Urafiki na huyu mke wa mtu uko hatiani

Kuna dada mmoja nilisoma naye darasa moja miaka mingi iliyopita, tulikuwa hatuna mahusiano yoyote...zaidi ya hisia zake na zangu kuwa zinawasiliana tu. Wiki tatu hivi zilizopita, nilipokea simu kutoka kwake tukasalimiana na kujuliana hali, pamoja na kuniambia jitihada alizotumia kupata namba yangu. Yeye alishaolewa na anafamilia yake zaidi ya miaka 10. Ilitokea wamehama hama kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine kutokana na mazingira ya kazi. Ndani ya wiki tatu hizi tumewasiliana sana, naye anatumia nguvu nyingi sana kunipigia simu, kutuma sms n.k

Juzi, ndipo akaamua kuniambia changamoto alizonazo kwenye ndoa; mumewe amebadilika, akirudi nyumbani anamjibu kwa ukali, hakuna masikilizano, matumizi hatoi, mzee anawajali watoto tu, amekuwa hana thamani ndani ya nyumba zaidi ya kuonekana kama beki 3.

Nilijaribu kumpa ushauri wa hapa na pale, lakini naona uelekeo wake naye anatafuta pa kupunguzia msongo wa mawazo. Najaribu kufikiria huu ukaribu huu unaojisogeza, unaweza kusababisha kula tunda kimasihara, lakini hofu yangu nisije kuwa kikwazo kwenye familia yake au yangu. Na nikikata mawasiliano naye pale anaponipigia nahisi nitakuwa sijamtendea haki.

Wakuu mnanishauriji kwenye hili jambo?
Angalia hii isipelekee wewe Kuzini:

"Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake"

Mithali 6:32
 
NJE YA MADA.


Soulmate. Naamini watu wengi hatukutani na wenzi wa nafsini bali tunapata wa mwilini.

Mara nyingi wenzi wa mwilini hua tuna hisia nao za matamanio ya kimwili zaidi ya rohoni. Na hisia hizi hudumu 2-4 yrs baada ya hapo mambo hubadilika negatively.

Ndoa ili iwe nzuri yenye mgogoro wa kuzungumzika baina ya wawili hawa, basi ni wajibu watu hawa waendane na vitu hivi vitatu

1. Hisia (kiunganishi kikuu na cha awali).
2. Tabia (kikolezo cha kiungo kikuu)
3. Mtazamo (nyanja mbali mbali za maisha na namna ya kuendesha maisha)

Kwenye no. 2 na no. 3 hapa tunazungumzia (likes & dislikes, imani, uwekezaji, tendo la ndoa, mostly hata historia hua na ufanano uauopishana sana). Haya yataleta umoja wa kinafsi ambao ni mkubwaa.

Umewahi kua kwenye mahusiano ambayo ukimwa na muhusiano wako anaumwa akiwa kwenye moment ngumu kihisia na wewe unapitia? Kama jibu ndio basi huu ndio muunganiko wa kinafsi.

Back to the point.

Mkuu tumia hekima na busara usiwekeze kwake naye asiwekeze kwako kuwe na emotion balance, ambayo haitaleta changes yoyote kwenu na familia zenu. Mfundishe kuhandle hisia zake za sasa. Trust me it is very possible without SEX.
 
Mara paa umebambwa na jamaa yake mko sehemu mnafanya yenu,mara paa mkeo naye kajua,hapo ndio utakapojua kuwa shetani hana maana hata kidogo kwenye hii dunia...
 
Back
Top Bottom