Upuuzi wa Kocha Pablo wa Simba SC unavyozidi kuisafishia Yanga SC njia ya kuwa Mabingwa wa NBC Premier League kwa 75% mpaka sasa

Unajua wabongo tupunguze ujuaji,,hivi katika football timu gani haifungwi??
Au nyie mlitaka kila mwaka simba achukue ubingwa itakuwa bado ni ligi au ibadilishwe iitwe Simba premier league
Ufungwe ukiwa na class players hakuna atakae laumu maana hata Munich anafungwa ,ila sio kufungwa huku una wachezaji wa kawaida ,imefika hatua hata timu vibonde wanajiamini Sana wakutanapo na Simba wakat haikua hivyo ,vitimu vidogo vilikua vinaingia uwanjani kwa waswas na kupata kujiamin katikat ya game ,Sasa kabla ya game Kila kitimu kinajiaminisha kuwa kinaweza mfunga Simba.
Mfano mzuri kwasasa upo kwa timu ya Yanga ,ikatokea wamefungwa hakuna wa kulalamika Sana maana Kila idara wameenea hii mashabik wanaweza sema Ni ajari kazin ila Sio kwa hii Simba ambayo Ina magalasa Kama Mugalu na Bocco.
 
Siku nikiwa na akili kama zako NAJINYONGA (Nitaiga style ya mashabiki wenu)
Huchoki tu Kunishobokea GENTAMYCINE kila mara na kuzidi Kuniongezea Umaarufu ( Fame ) wakati umeshasema hunipendi na mpaka kuniita Mwehu?

Je, kwa Wewe kuendelea Kujibizana nami uliyenita Mwehu na Kuonyesha kutonikubali ( Kunipenda ) unadhani aliye Mgonjwa wa Akili hasa ni nani?

Kumbe ninapowadharau na Kuwajibuni hovyo huwa sikosei / siwakosei.
 
Inawezekana kweli yanga akawa bingwa ila ni mapema sana hata raundi ya pili bado mashabiki wa simba mnawasikiliza wachambuzi ucharwa.
Shida Ni fowards tulizonazo ,hata akil inakataa kwa kikosi kilichopo et kitaleta makali Kama ya msimu uliopita ,Ni kikosi Fulani Cha kuunga unga ,kocha nae haelewek Leo apange hivi kesho vile .

Angalia yanga Wana kikosi Cha Kwanza tayar na wanaokaa bench nao Ni watu haswa.
Rudi Simba ,mfano akiumia hussen et wakuziba pengo Gadiel ,kapombe nae kachoka balaa na mbadala wake Ni mwenda ,katikati wanategemewa akina mzamiru ambae hata control siful ,winga et Morrison mchezaji mbinafs sijapata kuona yeye bila kupiga chenga hajacheza mpira na ndie bingwa wa kupoteza mipira ,nenda mbele una mugalu na kagere ambao wanaruka ruka tu.

Ngoja tuone ujio wa chama hasa kwenye viwanja rafik tuone labda ataleta mabadiriko Fulani lakin swala la ubingwa big no.
 
Ufungwe ukiwa na class players hakuna atakae laumu maana hata Munich anafungwa ,ila sio kufungwa huku una wachezaji wa kawaida ,imefika hatua hata timu vibonde wanajiamini Sana wakutanapo na Simba wakat haikua hivyo ,vitimu vidogo vilikua vinaingia uwanjani kwa waswas na kupata kujiamin katikat ya game ,Sasa kabla ya game Kila kitimu kinajiaminisha kuwa kinaweza mfunga Simba.
Mfano mzuri kwasasa upo kwa timu ya Yanga ,ikatokea wamefungwa hakuna wa kulalamika Sana maana Kila idara wameenea hii mashabik wanaweza sema Ni ajari kazin ila Sio kwa hii Simba ambayo Ina magalasa Kama Mugalu na Bocco.
Wewe unatumwa na mihemuko. Haya tupe takwimu Simba kafungwa mara ngapi ili uipe nguvu hoja yako. Vinginevyo na wewe si shabiki wa mpira bali mpiga kelele tu.
 
Yaani Kocha kabisa umeshapoteza Mechi Mbeya halafu Mechi muhimu ya leo Morogoro unakuja Kumjaribu Beki Mbovu Gadiel Michael wakati Mchezaji mahiri Mohammed Hussein Tshabalala unae na hujataka Kumuanzisha?

Yaani Kocha kabisa una Wachezaji very talented and creative kama Chama na Morrison unaacha Kuwaanzisha unawaingiza baadae kabisa?

Yaani kabisa Kocha Sisi Watu wa Mpira tumeshaona kuwa John Boko tayari 'Kwishnei' Kisoka halafu Wewe unamtetea huku ukiendelea Kumpanga Kikosini wakati una Vijana au Wachezaji wengine very Competent wa Kuisadia Timu?

Tayari Kocha uko na Kikosi na umeshaona ukitoa tu Meddie Kagere huna tena Mshambuliaji mwingine unaacha kuuambia Uongozi uachane na Chris Mugalu ili haraka tusajili 'Striker' mpya unabaki kudemadema tu utafikiri Ligi Kuu ya NBC ni ya Babu zako uliowaacha huko Kijijini Kwanu Hispania?

UKWELI MCHUNGU

GENTAMYCINE mpaka sasa nawapa 75% Yanga SC kuwa Mabingwa labda tu 'Complacency' iwagharimu na wasipouchukua Ubingwa nitawadharau kuliko Maelezo kwani Kiuhalisia na Kimazingira wana dalili zote za kuwa Mabingwa.

KWENU WANA SIMBA SC WENZANGU

Ili Yanga SC isiwe Bingwa inatakiwa ama ifungwe Mechi 3 au itoke Sare Mechi 4 je, tukiacha Unafiki na Ushabiki wetu mnadhani kwa Yanga SC hii ya sasa na walivyojipanga Kimkakati ndani na nje ya Uwanja hili litawezekana?

Na kumbukeni wakati huo tunaiombea mabaya haya Yanga SC na Sisi Simba SC tunatakiwa Kushinda tu Mechi zetu zote zilizobaki je, kwa Upuuzi na Ubovu wa Kocha Pablo mnadhani Simba SC yetu hii itaweza kulifanya hili wakati tuna Wachezaji dhaifu na wasio na Uchungu na Simba SC yetu?

LAWAMA KWA VIONGOZI WA SIMBA SC

Uongozi wa Simba SC wa sasa hauko serious na umewekeza zaidi katika Mapato na Biashara lakini siyo Ushindani wa Simba SC Uwanjani.

Wenzetu ( Watani ) zetu wanasajili Majembe ili Kujiimarisha zaidi Kiushindani Sisi kutwa tunahimizwa tu Kuchangia Ujenzi wa Uwanja wetu ili Ujengwe haraka kana kwamba TFF wametufukuza katika Viwanja vilivyopo.

NANI KASEMA HAJI MANARA KWENDA YANGA SC HAKUNA MADHARA YOYOTE KWA SIMBA SC YETU?

Tena Kuondoka kwa Haji Manara Kumetuathiri pakubwa Simba SC kwani alichokifanya Manara ni kuwaambia wana Yanga SC ( Viongozi na Wadhamini ) Siri zote zilizoipa Ubingwa mara Nne ( 4 ) na Yanga SC sasa nao kupitia GSM na Pesa walizonazo wanapita mule mule alikokuwa akipita Simba SC ( hasa Tajiri Mo Dewji ) na kwa Kujidhatiti Kwao kubakia Kileleni mpaka Watangazwe Mabingwa.

MIUJIZA

Najua duniani kuna Maajabu ( Miujiza ) ya kwamba pamoja na Yanga SC kutamba hivi ila nao wanaweza Kuukosa Ubingwa huu na Simba SC akauchukua tena.

Kwa Uchezaji mbovu wa Simba SC wa sasa na Umakini wa Yanga SC ni Mwendawazimu tu pekee atakataa kuwa hadi sasa ( leo ) Yanga SC ana 75% za kuwa Mabingwa.

LAWAMA NA VISINGIZIO VYA KIPUMBAVU

Kuna Watu wanadai Simba SC inaonewa na kwamba Yanga SC wanapendelewa.

GENTAMYCINE nakataa isipokuwa ninachojua tu ni kwamba Yanga SC imesajili Wachezaji wa Matokeo na Simba SC tumesajili Wachezaji wa Maonyesho na 10% kwa baadhi ya Viongozi wa Simba SC.

Upuuzi mwingine ni huu baada ya Kufungwa na Mbeya City na Leo kutoa Suluhu na Mtibwa Sugar FC baadhi ya wana Simba SC wanadai Viwanja vilikuwa Kikwazo.

Nami nauliza kama Viwanja vya Sokoine ( Mbeya ) na Manungu ( Morogoro ) ni Vibovu na Kikwazo Kwetu Klabu yetu ya Simba SC imejenga wapi Uwanja wake?

Na kama Viwanja vilikuwa ni Vibovu vya Mbeya na Morogoro imekuwaje Wapinzani wetu wenye Miguu na Nguvu sawa na Sisi wao wameweza Kuvicheza na wala hawalalamiki au Kudeka kama Sisi?

NINI KIFANYIKE KWA SASA?

Tuache Kuiwazia Yanga SC 24/7 na Kucheza Mechi zao Kifitna ili Wafungwe au Watoke Sare tuweze Kuwakaribia bali tujitathmini wapi tumekosea kwa Msimu huu, tujisahahiihishe na tucheze Mechi zetu Kimkakati na tusiruhusu tena Kufungwa au hata kutoka Sare Mechi nyinginezo kuanzia sasa.

HITIMISHO

Wana Simba SC tukubali tu kuwa Kutesa ni kwa zamu na Watani zetu Yanga SC kwa Msimu huu wapo vyema na walijipanga vvema Kimkakati ( hasa Ndani na Nje ) ya Uwanja.

Viongozi wa Simba SC amkeni haraka!!

Cc: Daudi Mchambuzi
Andiko lako lilikuwa zuri..umeharibu pale kumuhusisha Manara (Msukule) na Kufanya vibaya kwa Simba. Hana lolote yule ni mdangaji. Mengine uliyoyaongea ni kweli. Pia kocha sipendezwi na matendo yake njeya uwanja..nina mashaka kama kweli ni "Proffessional Coach" ana madhaifu mengi kama wale makocha wa ligi za mchangani...tusijekuwa tumepigwa na Friends of Simba ( wazee wa recruitment)
 
Ishu ya Bocco na watu kama Dilunga kupangwa wakumlaumu ni Matola huyo mseng* watu tunataka matokeo yeye analeta ushkaji!

Jana unashangaa kapanga mastriker wawili halafu kaweka viungo defensive minded, hiyo mipira sijui mbele alitaka iende kwa uwezo wa roho mtakatifu

Simba game zaidi ya 10 bado haina first eleven wakati kila namba inajulikana wachezaji bora!

Halafu viongozi walitaka kumtema Lwanga wakifikiri Kanoute ataziba pengo au? Cha ajabu unataka kumtema Lwanga unamuacha Mugalu!

Pia watu wameridhishwa na kiwango cha Kibu wanasahau ile namba last season alikuwa anacheza Miquison! 😂😂 Simba hii ya wachezaji kama Kibu halafu tunawasifia, ubingwa tushaupoteza.

Mwisho next time Simba ikitimua bench la ufundi ihakikishe pia inamfuta kazi na Matola au inamhamisha nafasi.
 
Andiko lako lilikuwa zuri..umeaharibu pale kumuhusisha Manara (Msukule) na Kufanya vibaya kwa Simba. Hana lolote yule ni mdangaji. Mengine uliyoongea ni kweli. Pia kocha matendo yake nina wasiwasi kweli kama ni "Proffessional Coach" ana madhaifu mengi kama wale makocha wa lingi ya mchangani...tujikuwa tumepigwa na Friends of Simba ( wazee wa recruitment)
Kocha hana tatizo mkuu tatizo ni kocha mpya halafu kocha msaidizi ni wa zamani! If you know you know
 
Shida Ni fowards tulizonazo ,hata akil inakataa kwa kikosi kilichopo et kitaleta makali Kama ya msimu uliopita ,Ni kikosi Fulani Cha kuunga unga ,kocha nae haelewek Leo apange hivi kesho vile .

Angalia yanga Wana kikosi Cha Kwanza tayar na wanaokaa bench nao Ni watu haswa.
Rudi Simba ,mfano akiumia hussen et wakuziba pengo Gadiel ,kapombe nae kachoka balaa na mbadala wake Ni mwenda ,katikati wanategemewa akina mzamiru ambae hata control siful ,winga et Morrison mchezaji mbinafs sijapata kuona yeye bila kupiga chenga hajacheza mpira na ndie bingwa wa kupoteza mipira ,nenda mbele una mugalu na kagere ambao wanaruka ruka tu.

Ngoja tuone ujio wa chama hasa kwenye viwanja rafik tuone labda ataleta mabadiriko Fulani lakin swala la ubingwa big no.
Mkuu utanisamehe nimekutusi kimoyomoyo, Kagere yupi ambaye unamsemea hapa? Huyu huyu top scorer kwa misimu miwili mfululizo au? Huyu huyu aliyekuwa anatokea bench halafu akamaliza na goli 13 au?

Kagere sio tatizo, tatizo ni anaocheza nao, kutoka Okwi, Chama, Miquison mpaka kuwekewa winger Kibu na wakina Dilunga bila shaka ushaona tofauti?

Cha mwisho nikukumbushe tu Kagere ndio top scorer wa Simba msimu huu, acha mihemko.
 
koch anatuangusha sana na upangaji kikosi wake tangu gem ya mbeya city nilishangaa kweli kuona anaweka viungo wakabaji watatu. sjui ana tatizo gani huyu mspain

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tumwambie bila kuficha matola aache kuchukua kamisheni kwa akina mugalu ,boko and nk ,umeipa yanga 75percent Basi Mimi 85
 
Yaani Kocha kabisa umeshapoteza Mechi Mbeya halafu Mechi muhimu ya leo Morogoro unakuja Kumjaribu Beki Mbovu Gadiel Michael wakati Mchezaji mahiri Mohammed Hussein Tshabalala unae na hujataka Kumuanzisha?

Yaani Kocha kabisa una Wachezaji very talented and creative kama Chama na Morrison unaacha Kuwaanzisha unawaingiza baadae kabisa?

Yaani kabisa Kocha Sisi Watu wa Mpira tumeshaona kuwa John Boko tayari 'Kwishnei' Kisoka halafu Wewe unamtetea huku ukiendelea Kumpanga Kikosini wakati una Vijana au Wachezaji wengine very Competent wa Kuisadia Timu?

Tayari Kocha uko na Kikosi na umeshaona ukitoa tu Meddie Kagere huna tena Mshambuliaji mwingine unaacha kuuambia Uongozi uachane na Chris Mugalu ili haraka tusajili 'Striker' mpya unabaki kudemadema tu utafikiri Ligi Kuu ya NBC ni ya Babu zako uliowaacha huko Kijijini Kwanu Hispania?

UKWELI MCHUNGU

GENTAMYCINE mpaka sasa nawapa 75% Yanga SC kuwa Mabingwa labda tu 'Complacency' iwagharimu na wasipouchukua Ubingwa nitawadharau kuliko Maelezo kwani Kiuhalisia na Kimazingira wana dalili zote za kuwa Mabingwa.

KWENU WANA SIMBA SC WENZANGU

Ili Yanga SC isiwe Bingwa inatakiwa ama ifungwe Mechi 3 au itoke Sare Mechi 4 je, tukiacha Unafiki na Ushabiki wetu mnadhani kwa Yanga SC hii ya sasa na walivyojipanga Kimkakati ndani na nje ya Uwanja hili litawezekana?

Na kumbukeni wakati huo tunaiombea mabaya haya Yanga SC na Sisi Simba SC tunatakiwa Kushinda tu Mechi zetu zote zilizobaki je, kwa Upuuzi na Ubovu wa Kocha Pablo mnadhani Simba SC yetu hii itaweza kulifanya hili wakati tuna Wachezaji dhaifu na wasio na Uchungu na Simba SC yetu?

LAWAMA KWA VIONGOZI WA SIMBA SC

Uongozi wa Simba SC wa sasa hauko serious na umewekeza zaidi katika Mapato na Biashara lakini siyo Ushindani wa Simba SC Uwanjani.

Wenzetu ( Watani ) zetu wanasajili Majembe ili Kujiimarisha zaidi Kiushindani Sisi kutwa tunahimizwa tu Kuchangia Ujenzi wa Uwanja wetu ili Ujengwe haraka kana kwamba TFF wametufukuza katika Viwanja vilivyopo.

NANI KASEMA HAJI MANARA KWENDA YANGA SC HAKUNA MADHARA YOYOTE KWA SIMBA SC YETU?

Tena Kuondoka kwa Haji Manara Kumetuathiri pakubwa Simba SC kwani alichokifanya Manara ni kuwaambia wana Yanga SC ( Viongozi na Wadhamini ) Siri zote zilizoipa Ubingwa mara Nne ( 4 ) na Yanga SC sasa nao kupitia GSM na Pesa walizonazo wanapita mule mule alikokuwa akipita Simba SC ( hasa Tajiri Mo Dewji ) na kwa Kujidhatiti Kwao kubakia Kileleni mpaka Watangazwe Mabingwa.

MIUJIZA

Najua duniani kuna Maajabu ( Miujiza ) ya kwamba pamoja na Yanga SC kutamba hivi ila nao wanaweza Kuukosa Ubingwa huu na Simba SC akauchukua tena.

Kwa Uchezaji mbovu wa Simba SC wa sasa na Umakini wa Yanga SC ni Mwendawazimu tu pekee atakataa kuwa hadi sasa ( leo ) Yanga SC ana 75% za kuwa Mabingwa.

LAWAMA NA VISINGIZIO VYA KIPUMBAVU

Kuna Watu wanadai Simba SC inaonewa na kwamba Yanga SC wanapendelewa.

GENTAMYCINE nakataa isipokuwa ninachojua tu ni kwamba Yanga SC imesajili Wachezaji wa Matokeo na Simba SC tumesajili Wachezaji wa Maonyesho na 10% kwa baadhi ya Viongozi wa Simba SC.

Upuuzi mwingine ni huu baada ya Kufungwa na Mbeya City na Leo kutoa Suluhu na Mtibwa Sugar FC baadhi ya wana Simba SC wanadai Viwanja vilikuwa Kikwazo.

Nami nauliza kama Viwanja vya Sokoine ( Mbeya ) na Manungu ( Morogoro ) ni Vibovu na Kikwazo Kwetu Klabu yetu ya Simba SC imejenga wapi Uwanja wake?

Na kama Viwanja vilikuwa ni Vibovu vya Mbeya na Morogoro imekuwaje Wapinzani wetu wenye Miguu na Nguvu sawa na Sisi wao wameweza Kuvicheza na wala hawalalamiki au Kudeka kama Sisi?

NINI KIFANYIKE KWA SASA?

Tuache Kuiwazia Yanga SC 24/7 na Kucheza Mechi zao Kifitna ili Wafungwe au Watoke Sare tuweze Kuwakaribia bali tujitathmini wapi tumekosea kwa Msimu huu, tujisahahiihishe na tucheze Mechi zetu Kimkakati na tusiruhusu tena Kufungwa au hata kutoka Sare Mechi nyinginezo kuanzia sasa.

HITIMISHO

Wana Simba SC tukubali tu kuwa Kutesa ni kwa zamu na Watani zetu Yanga SC kwa Msimu huu wapo vyema na walijipanga vvema Kimkakati ( hasa Ndani na Nje ) ya Uwanja.

Viongozi wa Simba SC amkeni haraka!!

Cc: Daudi Mchambuzi

Tatizo la Simba hawana washambuliaji Hilo ndio kweli. Sio kocha.
 
Huchoki tu Kunishobokea GENTAMYCINE kila mara na kuzidi Kuniongezea Umaarufu ( Fame ) wakati umeshasema hunipendi na mpaka kuniita Mwehu?

Je, kwa Wewe kuendelea Kujibizana nami uliyenita Mwehu na Kuonyesha kutonikubali ( Kunipenda ) unadhani aliye Mgonjwa wa Akili hasa ni nani?

Kumbe ninapowadharau na Kuwajibuni hovyo huwa sikosei / siwakosei.
Dunian Kote lazima mlemavu wa akili hasa ambao wapo kwenye profound stage kama ww lazima wazodolewe
 
Back
Top Bottom