Urafiki na Rwanda vs Urafiki na Kenya upi una Manufaa Kwa Tanzania?

Kansigo

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,670
2,156
Kumekuwa na maneno na hofu kutoka kwa baadhi ya Watanzania hasa baada ya Raisi Samia kufanya juhudi za kuurejesha tena uhusiano na Kenya ambao ulidhoofika sana awamu ya Tano.

Awamu ya Tano iliona Ni muhimu zaidi kuikumbatia Rwanda ya Kagame kuliko Kenya. Ikafikia wanyarwanda hadi wanakuwa sehemu ya mfumo wetu wa ulinzi kwa kiongozi wa juu.

Naomba tujadili ni upi uhusiano wenye Kati ya haya mataifa mawili una manufaa kwetu kama nchi.
 
Binafsi naona mataifa yote yana umuhimu kwetu, mfano Rwanda tunawategemea sana kwenye bandari yetu, na kuuza bidhaa zetu za viwanda. Kwa upande mwingine Kenya ni muhimu tena hasa tulio mpakani mwa Kenya maana jamii zetu zinaingiliana na mazao yetu tunauza Kenya.
Mataifa yote tunategemeana sana, huwezi kukimbia mwenzako kwa sababu zinazozuilika ama tatulika
 
Kenya ina afadhali, Rwanda ipo kojasusi na kipelelezi Kwetu. Kagame sijui anataka nini.

Rais Samia Suluhu unapotaka kuitembelea Rwanda Kuwa Makini na Rais Kagame. Kagame ni solid Dictator na mwona mbali mno kuliko kiongozi yeyote Africa hii. Ukiongeanaye na kukubaliananaye ukimpa kisogo anakumaliza.

Rwanda kwa mipango yake hiyo imechomeka majasusi nchi jirani zake mbalimbali. Yupo tayari kutumia majasusi wa kike Malaya kupeleleza au kuua viongozi wakuu wa nchi hizi na wapinzani wake waishio huko.

Kagame anapeleleza Sana mifumo ya ulinzi wa nchi jirani. Jirani akizubaa tu, huchomeka vijana wake ktk mafunzo ya kijeshi ya nchi husika na kijifanya raia wa nchi hiyo. Pia hutaka kutumia fursa za rasilimali za nchi jirani. Congo ni waathirika wakubwa Sana japo sisi pia hatupo salama kwani anatusaka kwa kutupeleleza usiku na mchana.
 
Kumekuwa na maneno na hofu kutoka kwa baadhi ya watanzania hasa baada ya Raisi Samia kufanya juhudi za kuurejesha tena uhusiano na Kenya ambao ulidhoofika sana awamu ya Tano. Awamu ya Tano iliona Ni muhimu zaidi kuikumbatia Rwanda ya Kagame kuliko Kenya.Ikafikia wanyarwanda hadi wanakuwa sehemu ya mfumo wetu wa ulinzi kwa kiongozi wa juu.
Naomba tujadili Ni upi uhusiano wenye Kati ya haya mataifa mawili una manufaa kwetu kama nchi
Naona mmeanza kujitaja vibaraka wa jiwe
 
Unailinganisha Rwanda na Kenya?
 
Unamaanisha urafiki na Rwanda au Kagame? Hivyo ni vitu viwili tofauti.
Lakini yote kwa yote, Rwanda ni nchi ndogo sana, yenye rasimali chache zenye ukomo, hatuwezi kusema tunaweza kuwategemea, ama kuwa na ushirika mkubwa wa kufanya sote tufaidike sawa sawa. Kieneo tu, Mkoa wa Morogoro huenda ni mkubwa mara tano ya nchi ya Rwanda.

Sasa tukirudi kwenye swali lako, Tanzania kujenga urafiki na Rwanda kwa gharama ya kuvunja urafiki na Kenya ni sawa kuiambia USA ivunje urafiki na Canada ili kujenga urafiki na Cuba.

Kenya na Tanzania ni zaidi ya marafiki, Kenya na Tanzania ni ndugu wa karibu sana wa siku zote. Ndugu huwezi kuwatenganisha. Kijamii na kiuchumi Kenya ni mshindani wetu na mshirika wetu mkuu. Ni nchi zinazotegemeana sana.
 
Hayo mambo ya undugu na urafiki ni lugha ya kidiplomasia huko duniani maana watu wanaitumia pale inapokuwa na maslahi kwao, Ila ni huku bongo tu ambapo bado tunayong'ang'ana nayo as if ni kitu halisia

Ongeleeni tu maslahi maana mambo ya undugu na Urafiki HAYAPO
 
Uyo kagame si alimtapeli mwendazake 5 trillion au hamjui
Au ndo maana Li Kagame halikuja Wala kutuma mwakilishi kwenye Msiba wa JPM, bora tubaki na Wakenya wetu ....Big up Mama kuyarudisha mahusiano
 
Kumekuwa na maneno na hofu kutoka kwa baadhi ya watanzania hasa baada ya Raisi Samia kufanya juhudi za kuurejesha tena uhusiano na Kenya ambao ulidhoofika sana awamu ya Tano. Awamu ya Tano iliona Ni muhimu zaidi kuikumbatia Rwanda ya Kagame kuliko Kenya.Ikafikia wanyarwanda hadi wanakuwa sehemu ya mfumo wetu wa ulinzi kwa kiongozi wa juu.
Naomba tujadili Ni upi uhusiano wenye Kati ya haya mataifa mawili una manufaa kwetu kama nchi
Kenya ni bora mara 100 zaidi kuliko Rwanda.

Tukifanya mahusiano mazuri na Kenya na Congo. Tumemaliza.

Rwanda ni kama Burundi tu. Tunawasaidia tu maisha
 
Mama anapaswa kukaa mbali kabisa na Kagame. Kama hamjui vizuri Kagame basi mama aende msoga akamuulize Kikwete amsimulie mambo ya Kagame.
 
Kenya ni sehemu sahihi kibiashara kwetu..wana eneo kubwa na population kubwa hapo tayari kuna soko la watu wengi...Kenya imeunganishwa na dunia miaka mingi aka mlango wa nchi nyingi za Ulaya na America kwa Africa....Stability ya Kenya na demokrasia yao inaleta confidence kwa watu wetu..
 
Rwanda ni nchi ndogo yenye watu wachache....soko lake ni dogo na kwa vyovyote vile automatically tukiwa stable tutawameza...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom