URA SACCOS yatoa vifaa tiba kwa Jeshi la Polisi Tanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Polisi.jpg

Chama cha Akiba na Mikopo cha Jeshi la Polisi Tanzania, URA SACCOS kimekabidhi vifaa tiba pamoja na kompyuta kwa vikosi vya Jeshi la Polisi Tanzania.

Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali ya Jeshi hilo iliyopo Kunduchi, Simiyu na Kumpyuta kwa ajili ya Kikosi cha Ufundi na kikosi cha Bohari Kuu ya Jeshi la Polisi.

Akikabidhi katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi hizo jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya URA SACCOS, Festo Christopher Mwikuni amesema vifaa hivyo vinathamani ya Tsh. 40,361,000 ikiwa ni kutimiza takwa la kisheria la kurudisha faida kwa jamii inayowazunguka.


Amesema Bodi ya Chama hicho pamoja na wanachama wanaamini vitatumika kwa manufaa ya Jeshi la Polisi na wananchi kwa ujumla.

Awali, Mkuu wa Kikosi cha Afya, Kamishna Saidizi wa Polisi, Hussen Yahaya na Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi Kamishna Msaidizi Fadhili Ishekazoba pamoja na Mkuu wa Kikosi cha Bohari Kamishna Msaidizi Moses Mziray kwa pamoja wamekishukuru Chama hicho kwa msaada huo kwani umekuja wakati muafaka.
 
Sasa hiyo si wenyewe kwa wenyewe wangeshea kwenye magroup yao ya WhatsApp tu.
 
Back
Top Bottom