Upweke

SaraM

Senior Member
Sep 8, 2011
162
109
Habari za Jumapili ndugu zangu wapendwa, nimekuwa najiuliza hili swala,
kila mtu akiwa na upweke ana njia yake ya kuondoa upweke alionao
na mimi pia huwa nina njia zangu za kuondoa upweke nilio nao,lakini kwa
sasa nahisi nafeli, tangu juzi najiona mpweke sana,huwa wa kwanza kuwashauri
marafiki zangu wanapopatwa na hali hii, lakini inaonekana kwangu nimeshindwa
embu marafiki zangu niambieni ni njia gani rahisi ya kuondoa upweke na
kuwa na furaha kama siku nyingine???
 
  • Kumbuka hauko mpweke peke yako.. wako wengi sana..kwenye hali kama yako...
  • Upweke una mwisho labda kama mwenyewe wataka uwe hivyo.
  • Wakati unasubiri mwisho wa upweke tafuta kitu ambacho kitavuta muda na kuchosha akili ili ufike kesho...
Mwisho... Usitafute njia ya mkato kutuliza upweke..utakuja kulia!
 
keep yrself busy, kiasi kwamba ukirudi home unazima tu kwa uchovu. Ukishindwa tafta mwenza
 
na nyie washauri mgonjwa hajajielezea ana aina gani ya upweke mshamdunda sindano ya kutafuta mpenzi!
 
Habari za Jumapili ndugu zangu wapendwa, nimekuwa najiuliza hili swala,
kila mtu akiwa na upweke ana njia yake ya kuondoa upweke alionao
na mimi pia huwa nina njia zangu za kuondoa upweke nilio nao,lakini kwa
sasa nahisi nafeli, tangu juzi najiona mpweke sana,huwa wa kwanza kuwashauri
marafiki zangu wanapopatwa na hali hii, lakini inaonekana kwangu nimeshindwa
embu marafiki zangu niambieni ni njia gani rahisi ya kuondoa upweke na
kuwa na furaha kama siku nyingine???
Nivigumu kukueleza njia zakuondoa upweke mpaka wewe uwe umetwambia ni upweke gani ulio nao then from there we can do something good here!Nakama unaona noma kueleza Pm kati ya watu walio kupa mawazo hapa na uhakika watakujibu kwa pm nasiajabu ukajikuta unarudisha furaha yako kwa mda wote!
 
  • Kumbuka hauko mpweke peke yako.. wako wengi sana..kwenye hali kama yako...
  • Upweke una mwisho labda kama mwenyewe wataka uwe hivyo.
  • Wakati unasubiri mwisho wa upweke tafuta kitu ambacho kitavuta muda na kuchosha akili ili ufike kesho...
Mwisho... Usitafute njia ya mkato kutuliza upweke..utakuja kulia!
Kweli kabisa sijui kwa nn kila ninachofanya naona hakinipendezi
 
Nivigumu kukueleza njia zakuondoa upweke mpaka wewe uwe umetwambia ni upweke gani ulio nao then from there we can do something good here!Nakama unaona noma kueleza Pm kati ya watu walio kupa mawazo hapa na uhakika watakujibu kwa pm nasiajabu ukajikuta unarudisha furaha yako kwa mda wote!
Hakuna kipindi unaona kila kitu kibaya unachofanya hufurahii, na wala hujui unataka nini
 
alafu saraM unauwezo mzuri wa kutoa sln ya tatizo coz utakavyokuwa makini ku collect data ndivyo utakavyokuja na best sln
really!
kwa hiyo nicollect kwanza data naweza kukuta soln in between sio
 
Nivigumu kukueleza njia zakuondoa upweke mpaka wewe uwe umetwambia ni upweke gani ulio nao then from there we can do something good here!Nakama unaona noma kueleza Pm kati ya watu walio kupa mawazo hapa na uhakika watakujibu kwa pm nasiajabu ukajikuta unarudisha furaha yako kwa mda wote!

Jibu hili hapa. Lifanyie kazi.
 
Hakuna kipindi unaona kila kitu kibaya unachofanya hufurahii, na wala hujui unataka nini

Vingine ni vipindi vya kawaida sana na ni vya mpito! Waweza refresh kwa kusafiri, hii itakusaidia kubadilisha mazingira na kukutana na watu wengine zaidi ya wale ulowazoea kila siku na vilevile huchangamsha akili kwa kupata ideas tofauti tofauti!
 
Binadamu ametawaliwa na agenda kuu moja tu, hiyo ikikosekana mengi yataharibika!
Nayo ni Mpenzi anaekupa MAPENZI ya kweli yenye kukutoa ktk ulimwengu wa kawaida na kukudumbukiza ktk ulimwengu usioelezeka hata kidogo!

Nakusihi Sara tuliza akili yako muweke mungu mbele huku ukimweleza shida yako nae atashusha mkono wake juu yako!

Kwa msaada zaidi ni PM
 
Kuhisi upweke for just a day, ni kitu cha kawaida, lakini hali ya upweke au sononi, ikikukamata for more than a week, then hapo kuna tatizo. Lakini hali ya kuhisi upweke kwa siku moja au mbili umkuta kila mtu katika maisha ya kila siku...! Jitahidi kuwa busy.

Jishughulishe na kazi za nyumbani kama vile usafi au tembelea jamaa na marafiki ambao wewe unaelewana nao sana...!

Epuka kuondoa upweke kwa kunywa pombe au kufanya ngono, hii itakupelekea kuwa addicted na mambo hayo.
 
Kitu kimoja ni kujihisi uko mpweke, chengine ni kujiona au kuchagua kuwa peke yako. Hii ya pili ni ya muda sana au pengine ya kujichagulia.
Aina ya mwanzo ni hisia za kutokuwa na mtu wa karibu au mwenza wa kushare naye mawazo, iwe mpenzi au rafiki. Pengine ni kwa sababu ya stress tu za kazi na maisha. Kama sio ugonjwa, upweke ni suala la muda tu.

Kuhusu namna ya kuwa na furaha, nakumbuka mwanandishi mmoja wa Kiyahudi (jina nimesahau), alisema "Kitu pekee cha kukufanya uwe na furaha ni kazi na marafiki". Hakutaja wapenzi wala familia. Nadhani kwa sababu wapenzi na familia mara nyengine wanaweza kutusaliti, watoto na wapenzi wanaweza kukutoka, ama kwa sababu wana maisha yao, wanaweza kuwa mbali nasi na si kila kitu tunapaswa kuwaeleza wao; Mungu anaweza kuwahitaji au wakaamua kutuwacha. Wanaokuwepo karibu yako siku zote ni rafiki zako na kazi au amali yako.

Ushauri wangu kwa hivyo ni kuwa kukimbilia kwa rafiki mkweli na mwaminifu wa kuongea naye, angalau kwa kutoa dukuduku lako. Huyu atakushauri na kukupa moyo. Si pombe, wala ngono kama walivyoshauri wengi.
 
unashida gani...???????? sema usikike.. kuna watu wa kila aina humu wa kukusaidia
 
Habari za Jumapili ndugu zangu wapendwa, nimekuwa najiuliza hili swala,
kila mtu akiwa na upweke ana njia yake ya kuondoa upweke alionao
na mimi pia huwa nina njia zangu za kuondoa upweke nilio nao,lakini kwa
sasa nahisi nafeli, tangu juzi najiona mpweke sana,huwa wa kwanza kuwashauri
marafiki zangu wanapopatwa na hali hii, lakini inaonekana kwangu nimeshindwa
embu marafiki zangu niambieni ni njia gani rahisi ya kuondoa upweke na
kuwa na furaha kama siku nyingine???

upweke gani sasa sara fafanua bwana upo wap kwanza Dar au mkoani kama ni Pm.
 
Back
Top Bottom