Urafiki au Upumbavu au ? : Kununuliana BIA kwenye sehemu za Starehe!

BE inaonyesha wewe ni bahili sana......................

Bill-Of-Quatity:

Siyo "mkono wa birika", bali inanikera sana mtu kuninulia bia akiwa anategemea na mimi nimnunulie bia in the near future!
 
Kwani wakati naenda bar nilijua kama nitakutana na wewe?

Ha ha ha jamanai mwanaume mchoyo wewe??? Kha!!!

Kama ndo hivyo unakunywa ya nini sasa mpaka ufikishe hizo bia (offer) tatu??? Acha basi mwambie Ashura arudishe kwa aliyemtuma.
 
@Nyambala:

Kwahiyo kununuliana bia ni dalili ya "kuwekeza"?

Scenario ninayoongelea iko hivi:

Mimi nimekwenda kumtembelea rafiki yangu Kunduchi Mtongani, baada ya kuagana naye napitia MALANJA "Executive?" INN kusudi kujiweka sawa kwa safari yangu ya kurudi Gongo La Mboto. Nipo kaunta nimesimama, naagiza bia yangu ya kwanza, mara anakuja "rafiki wa zamani" tunasalimiana, anakwenda kuketi. Dakika tatu baadaye "waiter" ananiletea bia na kuniambia "imetoka kwa yule baba"! Dakika kumi baadaye "offer" nyingine, dakika 30 baadaye "offer" ya tatu!

Sasa huo ndiyo "ukarimu" au "ulimbukeni"? Unawezaje kutengeneza marafiki kwa njia hiyo ya "bandika bandua" kwa mtu ambaye hamjaonana for "ages"?

Mkuu kama umenisoma vizuri kuhusu hiyo reciprocal, siyo kuwekeza bali ni ile ya kimtoni mtoni we are in a pub I buy one, you buy one papo kwa papo. Siyo eti mambo ya jana nilikununulia au juzi. Kwa hii scenario uliyoielezea hapa ofcourse ni kaulimbukeni tu flani!
 
Nakuunga tena mkono anajua budget zako,wanaonikera zaidi ni mijinaume inayojua kutangaza ufalme bar ikikukuta unakunywa kibia chako ..................halafu uliza baada ya hapo nini inafuata kikaratasi na ujumbe kwa mhudumu eti mawasiliano.............................kengeeeeeeeeeeeeeee wakubwa sijui nani aliwaambia tuna thamani ya bia moja na nyama choma.

Bill-Of-Quatity:

Siyo "mkono wa birika", bali inanikera sana mtu kuninulia bia akiwa anategemea na mimi nimnunulie bia in the near future!
 
Nakuunga tena mkono anajua budget zako,wanaonikera zaidi ni mijinaume inayojua kutangaza ufalme bar ikikukuta unakunywa kibia chako ..................halafu uliza baada ya hapo nini inafuata kikaratasi na ujumbe kwa mhudumu eti mawasiliano.............................kengeeeeeeeeeeeeeee wakubwa sijui nani aliwaambia tuna thamani ya bia moja na nyama choma.

Sijui ni macho yangu au kwa vile sijaingia JF muda kha!!! nimecheka sana aisee.

Ha ha ha eti kikaratasi mie kuna mmoja alijifanya eehhh Black Berry yako nzuri hebu nione jamaa likajibeep kesho likanipigia eti unanikumbuka tulikaa wote Mbezi Garden jana nilivyosikia tu hivyo hata sikuuliza alipataje namba nikakata na simu
 
Usicheke sana mpenzi ndo dunia na watu wake wana maudhi yasiyo na kipimo..............Halafu mie na kiburi changu cha kimanyema hata kama sina kitu mfukoni kujirahisisha sababu ya ofa za bar oteeeeeee mae kanyi.
Baba-Enock................HAKUNA URAFIKI HAPO NI UPUMBAVU.

Baada ya kuwa mywaji wa BIA kwa takribani miongo minne huwa najiuliza ni kwanini mtu anakukuta baa - hujamwalika wala hajakualika mnasalimia anakaa meza yake na baada ya muda anakuagizia kinywaji - "waiter/dada mpatie yule jamaa bia moja"! Huu utaratibu ni urafiki wa kweli au ni upumbavu au ni ishara ya nini?

Sijawahi kupata jibu - Naomba kuuliza!!!

Upumbavu
 
afadhali unaokutana nao bar kuna wale anakutafuta, anakupitia ofisini au nyumbani na tayari wameshapanga bar gani muende halafu mkifika bar,wanakutazama utasema wewe ndo baba yao hivi...... mimi huwa najiuliza,kama mtu hela huna,si ukae tu nyumbani?????????
 
Mimi nakushauri uache tu hyo pombe kwani imedumaza uwezo wako wa kufkr, yani umekunywa pombe miongo minne (miaka40) swali jepesi hvyo unajiulza leo.
 
afadhali unaokutana nao bar kuna wale anakutafuta, anakupitia ofisini au nyumbani na tayari wameshapanga bar gani muende halafu mkifika bar,wanakutazama utasema wewe ndo baba yao hivi...... mimi huwa najiuliza,kama mtu hela huna,si ukae tu nyumbani?????????

Hahahah..
"Kizuri kula na nduguyo." - Wahenga
 
Pass it around akikununulia moja anategemea na wewe utampiga round..., ni aina ya kushare umasikini na kusaidiana kuendeleza umasikini na kutiana hasara
 
Pombe zinaleta urafiki kwa haraka sana! Mimi nimepata marafiki wengi sana kupitia bar! Nimepata deals nyingi sana kupitia kwa marafiki wapya naokutana nao bar! Ukitaka kupata potential informations kutoka kwa mtu ambaye unaona una upotential fulani, wewe mnunulie bia!!
Bia is everything meen!!
Maneno yako sadakta Mkuu. Mzee wangu mmoja aliwahi kuniambia:
"Marafiki wangu wote nimewapata kwenye glasi ya wiski na wala sio kwenye kikombe cha maziwa". Hii ni kuunga mkono upataji wako wa marafiki.
Lakini pia kuna sehemu nyengine tunakoweza kupata marafiki wa kweli kama vile vyuoni, kazini, kwenye mikusanyiko ya kijamii na michezo, safarini n.k.
Ninaposema marafiki wa kweli, hawa wa kukutana baa binafsi huwa ninawaweka upande kwani urafiki wenu "unaweza kuanzia kwenye glasi na kuishia humo humo". Mfano, katika mazingira mengine, siku hukuenda bar "marafiki zako" watagundua haraka kuwa hupo, lakini hilo halitawazuwia wasijipatie 1Moto 1Baridi zao. "Wanaweza hata "kunywa kwa afya yako" lakini usitarajie kuwa iko siku watahangaika kweli kujua kulikoni ikiwa siku 3 huonekani baa. Kubwa wanaweza kusema tu, "Acchanna nnayye b-bwa- bwanna. Jamaa atta-kuwa ama ka- kacha-ccha au ka-ffa na kufariki. Si unajua tena, ka-udedi. Waiter, lette ka-mma tul-tullivyo happa".
 
@Nyambala:Kwahiyo kununuliana bia ni dalili ya "kuwekeza"?Scenario ninayoongelea iko hivi:Mimi nimekwenda kumtembelea rafiki yangu Kunduchi Mtongani, baada ya kuagana naye napitia MALANJA "Executive?" INN kusudi kujiweka sawa kwa safari yangu ya kurudi Gongo La Mboto. Nipo kaunta nimesimama, naagiza bia yangu ya kwanza, mara anakuja "rafiki wa zamani" tunasalimiana, anakwenda kuketi. Dakika tatu baadaye "waiter" ananiletea bia na kuniambia "imetoka kwa yule baba"! Dakika kumi baadaye "offer" nyingine, dakika 30 baadaye "offer" ya tatu!Sasa huo ndiyo "ukarimu" au "ulimbukeni"? Unawezaje kutengeneza marafiki kwa njia hiyo ya "bandika bandua" kwa mtu ambaye hamjaonana for "ages"?
Kwa mazingira hayo inabidi mkae meza moja mbadilisheni mawazo mpeane za kutoonana kitambo la sivyo muhudumu akija tena anaweza akakuambia "samahani yule jambazi anaomba uhamie kwenye meza yake kaunta ye hawezagi kukaa".
 
kama kweli hutaki kemea hiyo roho ya kununuliwa bia ili walau uongoze muongo mmoja mbeli hujanywa kabisa.
 
afadhali unaokutana nao bar kuna wale anakutafuta, anakupitia ofisini au nyumbani na tayari wameshapanga bar gani muende halafu mkifika bar,wanakutazama utasema wewe ndo baba yao hivi...... mimi huwa najiuliza,kama mtu hela huna,si ukae tu nyumbani?????????

The Boss,

Hii ni kali sana, lakini zipo sana pia...

Mtu anaku-beep, unampigia, anakwambia njoo akupe "bia moja" Maryland, unachukua Bajaj, unafika pale unamkuta amekaa na "timu", anakukaribisha na kukutambulisha, anakununulia bia moja, halafu ukimaliza anakwambia, vipi naomba tuongee kidogo, mkienda "chemba" anakwambia "hana kitu" kwahiyo "umlinde"! Mwisho wa yote unanunua round mbili au tatu halafu ukitaka kuondoka anakwambia "unaniachaje bro"! SHAME!!!
 
mkuu
ndo sababu mimi sina marafiki wa pombe
mbaya zaidi unaweza kukuta keshaopoa na kimwana
na pesa ya gesti hana,anakusubiri umuokoe,watu wa ajabu mno
na ukimkatalia uadui unaanza,
mwingine unakuta kushasambaza uongo kuwa
unamletea pesa yake,kumbe hakudai wala nini...
wewe ndo unamkopesha,watu wako funny....
 
mkuu
ndo sababu mimi sina marafiki wa pombe
mbaya zaidi unaweza kukuta keshaopoa na kimwana
na pesa ya gesti hana,anakusubiri umuokoe,watu wa ajabu mno
na ukimkatalia uadui unaanza,
mwingine unakuta kushasambaza uongo kuwa
unamletea pesa yake
,kumbe hakudai wala nini...
wewe ndo unamkopesha,watu wako funny....

Hii nilikuwa siifahamu, kumbe ndiyo maana unafika kwenye meza watu wanakuangalia kama vile umekuja kuomba Bia?

Nimecheka kwa sauti mpaka watu wamestuka!
 
Maneno yako sadakta Mkuu. Mzee wangu mmoja aliwahi kuniambia:
"Marafiki wangu wote nimewapata kwenye glasi ya wiski na wala sio kwenye kikombe cha maziwa". Hii ni kuunga mkono upataji wako wa marafiki.
Lakini pia kuna sehemu nyengine tunakoweza kupata marafiki wa kweli kama vile vyuoni, kazini, kwenye mikusanyiko ya kijamii na michezo, safarini n.k.
Ninaposema marafiki wa kweli, hawa wa kukutana baa binafsi huwa ninawaweka upande kwani urafiki wenu "unaweza kuanzia kwenye glasi na kuishia humo humo". Mfano, katika mazingira mengine, siku hukuenda bar "marafiki zako" watagundua haraka kuwa hupo, lakini hilo halitawazuwia wasijipatie 1Moto 1Baridi zao. "Wanaweza hata "kunywa kwa afya yako" lakini usitarajie kuwa iko siku watahangaika kweli kujua kulikoni ikiwa siku 3 huonekani baa. Kubwa wanaweza kusema tu, "Acchanna nnayye b-bwa- bwanna. Jamaa atta-kuwa ama ka- kacha-ccha au ka-ffa na kufariki. Si unajua tena, ka-udedi. Waiter, lette ka-mma tul-tullivyo happa".
Nakubaliana na wewe kwa some extent lakini pia kuna vitu ambavyo pia unatakiwa uvifahamu.
marafiki unaokutana nao vyuoni au mashulen ni wa muda tu, mkimaliza chuo kila mtu anakuwa kivyake!
makazini nako sidhani kama kuna urafiki wa kweli! wengi mtakuwa na job relationship lakini baada ya kazi kila mtu anafuata interest zake
michezoni, siyo kila siku mnaweza kuonana!
Ukiangaliaa bar.... ni rahisi sana kushare vitu flani, vya kifamilia, kiuchumi na vingine vingi tu!
kwenye pombe mnakuwa na mda mrefu wa kuzungumza, unaweza ukakaa baa kuanzia saa 11 jion mpaka saa 6 usiku bila kuboreka
Baa kunakuepushia mambo mengi hasa kero za wife nyumbani!(kwa waliooa mtazifahamu)
Kwenye pombe kila siku unapata mambo mapya!
 
Usicheke sana mpenzi ndo dunia na watu wake wana maudhi yasiyo na kipimo..............Halafu mie na kiburi changu cha kimanyema hata kama sina kitu mfukoni kujirahisisha sababu ya ofa za bar oteeeeeee mae kanyi.
Baba-Enock................HAKUNA URAFIKI HAPO NI UPUMBAVU.

HAA! sister angu kabisa.mi sikujua kama hivi vitu vinarithishwa bana!inawezekana nimerithi hii kitu(kibri,japo ni sunna tu) dadake.
kweli bana nyie sio wa bia na nyama choma,hebu wekeni viwango pale juu kidogo afu muone kama wahudumu watakuwa na kazi ya kusafirisha vikaratasi vyenye namba za simu tena!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom