Urafiki Gani Huu...!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,724
Wanajamvi nambieni...

Ni urafiki gani huu, kati ya usingizi na kifo?
Ni undugu gani huu, kati ya hofu na mauti?
Ni ujirani gani huu, kati ya mashaka na upotevu?

Ni ushirika gani huu, kati ya ugonjwa na mahututi?
Ni umoja gani huu, kati ya jeneza na kaburi?
Ni mapenzi gani haya, kati ya mfu na sanda?
 
Ni urafiki nafiki
Nadhifu husio adilifu
Urafiki wa lazima siku nzima
Maisha ya daima pasipo dhima
uuuiiiii uuuuiiiiii uuuuiiiiiiii

duh!!! Mzeiya PJ huu utenzi wako umenisikitisha sana mpaka nimefikiria kuachia ngazi JF, it makes me sad all the time when i read it
 
Huo sio urafiki, usojuana kwa dhiki
viwili havipikiki, na moto haviinjiki
kamwe usitake dhiki, kivifanya marafiki
kifo, sanda, mauti, ni njia za kwenda kwetu!
 
urafiki wa kinafiki
uhusiano wa kifedhuli
Ushirikiano wa kibandudi
urafiki usi mashiko,
urafiki wenye majonzi
 
urafiki kafiri
urafiki wa siri
urafiki wa majonzi
urafiki wa machozi
urafiki wa nakozi
urafiki wa mapozi
urafiki wa makofi
urafiki wa mbali
urafiki si mbali
urafiki mauti
urafiki sio mahususi
 
Back
Top Bottom