Upuuzi wa TBC1: Rais Kikwete atukanwa 'live' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upuuzi wa TBC1: Rais Kikwete atukanwa 'live'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hilbajojo2009, Oct 27, 2010.

 1. h

  hilbajojo2009 Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MALALAMIKO ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya kampeni za mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa kuwa zimejaa matusi, yalidhihiri jana pale kampeni za mgombea huyo zilipotumika kumtukana Rais Jakaya Kikwete na mama yake mzazi.

  Kabla ya kuanza kumtukana Rais wa nchi ambaye pia ni mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Slaa mwenyewe alitamba kuwa katika viwanja hivyo vya Mwembeyanga, Temeke ndipo alipotoa tuhuma dhidi ya viongozi wengine bila kushitakiwa wala kukamatwa.

  Dk. Slaa ambaye alianza hotuba yake kwa kutoa maneno machafu dhidi ya CCM na viongozi wake na kutumia muda kidogo kuelezea hoja za Ilani ya uchaguzi ya chama chake na kujibu hoja za wapinzani wake, kabla ya kumaliza alitoa nafasi kwa mgombea ubunge wa Temeke kuonesha umahiri wa kujenga hoja.

  Mbali na kumpa nafasi mgombea huyo aoneshe umahiri huo kwa dakika mbili ili apimwe kama anaweza kutumia dakika tatu wanazopewa wabunge kujenga hoja bungeni, Dk. Slaa aliwaomba wananchi wampigie kura mgombea huyo, kwa kuwa kupitia wagombea wa ubunge wa Chadema akiwemo huyo, ndipo anapotarajiwa kumpata Waziri Mkuu na mawaziri wengine wasiozidi 20.

  Hata hivyo mgombea huyo, Dickson Amos, alitumia nafasi hiyo kumtukana matusi ya kumdhalilisha Rais Kikwete na mama yake mzazi na kusababisha matangazo ya moja kwa moja ya TBC1 kutoka katika viwanja hivyo, kukatishwa ghafla ili kustahi ustaarabu wa jamii ya kitanzania.

  Matusi hayo ambayo ni aibu kuyaandika, yalitolewa katika mkutano wa hadhara na uliokuwa ukisikilizwa na wasikilizaji mbalimbali wa TBC 1 nchi nzima.

  Katika muda mfupi alioutumia kujibu hoja zilizoelekezwa kwake na wapinzani wake kisiasa, Dk. Slaa alisema hahitaji shahada ya uzamivu kwa ajili ya kusimamia masuala ya uchumi wa nchi.

  Alikiri kweli yeye ni mbumbumbu wa uchumi kwa sababu amesomea sheria, lakini uchumi aliosoma mwaka 1972 unatosha kujua hali ya Mtanzania na jinsi ya kumsaidia.

  Alikuwa akimjibu Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala aliyesema mgombea huyo hajui mambo ya uchumi na kumtaka aache kuyajadili.

  Aliwataka Watanzania kumpatia wabunge wengi wa Chadema ambao watafuta sheria iliyopandisha bei ya bati na ya saruji na kudai kuwa Watanzania wanalipa kodi nyingi katika bidhaa zao kuliko hata ilivyo kwa nchi za Afrika Mashariki.

  “Kama Dk. Kamala haelewi ninachosema akasome gazeti la East Afrika ukurasa wa tatu, ila nina mashaka kama anajua Kiingereza vizuri… na afahamu kuwa Dk. Slaa ni rais wa Watanzania na sio wa Afrika Mashariki,” alisema na kuongeza kuwa yuko tayari kufuta mikataba yote inayowaumiza wananchi.

  Source: Habari leo 27/10/2010
   
 2. h

  hilbajojo2009 Member

  #2

 3. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kumbe ni gazeti la habari leo!
  Hawa wanatumikia ccm badala ya serikali. Hakuna mkutano wa kampeni usio na 'vijembe'
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Nonsese kabisa!!!! Acheni hizo Habari Leo -- tunawafahamu nyie ni mawakala wa CCM pamoja na kwamba mnalipwa kutokana na kodi zetu. Hamujwezi kuongeza mauzo ya gazeti lenu kwa crap ya namna hii Niliiangalia hotuba yote live -- hakuna matusi -- ni shutuma juu ya shutuma ya utawala mbovu wa JK, binafsi kupenda anasa badala ya kushughulikia umasikini wa Wananchi, kuwalea mafisadi na kuwapigia debe pamoja na kwamba wana kesi mahakamani.

  Dr Slaa alisema pamoja na JK kuwa mbunge wa Bagamoyo karibu 20 yrs, hakufanya lolote, watu wengi wa kwake huko ni masikini sana, atafanyaje kwa Tanzania nzima?

  Aliloambiwa JK ni hali halisi ya utawala wake, na si matusi, labda tu hayo yalitamkwa kwa njia ya ukali, kwani afanyayo rais huyu yanaudhi kwelikweli!!!
   
 5. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,026
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Na hayo matusi ni yapi tena Methali ni matusi?
  Basi tusingezitumia mashuleni
  baada ya maelezo, Alisema "JK hakufunzwa na mamaye, na asiyefunzwa namamaye atafunzwa na Ulimwengu"

  Kwani hilo ni Tusi? Na TBC1 walikata saa ngapi? Mbona mimi kwangu haikukata au ndo wale wanaotumia kwa diwani wa CCM
   
 6. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Ila ni vema wabunge wathibiti ndimi zao kipindi hiki cha kampeni wachunge maneno wanayosema yasije kutumika kama mtego wa kuwanasa. Huyu Bwana Dickson nilimsikia na sikufurahia sana personal attack aliyo elekeza kwa JK na mama yake. Ukweli hakutakiwa kumhusisha mama yake JK kwenye matusi ya kumwita JK hana adabu na hukufunzwa na mama yake basi sisi tutamfundisha adabu ili awaheshimu watanzania. Hii kwangu nasema alikwenda EXTREME katika utashi tu wa kawaida. Nafikiri angemwita fisadi, mwizi au Mwongo nisingekuwa na shida.

  CHADEMA HOYEEEEEEEEEEEEEEE
  TUMPE DK SLAA KURA ZETU ILA PIA TUWAONYE WANAOTAKA KUMFANYA AONEKANE HANA STAHA
   
 7. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Kuandika tu katukanwa bila kuweka hata tusi mojawapo ni falacy. Kila hoja inayotolewa lazima iwe na ushahidi. Nadhani waandishi wa habari wanatumika vibaya hapa. Ni aibu kubwa. Kama hakuna ushahidi hakuna haja ya kuandika!
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,686
  Likes Received: 21,950
  Trophy Points: 280
  Yule mgombea ubunge alisema bwana mkubwa hana adabu kwa vile anawadanganya waTZ wadogo kwa wakubwa. Mtu anayewadanganya waliomzidi umri kumwambia hana adabu sio tusi ila ni kumfahamisha hiyo tabia yake "ya kukosa adabu" aiache.
  Mtu nzima mwenzio akikudanganya anakuwa kakudharau na kakuvunjia heshima(adabu).
   
 9. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu bado unasoma hilo gazeti? Hilo tangu lianze limekuwa chombo cha propaganda cha CCM. Bila shaka wahariri wake hawajui wajibu wao kama gazeti la umma. Lakini ma-spy wangu wanasema mmoja wa wahariri, waliyemtaja kwa jina la Kingoba, ni swahiba sana wa JK na muda wote wa kampeni yupo naye. Huyu naambiwa ana nguvu na ndiye anayefanya maamuzi ya kupindisha habari zote zinazochapwa na gazeti hili kumpendelea Kikwete. Uzuri ni kwamba hakuna watu makini wanaosoma gazeti hili lililogeuka kuwa la udaku, na hata mauzo yake ni duni sana kama lyalivyo Uhuru na Mtanzania (gazeti la Rostam).
   
 10. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Mbona washindani wakiitwa na wana CCM makapi, mbumbumbu, wazinzi... sijawahi kuona wanaandika CCM yawatukana washindani? NB: Sitaki kutumia neno 'wapinzani'. Kwa hiyo, ni washindani.
   
 11. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nonsese kabisa!!!! Acheni hizo Habari Leo -- tunawafahamu nyie ni mawakala wa CCM pamoja na kwamba mnalipwa kutokana na kodi zetu. Hamujwezi kuongeza mauzo ya gazeti lenu kwa crap ya namna hii Niliiangalia hotuba yote live -- hakuna matusi -- ni shutuma juu ya shutuma ya utawala mbovu wa JK, binafsi kupenda anasa badala ya kushughulikia umasikini wa Wananchi, kuwalea mafisadi na kuwapigia debe pamoja na kwamba wana kesi mahakamani.

  Dr Slaa alisema pamoja na JK kuwa mbunge wa Bagamoyo karibu 20 yrs, hakufanya lolote, watu wengi wa kwake huko ni masikini sana, atafanyaje kwa Tanzania nzima?
   
 12. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Mbona washindani wakiitwa na wana CCM makapi, mbumbumbu, wazinzi... sijawahi kuona wanaandika CCM yawatukana washindani? NB: Sitaki kutumia neno 'wapinzani'. Kwa hiyo, ni washindani.
   
 13. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa wa Habari Leo ma choko kweli.

  Jana walitumia tusi: "mbumbumbu"
  Leo wanakuja kwa kujitetea: "hajui"

  Mbona Habari Leo hamnazo? Yaani jana tu munafikiri tumesahau??
   
 14. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hivi tusi ni nini vile?
   
 15. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  "..........Matusi hayo ambayo ni aibu kuyaandika, yalitolewa katika mkutano wa hadhara na uliokuwa ukisikilizwa na wasikilizaji mbalimbali wa TBC 1 nchi nzima........"

  Mhhh sidhani kama alivyosema mwandishi wa habari leo kuwa ni sahihi yaani matusi hayo ni mazito hayafai kutajwa. Bahati nzuri mwenyewe nimeyasikia LIVE, alichosema yule mgombea ubunge wa Chadema (jimbo la temeke) japo siafikiani naye kwa maana kumuhusisha mzazi wa mtu ktk issues ambazo yeye hahusiki ni makosa kimsingi. Kama huyo jamaa anasema JK hakufundishwa na mama yake ndio maana anafanya kama anavyofanya, kwa mtazamo wangu NAFIKIRI HATA HUYU MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA NAYE PIA HAJAFUNDISHWA NA MAMA YAKE, MAANA KWA MWENYE AKILI YEYOTE ASINGESEMA KAMA ALIVYOSEMA. JAMII YETU INATUFUNDISHA KUHESHIMU WATU WAZIMA, HATA KAMA SI MZAZI WAKO. UNAPOMTUSI MZAZI WA MWENZIO NI SAWA NA KUMTUSI MZAZI WAKO.

  BAADA YA KUMSIKILIZA HUYU MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA NAPATA WASIWASI KAMA KWELI HUYU JAMAA NI MWANACHADEMA DAMU DAMU NA SIO MTU ALOPANDIKIZWA ILI CHADEMA WALIKOSE JIMBO HILO. KABLA YA MATUSI YA HUYO JAMAA NILIAMINI KUWA MWAKA HUU CHADEMA ITAPATA MAJIMBO YOTE YA DAR, LAKINI BAADA YA MATUSI YA HUYO JAMAA NIKASIKITIKA SAANA NA KUSEMA BASI CHADEMA WESHAPOTEZA HILO JIMBO. NAWAOMBA SAANA VIONGOZI WA JUU WA CHADEMA KUWA KWA MUDA ULIOBAKI WAJIEPUSHE NA BLANDA KAMA ALIZOFANYA HUYU JAMAA HIYO JANA
   
 16. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hivi hilo gazeti linauza nakala ngapi mana wanaonunua ni
  .ccm

  .maofisa wake wa juu wizarani ili walinde ajira zao.
  .wapambe wa mama salma
  .wapambe wa jk

  big up to mwananchi,tz daima na nipashe
   
 17. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Alichosema ni sawa sawa kabisa kama Kikwete anaona katukanwa akashitaki.Halafu nyie habari leo mumefulia ndiyo maana mnaitwa toilet paper badala ya gazeti
   
 18. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi kumwita mtu photocopy ni sifa eeh?
   
 19. The Native Son

  The Native Son Member

  #19
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Waandishi kama huyu ndo huwa nawaona wana- Paralysis of Analysis, wanazongwa na "Emotions" tu.
   
 20. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Habari Leo!!! Duh!! Kwanza hata hawajui kwa nini watu wana chuki dhidi ya CCM na JK wao!!! Wapinzani wanahangaika viwanja vya kufanyia mikutano kutokana na roho mbaya ya CCM -- wanawakatalia viwanja walivyopora!!! Hii ni roho mbaya sana -- inaudhi na inapandisha hasira.
   
Loading...