Urafiki wa Dam: Morani na Mdosi

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
2,000
Well, well,well sasa twaanza kuona ni jinsi gani misheni zilivyoanza andaliwa na hawa jamaa wawili.

NdiyoMorani kaachia ngazi, lakini hilo halitoshi kutamatisha uhujumu uliofanyika. Paper trail ifanyike ijulikane pesa zilikwenda kwa nani baada ya CRDB kuwalipa kina GIRE. Kwa kuwa hawajamaa walijidaieti wao ni Wamarekani, basi FBI na IRS ziombwe zisaidie kufanya uchunguzi na ile ofisi ya FINCEN, OFAC ambazo ziko chini ya Dept. Of Treasury ya Marekani zisaidie mpaka tuelewe hizi pesa ziko wapi!

Lakini turudi kwenye ndoa hii ambayo machoni petu ni haramu, when did Morani and Mdosi became BFF(Best friend for life)?

http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/2/8/makala2.php

Jambo la pili lililomtumbukiza Lowassa katika mwisho huu mbaya wa kutumikia kiti cha waziri mkuu, ni tabia ya kuamini marafiki na kushindwa kutenganisha nafasi yake kabla ya kuwa waziri mkuu na baada ya kushika wadhifa huo mkubwa nchini. Bado kuna hisia za kuamini marafiki kuliko mfumo wa kiutendaji ulioko kisheria na kikanuni.
Tathmini iliyofanywa na Kamati ya Dk. Mwakyembe imesema kwamba mradi wa Richmond ulikuwa ni wa Lowassa na rafiki yake, Mbunge wa Igunga, Rostam Azizi, kauli ambayo Waziri Mkuu huyo aliikanusha jana asubuhi.
Kwamba Lowassa na Rostam ni marafiki si kitu cha kuhoji. Watu hawa walipata kuishi nyumba moja wakiwa na nyadhifa kubwa tu za kisiasa. Rostam na Lowassa walikuwa wanaishi nyumba moja Dodoma. Haya ni mambo yaliyotokea wakati wa Bunge la 1995-2000.
Katika urafiki huu, Lowassa alijikuta akiishi kwa kuamini maneno ambayo alikuwa akipewa na marafiki zake (hususan Rostam) kwamba Richmond ni kampuni halali, yenye uwezo wa kutekeleza majukumu yake na kwa maana hiyo kupewa kazi ya kuzalisha umeme wa dharura isingekuwa jambo baya. Ikumbukwe kwamba wapo wafanyabiashara waliotoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya kusaidia CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, hawa wamekaa mkao wa kurejesha fedha zao.
Ni kutokana na mkao wa kusaka fedha, mikakati ya kutunisha mifuko, Richmond ilipewa kazi ya kufua umeme wa dharura kwa kutumia gesi. Richmond imethibitika kwamba ni kampuni ya kitapeli, kampuni ya kwenye mkoba, ambayo kwa hakika haina hata uwezo wa kufunga balbu kwenye nyumba, achilia mbali kufua umeme megawati 100. Lowassa ama kwa kutokutambua nia za marafiki zake aliowaamini, na ama akiwa amehakikishiwa kwamba Richmond ni kampuni nzuri au kwa sababu ya haraka zake za kutokutaka kujipa muda wa kutafakari na kudadisi mambo yaliyokuwa nyuma ya Richmond; yaani uwezo wake, historia yake, na hata walikokuwa wanaipigia upatu; amejikutaka akiachia ngazi mapema kuliko alivyowahi kuwaza moyoni mwake.

It all started after Lowassa was dumped in 1995!
 

Lione

Senior Member
Dec 1, 2007
113
0
Tatizo nikwamba kuna watu wanajua mengi humu ndani,lakini wavivu kumwaga radhi
 

Lione

Senior Member
Dec 1, 2007
113
0
ORDER PLSSSS
Kama kuna mtu mwenye taarifa muhimu,azimwage hapa,maana taifa liko icu,tumsaidie muungwana,kufanya maamuzi,maana inaelekea anafuatlia kwa klaribu sana jf,na nimemba pia,mnalijua hilooo?
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
2,000
" Kweli ni huzuni, kwa kuanguka kwake morani, kulipotokea pale bungeni, akasema moyoni, nafukuzwa kazi kwa uzushi, akalia kwa huzuni, hata mwisho akachoka, pale juu kizimbani akabwaga nyanga kwa huzuni"!
 

Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,397
1,250
" Kweli ni huzuni, kwa kuanguka kwake morani, kulipotokea pale bungeni, akasema moyoni, nafukuzwa kazi kwa uzushi, akalia kwa huzuni, hata mwisho akachoka, pale juu kizimbani akabwaga nyanga kwa huzuni"!

Rev naona umeamua kututolea "remix", lakini kumbuka sheria za hakimiliki!
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
2,000
Hawa wawili wameshaanza kutapatapa. MMoja kapokelewa na maandamano ya Hosana yuaja mtawala, mwingine anadai mimi siwajui hawa watu hata warithi wake pamoja na kuwa waminipa mlo wa ukandarasi!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom