Urafiki Tata: TZ, KE & nchi za Afrika Mashariki na sapoti ya Kuhama kwa Ubalozi wa Marekani Jerusalem

Kaka Pekee

JF-Expert Member
Apr 3, 2018
336
559
Kwa kuzingatia kuwa nchi yetu imeamua kuingia/ kuendeleza uhusiano na ISRAEL nimeshtuka kuona Muandishi huyu wa Daily Nation Kenya alichoandika Kenya: What Kenya's Show At U.S. Jerusalem Embassy Shift Means kifupi ni juu ya Kenya, na nchi nyingine za Africa kushiriki kikamilifu katika tukio la mualiko wa Kui sapoti Marekani kuhamisha ubalozi wake Jerusalem. Afrika tukiwa ndio tuliotuma uwakilishi mzito wa kutuma maafisa wake wa juu zaidi katika hafla hiyo.

TUKUMBUKE KUWA: The Arab League (Muungano wa nchi za Kiarabu)inayojumuisha majimbo wanachama 22 iliomba jumuiya za kimataifa zisiunge mkono suala hilo dhidi ya Marekani na Israel...Hawa jamaa pia wana pesa nyingi sana kuweza kufund au kufanya chochote chenye maslahi na wao bila tatizo.

na ilisemekana kuwa kuna hofu kubwa ya wanaharakati kuandaa Mashambulio yatakayo walenga raia wa marekani nchini israel endapo itahamisha ubalozi wake. kwa kutumia mbinu mbalimbali "Extremists may use the upcoming relocation of the US Embassy in Israel to target US citizens. Terrorists may employ a variety of tactics," it said.

Raia hao walionywa kuwa "Mashambulio hayo yanaweza kulenga Shule, hospitali, makanisa, vivutio vya watalii, usafiri, na sehemu za mkusanyiko wa watu mbalimbali, hivyo raia wa marekani wakae chonjo na kuripoti tukio lolote linaloashiria uhalifu."

MAJANGA YALIYOPITA:
Tanzania na Kenya ziliwahi kuwa ni nchi zilizokumbwa na Janga la Kulipuliwa kwa Balozi za Marekani mwaka 1998. Ninapata wasiwasi nikiona Tumejikuta tukihusika na matukio ya uhusiano tata kama huu na Israel ambao unapingwa na mataifa mengi hatari (Yenye Uhusiano na Mrengo/Msimamo Mkali)

NB:
Waziri wa mambo ya nje wa Israel aliiambia Al-Jazeera kuwa walialika nchi 86 ambazo wanafanya nazo shughuli za kidiplomasia lakini nchi 33 tu ndio zilithibitisha ushiriki wao zikiwemo nchi zetu.

Watu wetu wa Intelijensia wanapaswa kuwa makini sana na Maamuzi ya Nchi yetu katika Uhusiano na Mataifa yenye Migogoro kama Israel. Na Tuombe Mungu hawa Jamaa wasije kutushughulikia huku kwetu tena kama Mwaka 1998 kwa kuwa tumeungana na kuwasapoti mahasimu wao Marekani... ukizingatia kuwa Wanaharakati wenye msimamo mkali wa nchi hiyo ndio wanaongoza kwa kujitoa Mhanga.

** Israeli forces killed at least 58 Palestinians as they moved to quell the protests.

Stori kamili: Kenya: What Kenya's Show At U.S. Jerusalem Embassy Shift Means

1.PNG
 
Kipindi kile hatujaanzisha ubalozi na Israel tulipigwa kwa sababu zipi?
Kipindi kile kwa utafiti ilionekana tulishambuliwa sababu ya hali ya kiusalama ilivyokuwa nchini. Ilikuwa ni rahisi kwa mtu yeyote kuingia na kuishi Tanzania kama tu hatovunja sheria za nchi. (Hali ya Kiusalama ilikuwa Poor) hivyo ikawa rahisi kumfuata hasimu wao (Marekani) nchini na kumshambulia hapa na Kenya ndio maana baada ya tukio hilo ndio tulianza kuona Askari wakifanya Doria na Silaha Barabarani( Vuta kumbukumbu...Haikuwa hivyo kabla).

Kwa sasa tunapaswa kuwa na Umakini zaidi sababu tu, mgogoro wa nchi ya ISRAEL na washirika wake huko mashariki ya kati ni hatari zaidi sababu ya wingi wa watu wanaojitoa muhanga na jinsi walivyoendelea kiteknolojia. Kama hukubaliana na hili unadhani tuna teknolojia ya kushindana na hawa jamaa wakiamua kufanya yao kama tu wakiamua kutushambulia?.

Anyway Take hapa ni kuwa makini zaidi na kutojishughulisha na siasa za Hatari na Ushirikiano/uhusiano na Marafikiambao wanaweza kutuweka Matatani. Maswala mengine ni vyema tukajiweka pembeni tukiangalia. Saint Ivuga
 
Back
Top Bottom