda hayo mazito zaidi yangemgusa kwa karibu Kikwete na sia ajabu yanaweza kabisa kuanikwa hadharani kama sakata hili likipamba moto na kuwa patashika nguo kuchanika.
 
  • 'Majemedari' wake wajipanga
  • Kikwete huenda akahusishwa

Na Saed Kubenea
MwanaHALISI

EDWARD Lowassa, aliyekuwa waziri mkuu, anatarajiwa kuibukia katika mkutano ujao wa Bunge na kupasua kile kinachoitwa "ukweli kuhusu utata wa mkataba wa Richmond," imefahamika.

Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya kambi yake na katika serikali zinasema Lowassa amekuwa akishinikizwa na marafiki zake kuweka “mambo hadharani” kwa lengo la kujinasua kwenye kitanzi cha Richmond.

Mkutano huo wa Bunge la Muungano, unaoanza Jumanne ijayo mjini Dodoma, unakuwa muhimu kwa kuwa ndimo serikali iliahidi kuwasilisha ripoti ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond Development Company (LLC). Suala la Lowassa kupasua ukweli linakuja karibu mwezi tangu atamke kuwa yeye na Rais Jakaya Kikwete ni marafiki wa kweli, ambao hawakukutana njiani na kwamba hakuna wa kuwatenganisha.

Alisema yeye na Kikwete wametoka mbali na urafiki wao, “hauwezi kuvurugwa na kikundi kidogo cha watu.”

Hata hivyo, kauli ya Lowassa ilitolewa siku mbili tangu Rais Kikwete aseme, mapema mwezi uliopita, kwamba, “sina ndugu wala rafiki” katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi.

Rais alikuwa akijibu swali la mmoja wa wananchi, katika kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo kwenye televisheni, ambaye alimtuhumu kulinda marafiki zake wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Rais Kikwete alinukuliwa pia akisema serikali yake ina mpango wa kutafuta msaada wa kitaalamu kutoka vyombo vya kimataifa ili kujiridhisha kuhusu utata wa zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Richmond.

Kampuni ya Richmond ambayo ilipewa zabuni ya kuagiza mitambo ya kufua umeme wa dharura mwaka 2006, ndiyo chanzo cha kujiuzulu kwa Lowassa na mawaziri wengine wawili.

Mawaziri waliojiuzulu ni Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha kutokana na kuhusika kwao katika mchakato wa mkataba wa Richmond ambao Rais Kikwete amebainisha kuwa ulijaa uzembe na ubabaishaji.

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema kauli ya Lowassa ilikuwa “inatoa salamu” kwa Kikwete, kwamba siku atakayopata nafasi ya kuzungumza, hatakuwa na simile – ataanika kila kitu hadharani.

Haikufahamika iwapo “kuanika kila kitu” kunamaanisha kumhusisha Rais Kikwete katika kashfa ambayo tayari bunge limeitolea maamuzi.

MwanaHALISI linaweza kuthibitisha kwamba Lowassa na wapambe wake wako mbioni kukamilisha wanachoita, “mkakati wa kusafisha njia kuelekea kilele cha uongozi.”

Chanzo cha habari cha gazeti hili kimemnukuu mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba akisema, “Ni lazima Lowassa apasue jipu katika mkutano huu.”

Serukamba, mmoja wa wabunge wanaotajwa kuwa ni watetezi wakubwa wa Lowassa ndani na nje ya bunge, anasema katika mahojiano hayo, “Tunategemea hivyo na kila kitu kitakwenda kama tulivyopanga.”

Mbunge Serukamba alikuwa akijibu swali aliloulizwa juu ya hatua waliyofikia kuhusu mpango wa Lowassa kuzungumza “kutoboa kila kitu bungeni.”

Kambi ya Lowassa inasemekana kupata nguvu mpya baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumsulubu Spika wa Bunge la Jamhuri, Samwel Sitta kwa madai kuwa anasababisha “kuchafuka kwa hali ya hewa” bungeni na kudhoofisha serikali.

Uchunguzi wa awali wa mkataba wa Richmond ulibainisha kuwapo kwa uzembe, jambo ambalo lilibainishwa na Kamati Maalumu ya Bunge ya Nishati na Madini, iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe.

Wakati Lowassa akipanga kujisafisha, mmoja wa wajumbe wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba huo amesema wanasubiri kauli yake “kwa hamu kubwa.”

“Unasema amepanga kulipuka bungeni? Ha, ha! Tunamsubiri. Nakuhakikishia hapatatosha,” alisema akitoa kicheko chembamba.

Alisema, “Kwa kweli mdogo wangu, nakwambia ataumbuka; maana hata zile taarifa za ndani, ambazo hazikuwa zimepata mwanya wa kutoka, zitawekwa kwenye paa la nyumba.”

Sakata la Richmond linatarajiwa kuchukua sura mpya katika mkutano huu wa bunge iwapo serikali itatoa taarifa ya utekelezaji, kama ilivyoahidi na baadaye kujadiliwa na wabunge.

Ni katika hatua hiyo, taarifa zinaeleza, wapambe wa Lowassa wanataka kujipanga ili kushawishi wabunge kuwa kigogo huyo “hakuhusika” katika kashfa ya Richmond.

Mkataba wa Richmond ndio ulisukuma Lowassa nje ya uwaziri mkuu hapo Februari mwaka 2008. Tangu hapo, Lowassa na wapambe wake wamekuwa wakijitahidi bila mafanikio kutaka kurejesha hadhi hiyo ya kisiasa.

Taarifa zinasema tayari kuna mkakati wa kupanga “idadi nzuri” ya wabunge ili wakati Lowassa anazungumza, waweze kumshangilia kwa kupiga makofi ili kuzima nguvu ya “wapinzani wake.”

“Ndiyo, tumeshapata zaidi ya wabunge 100 wanaotuunga mkono. Tunataka pale Lowassa anapozungumza asitokee mtu wa kutujibu. Na kila anayetaka kujibu akutane na kishindo chetu,” mbunge mmoja alimueleza mtoa taarifa.

Kuna taarifa kuwa kundi la Lowassa limepanga kutumia mbinu iliyotumika katika NEC kuzima sauti na ushawishi wa wabunge wanaopinga mkataba huo wa Richmond.

Hata hivyo, mjumbe mmoja wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini aliliambia MwanaHALISI kwamba ni lazima Lowassa aje na utetezi wa nguvu, vinginevyo anaweza kujikuta anazama badala ya kuibuka.

Kamati Teule iliyochunguza Richmond, ilitoa mapendekezo 23, yakiwamo ya kuwachukulia hatua waliohusika kuibeba kampuni hiyo kinyume cha taratibu na hata sheria za nchini.

Iwapo Lowassa atapata fursa ya kutimiza azma yake, kuna uwezekano wa kuchafuka tena kwa hali ya hewa bungeni kutokana na kile ambacho baadhi ya wabunge wanadai “kutokubali kusafisha watuhumiwa.”

Kundi la Lowassa linataka kutumia kauli ya Rais Kikwete kwamba alizuia waziri wake mmoja kufanya malipo ya awali kwa Richmond akihofia “inaweza kuwa kampuni ya mfukoni.”

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, kauli hiyo ya rais inatafsiriwa kusema kuwa Lowassa alishirikisha kiongozi huyo wa nchi katika “hatua zote za kufikia mkataba” ambao ulikuja kufahamika kuwa wa upendeleo na unaovunja kanuni na sheria.

“Sisi hatujali nani anaumia na nani ananufaika. Tulichopanga ni kupasua jipu,” anasema mbunge huyo kutoka kambi ya Lowassa.
 
Safari hii tutasikia mengi na kila mtu anataka kulinda nafasi yake ya ubunge, kwa hiyo choko choko kama hizi tutazisikia sana na hapa ndio watu wanapojidai ni wazalendo wa kutaja kashfa za wengine
 
mimi naenda sumbawanga nikirudi lazima kieleweke tu.................sasa maana haki hitendeki kabisa.........kilichobaki ni kutana ROHO TU.Haiwezekani mafisadi wawe wanakula nchi kwa kiasi hicho
Naendaaaaaaaaaaa
 
Mwakyembe wakati fulani alinukuliwa akisema kwenye taarifa yao kuna mambo hawakuyasema. Hii ikampa ahueni sana EL. Sasa wanashinikiza suala hili liende mahakamani kisiasasiasa hivi. Hakuna watakachoambulia. EL alikuwa anaandika memo zake kijanja sana na kwa tahadhari kubwa. Ni FISADI mzoefu mno pengine kuliko Mtanzania ngozi nyeusi yeyote.
 
Ushauri wa bure kwa EL.

Usimhusihe JK katika suala la Richmond, it is bound to backfire with devastating effects. Kwamba JK ni rafiki yako haihalalishi makosa yaliyotendeka.

Waombe waTanzania radhi kwa makosa uliyoyafanya katika sakata lote la Richmond-this will defuse all hatred against you.

Lishukuru Bunge na wabunge kwa umakini,hawa ni wawakilishi wa wananchi, kwani ndio waliokufikisha hapo ulipo.You cant fight the mass and win, hata ukiwa na lundo la pesa.

Kama unaipenda Tanzania na ustawi wake, waTanzania watakuelewa ukifanya hayo na kufunika kombe.

Kwa sasa hivi kauli zako za urafiki wako na JK sana sana zimeamsha upya moto wa chuki dhidi ya ufisadi uliofanyika katika sakata la Richmond na kuamsha hisia kuwa pengine JK naye anahusika.
 
Leo naona kama siku ndefu sana....sanaa...nasubiri mno mapendekezo..ya serikali
 
Ni siasa tu, kama ni ile report ya Dr. mwakyembe, sioni watamshitaki Lowassa kwa kosa gani?

Watanzani tuwe waelevu wa sheria, vinginevyo ndio maana mafisadi wanatushinda kirahisi mahakamani.

Kama mtu anafikiri anaweza kumfikisha Lowassa mahakamani kwa makosa yaliyomo kwenye tume ya Mwakyembe, basi huyo mtu ni very naive na si ajabu hajui hata sheria.

Malipo ya Lowassa ni kisisa; tayari kalipa kisiasa kwa kupoteza kuwa waziri mkuu na pia anaweza kupoteza kuwa mbunge. Lakini kumwambia wanaweza kumpeka mahakamani ni fantassy at best.

Halafu hii ya wanasiasa kushinda magazetini kila siku inasikitisha sana. Kama wana ushahidi si wafanye kweli bungeni? Hizi kelele magazetini ni za watu waoga ambao majimbo yao yako hatarini na wanataka kura za huruma.

Ukiingiza chuki kwenye kutenda haki au kuamua sheria, utaishia kuchemsha mtu.
 
Back
Top Bottom