Upuuzi huu wa Wanasimba wenzangu na baadhi ya Waandishi wa Habari za Michezo siwezi Kuuvumilia na leo nawatoleeni Uvivu.....!

Ninapoelekea nitaacha kuwa Mshabiki wa Simba SC na nitabakia tu na Timu yangu ya Liverpool FC kwani kama kuna Mashabiki wa mpira wa Tanzania wanaoudhi, wanaokera, wanaoboa na pengine nahisi wanaweza wakawa ama ni Wageni wa Mpira au wana Matatizo ya Akili basi ni wa Simba Sports Club.

Huwa siwezi Kuvumilia Ujinga / Ungumbaru na Upopoma / Upumbavu na leo nawatoleeni Uvivu Mashabiki wa Simba SC na wala Waandishi wa Habari za Michezo nchini Tanzania kwa kinachoendelea. Leo hata mkinichukia sijali ila ' dozi ' nawapeni.

Hivi Simba SC ni nani asitoke Sare au asifungwe? Hivi Simba SC ina hatimiliki ya Ushindi katika Ligi ya Tanzania? Kwahiyo Timu ya Ndanda FC haina haki ya ama Kuifunga au Kutoka Sare na Simba SC? Kwanini mnataka Kuzidharau Timu zingine 19 zilizopo katika Ligi ya Tanzania?

Eti leo mnadai kuwa Simba SC haijashinda kwakuwa Kocha ' Mnafiki ' mwenzenu Masoud Irambona Djuma hakwenda. Hivi ni mara ngapi Simba SC hii hii yetu ilifungwa mbele ya ' Mnafiki ' wenu Dhjuma akiwa na Timu? Leo nina hasira kweli nanyi na ' mtanikoma ' wallah!

Mnakuja na Hoja za Kipuuzi kabisa kwamba eti Simba SC imesajili ' Kitajiri ' hivyo haitakiwi kutoka Sare au Kufungwa. Hivi kuna Timu Tajiri na zinasajili Kitajiri duniani kama Real Madrid na Barcelona? Hivi huwa hazifungwi tena goli nyingi tu?

Jitu lingine linakuja na hoja kwamba kwanini Simba SC ilicheza na akina Okwi, Kagere na Bocco ndani lakini ilitoka sare juzi na Ndanda FC? Hivi Barcelona FC haikuwahi kucheza katika mechi zake za ligi huko Hispania ikiwa na Utatu kamili na takatifu wa akina Messi, Suarez na Neymar na bado wakafungwa?

Hebu jifunzeni mpira na mnatia aibu yaani kila Siku mnakimbilia Vibanda Umiza kukodolea mipira ya Ulaya lakini bado hamjifunzi tu mpira na mnakuja na hoja za Kitoto kabisa ambazo kwa Karne hii hazitakiwi. Hivi juzi Simba SC ingefungwa leo hii ingekuwaje? Wapuuzi wakubwa nyie!

Kuna Siku nilikuja na Uzi hapa hapa kuwa Simba SC kama itaendelea kubaki na huyu Kocha wenu Msaidizi ' Mnafiki ' Masoud Djuma haitoweza kufanya vyema lakini hamkunielewa na nilishawaambieni kuwa kuna Siku mtakuja kunielewa GENTAMYCINE na sasa yale yale ambayo niliyasema kuhusu Yeye yanaanza kutimia na kama akiendelea kubaki hapo mtakuja kuyaona makubwa.

Hivi nyie hamjiulizi swali kwamba kwanini kila Kocha mpya kutoka nje anayekuja Simba SC lazima tu atakuwa haendani na ' Mnafiki ' wenu Djuma? Anzeni kwa Omog, njooni kwa Lechantre na sasa huyu Aussems. Hivi ina maana hawa Makocha wote wana ' Chuki ' binafsi na Masoud Djuma?

Leo mmenitibua sana nyie Wanasimba! Na naomba sana mwaka huu tusiwe Mabingwa ili sasa ' tuchapane ' vizuri kwani hatutaki Kuheshimu Kanuni za mpira ambapo ni lazima umheshimu Mpinzani wako. Kwanza mnatakiwa muwaombe radhi Ndanda FC kwa kudhani kwamba wao wapo Ligi Kuu ili tu Kufungwa na Simba SC na siyo Kuonyesha Upinzani.

Na kama Waandishi wa Habari na Watangazi wa Habari za Michezo nchini Tanzania nanyi mna akili fupi na za hovyo hovyo kama za baadhi ya Wanasimba basi naweza kuanza ' Kuwadharau ' na kuwawekeni katika Kundi la Watu ' wasiojitambua ' na pengine bado mnatakiwa mkajifunze vizuri mambo ya mpira.

Sijawahi Kuchukizwa na Kuchukia kama leo.

Nawasilisha.
Bora umewaambia mkuu
 
Kwani usipoishabikia sima we ni nani? So afadhali ujiondokee zako utupunguzie mikosi!
 
Mtoa mada uko sahihi kabisa...ningekuwa bosi wa Simba, huyo Kocha msaidizi ningeshamfungishia virago,mbona alipigwa 2 kwa 0 na Gor-mahia washabiki walikaa kimya, wakt huo walimsema sana kocha mkuu aliyeiwezesha simba hadi ikafika fainali ya Sportpesa....huyu kocha msaidizi wasipomuangalia atukuwa na nguvu kuliko wenye timu yao.
 
nyie mikia wote mnafanana tu akili zenu! na leo mmekiona cha mtema kuni, ndo maana mmeangukiwa na mbao. na bado!
 
umeongea ukweli bro simba wanazingua hasa ukifuatilia magezeti unaweza kufikir wana kiwango cha juu kuliko hata timu ya msuva
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom