Upuuzi mwingine wa Serikali legelege (An invitation to save BAHI swamp area) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upuuzi mwingine wa Serikali legelege (An invitation to save BAHI swamp area)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by socrates jr, Aug 19, 2011.

 1. socrates jr

  socrates jr Member

  #1
  Aug 19, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5

  Tangu zamani nilisikia wakisema Tanzania ni kichwa cha mwenda wazimu, lakini pengine sikuelewa maana hata mama alipo niambia kua-uyaone mwanangu nilifikili niyaone maghorofa kumbe alimaanisha niaone mambo yanayo kera na kuchefua kama yanayofanywa serikali ya huyu Mheshimiwa wa chama cha zamani. Ni ni takribani mwezi mmoja sasa umepita tangu ufanyike uzinduzi wa ripoti ya utafiti kuhusu uchimbaji wa madini ya Yurani (uranium) uliondaliwa wanaharakati wasio wakiserikali kutoka shirika la CESOPE. Utafiti huu uliongozwa na doktaDamas K Mbogoro kutoka idara ya uchumi chuo kikuuu Dodoma. Mbali na mambo mengine mengi yaliyo jadiliwa na washiriki wakiwemo Mh. Tundu Lisu na wengine kibao, jambo lililonisikitisha zaidi ni kile kilicho fafa nuliwa/ kufichuliwa na ripoti yenyewe. Hapa nakuleteeni sehemu moja wapo ya aya muhimu ktk ripoti hiyo: Evidence suggests that Uranium exist over the whole of Bahi district and 5 wards of Manyoni district. The Tanzanian govt appears ready to permit international companies to explore this area for Uranium. The net benefit to Tanzania for the three planned mining projects is estimated to be approximately TS 25,700,000,000/= (US$ 17,500,000) per annum-about 9% of the current market value of the local produce. Hiyo amount iliyo tajwa hapo juu ndicho tutakacho kipata (kama kweli kitapatikana) jaribu kukilinganisha na TSHs 278,909,197,400/= ambazo zinakisiwa kupatika kwa mwaka jana peke yake huku kukiwa na ongezeko la tija (productivity) zaidi ya asilimia 10 takribani kwa kila shughuli kuu ya kiuchumi inayo fanywa na watu wa Bahi (ongezeko hili la tija ni kwa kipindi cha 2006/2010). Bila shaka kwa takwimu ka hizi ni mtu mwenye upungufu wa timamu kichwani pekee ambaye atakuwa tayari kukubali biashara ya aina hii, ama sivyo, sisi ni mazuzu kama mwalimu alivyosema “tunabadilishana almasi kwa vipande vya chupa ” Labda tuachane mambo ya takwimu maana hesabu ni janga la kitaifa kwa walio wengi, je tunaufahamu wakutosha kususu madhara yanayoweza kuletwa na shughuli za uchimbaji wa Yurani? Vipi kuhusu mvurugano ktk mfumo wa mzima wa kiikolojia utaotokea baada ya uchimbaji kuanza ikizingatiwa kuwa Bahi ni eneo owevu? Mradi kama huu kwa sasa unatekelezwa ktk mbuga ya Selous pamoja namto Mkuju huko kusini. Huko Selous baadhi ya wana vijiji waliamishwa na serikali kwa nguvu kwa madai ya kupisha shughuli za uhifadhi wa mbuga (baadhi ya vijiji vilivyo athirika ni pamoja na Mchomero, Kiromesera, Songambele na Kitundu) sina taari juu ulipwaji wa fidia kwa wakazi wa vijiji hivyo kama ninyi mnayo tafadhali nifahamisheni. Chakushangaza zaidi haikupita hata mwaka mmoja eneo hilo lilikabidhiwa kwa kwa kampuni ya MANTRA resourses Ltd kwaminajili ya kuendeleza shughuli za utafiti na uchimbaji wa Yurani. MANTRA baadae iliuza hisa zake kwa kampuni la warusi kwasababu yenyewe (MANTRA) haikuwa na uzoefu wa kutosha ktk shughuli hizo za uchimbaji. Pengine tulifikiri Selous wanaishi “ngedele” pekeyao ndiyo maana tukapuuzia, la hasha:wala si hivyo, wako pia ndugu zetu wanaishi pande hizo. Sikusikia ngedele wala pimbi wakilalamikia shughuli hizo za MANTRA lakini WWF na mashirika mengine yanayotetea mazingira yaliilalamikia na kuionya serikali juu ya uamuzi wake huo usio na tija sio kwa wanyama na mimea tu bali pia hata kwa maisha ya wanadamu. Lakini kama kawaida sikio la kufa halisikii dawa, serikali iliamua kubana pua na kuuchapa usingizi chooni. Jamani tuamke, tusiruhusu yaliyotokea Selous, Nyamongo, Geita na kwingineko kuendelea kutokea, tutalaumiwa na kizazi kijacho achiliambali kupata laana ya “kizazi hata cha saba” . Let us join our hearts, share our understanding and develop a common goal for the betterment of our current and future generation. Let us fight and free Tanzania from this grief. SAVE BAHI SAVE TANZANIA.
   
 2. m

  mwelimishaji Member

  #2
  Aug 19, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakushukuru kwa taarifa hii.
  Sasa ni wakati wa kuamka na kusema kama JKNyerere: Tumenyonywa Kiasi cha kutosha, Tumenyanyaswa kiasi cha kutosha, Tumepuuzwa kiasi cha kutosha, NA SASA TUNATAKA MAPINDUZI ....SIO CHAMA CHA MAPINDUZI.
  Ubeberu huu utatumaliza kama hatutajikomboa wenyewe. We need to FIGHT for our RIGHTS, and if we have to DIE, let us DIE but not like HOGS.
  Jamani imekuwa kama vile nchi yetu haina UHURU huku tunasherehekea miaka 50 ya Uhuru. TUKO HURU KWELI?
   
 3. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Tuamke. Mimi nimeanza. Wiki hii nimekuwa na bahati sana ya kupata mtoto. Mtoto wangu aliponyonya maziwa kwa mara ya kwanza nilimwambia kama hutaupinga ufisadi maziwa haya na yakupalie. Naamini mwananangu atafanya ukombozi, kwani kizazi changu kimelala.
   
 4. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Ni kuchukua hatua sasa
   
 5. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Nyumbani kwangu Bahi, ule mchele wake ulivyokuwa mtamu (special Super), wale kambale pale watu ndo huwa wanashiba kipindi cha njaa. Leo ndugu zangu mnataka kukimbizwa mkawe wakimbizi, bora basi kuwe na cha maana mi naona kama kuna dili tu hapo. Subirini nyie tupate akili vizuri ndo tuchimbe wenyewe kwani yanaoza hayo afteral hata hela zikiingia mtazifisadi tu, tulieni msiwasumbue watu wetu. Yani papara tu, hebu tulizeni hivyo vitenesi vyenu.
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ulegelege utaisha tu pindi vijana tutakapofanya mapinduzi ambayo yataing'oa CCM madarakani
   
Loading...