Upuuzi huu wa Wanasimba wenzangu na baadhi ya Waandishi wa Habari za Michezo siwezi Kuuvumilia na leo nawatoleeni Uvivu.....!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,382
2,000
Ninapoelekea nitaacha kuwa Mshabiki wa Simba SC na nitabakia tu na Timu yangu ya Liverpool FC kwani kama kuna Mashabiki wa mpira wa Tanzania wanaoudhi, wanaokera, wanaoboa na pengine nahisi wanaweza wakawa ama ni Wageni wa Mpira au wana Matatizo ya Akili basi ni wa Simba Sports Club.

Huwa siwezi Kuvumilia Ujinga / Ungumbaru na Upopoma / Upumbavu na leo nawatoleeni Uvivu Mashabiki wa Simba SC na wala Waandishi wa Habari za Michezo nchini Tanzania kwa kinachoendelea. Leo hata mkinichukia sijali ila ' dozi ' nawapeni.

Hivi Simba SC ni nani asitoke Sare au asifungwe? Hivi Simba SC ina hatimiliki ya Ushindi katika Ligi ya Tanzania? Kwahiyo Timu ya Ndanda FC haina haki ya ama Kuifunga au Kutoka Sare na Simba SC? Kwanini mnataka Kuzidharau Timu zingine 19 zilizopo katika Ligi ya Tanzania?

Eti leo mnadai kuwa Simba SC haijashinda kwakuwa Kocha ' Mnafiki ' mwenzenu Masoud Irambona Djuma hakwenda. Hivi ni mara ngapi Simba SC hii hii yetu ilifungwa mbele ya ' Mnafiki ' wenu Dhjuma akiwa na Timu? Leo nina hasira kweli nanyi na ' mtanikoma ' wallah!

Mnakuja na Hoja za Kipuuzi kabisa kwamba eti Simba SC imesajili ' Kitajiri ' hivyo haitakiwi kutoka Sare au Kufungwa. Hivi kuna Timu Tajiri na zinasajili Kitajiri duniani kama Real Madrid na Barcelona? Hivi huwa hazifungwi tena goli nyingi tu?

Jitu lingine linakuja na hoja kwamba kwanini Simba SC ilicheza na akina Okwi, Kagere na Bocco ndani lakini ilitoka sare juzi na Ndanda FC? Hivi Barcelona FC haikuwahi kucheza katika mechi zake za ligi huko Hispania ikiwa na Utatu kamili na takatifu wa akina Messi, Suarez na Neymar na bado wakafungwa?

Hebu jifunzeni mpira na mnatia aibu yaani kila Siku mnakimbilia Vibanda Umiza kukodolea mipira ya Ulaya lakini bado hamjifunzi tu mpira na mnakuja na hoja za Kitoto kabisa ambazo kwa Karne hii hazitakiwi. Hivi juzi Simba SC ingefungwa leo hii ingekuwaje? Wapuuzi wakubwa nyie!

Kuna Siku nilikuja na Uzi hapa hapa kuwa Simba SC kama itaendelea kubaki na huyu Kocha wenu Msaidizi ' Mnafiki ' Masoud Djuma haitoweza kufanya vyema lakini hamkunielewa na nilishawaambieni kuwa kuna Siku mtakuja kunielewa GENTAMYCINE na sasa yale yale ambayo niliyasema kuhusu Yeye yanaanza kutimia na kama akiendelea kubaki hapo mtakuja kuyaona makubwa.

Hivi nyie hamjiulizi swali kwamba kwanini kila Kocha mpya kutoka nje anayekuja Simba SC lazima tu atakuwa haendani na ' Mnafiki ' wenu Djuma? Anzeni kwa Omog, njooni kwa Lechantre na sasa huyu Aussems. Hivi ina maana hawa Makocha wote wana ' Chuki ' binafsi na Masoud Djuma?

Leo mmenitibua sana nyie Wanasimba! Na naomba sana mwaka huu tusiwe Mabingwa ili sasa ' tuchapane ' vizuri kwani hatutaki Kuheshimu Kanuni za mpira ambapo ni lazima umheshimu Mpinzani wako. Kwanza mnatakiwa muwaombe radhi Ndanda FC kwa kudhani kwamba wao wapo Ligi Kuu ili tu Kufungwa na Simba SC na siyo Kuonyesha Upinzani.

Na kama Waandishi wa Habari na Watangazi wa Habari za Michezo nchini Tanzania nanyi mna akili fupi na za hovyo hovyo kama za baadhi ya Wanasimba basi naweza kuanza ' Kuwadharau ' na kuwawekeni katika Kundi la Watu ' wasiojitambua ' na pengine bado mnatakiwa mkajifunze vizuri mambo ya mpira.

Sijawahi Kuchukizwa na Kuchukia kama leo.

Nawasilisha.
 

Gwele

JF-Expert Member
Jun 7, 2016
1,206
2,000
Mashabiki wetu wengi huwa siwaelewi kwakweli huyu bwana Masoud Djuma wanampa kichwa kana kwamba bila yeye timu haipati matokeo wakati mara kadhaa ameongoza hii timu akikaimu nafasi ya kocha mkuu lakini alishndwa refer Mapinduzi Cup na Sportpesa NB.Timu zote duniani zimewahi kutoa sare na hata kufungwa pia
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,382
2,000
Sawa Hajji Tumekuelewa but all in all kushabikia Mpira wa bongo ni kutumia mda wako vibaya

Aliyekuambia Mimi ni Haji Manara Msemaji wa Simba SC nani? Hivi Haji Manara ni Mshabiki wa Liverpool FC au ni wa Manchester United? Halafu ni kwanini huwa mnapenda sana Kunifananisha GENTAMYCINE na Watu wa Kada mbalimbali hapa nchini ambao hata sihusiano nao kwa lolote?
 

monopoly inc

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
3,215
2,000
Aliyekuambia Mimi ni Haji Manara Msemaji wa Simba SC nani? Hivi Haji Manara ni Mshabiki wa Liverpool FC au ni wa Manchester United? Halafu ni kwanini huwa mnapenda sana Kunifananisha GENTAMYCINE na Watu wa Kada mbalimbali hapa nchini ambao hata sihusiano nao kwa lolote?
Alie sema wewe ni Hajji manara msemaji wa simba ni Nani?
 

monopoly inc

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
3,215
2,000
Uzuri ni kwamba tayari nimeshakuripoti kwa Moderators na naamini akina Paw , Invisible , JamiiForums , Moderator watanitendea haki yangu kama Member juu ya hii ' post ' yako. Mmekuwa na tabia Mimi nikiwajibu vibaya mnakimbilia kwa Moderators ili nipigwe BAN hivyo nami leo nafanya kama ambavyo nyie huwa mnafanya Kwangu na huenda sasa huu ukawa ndiyo ' Utamaduni ' wangu wa Kudumu kwa wale Members wote mnaopenda ' Kunichokoza ' na kuja na ' Agenda ' zenu dhidi yangu.

Tutafika tu!
sasa unalia lia nini katika post hiyo kwani inatatizo gani
 

monopoly inc

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
3,215
2,000
Rejea soma post yako # 2 uliyoiandika. Jaribu kupunguza ' Upopoma ' ulionao Kichwani mwako tafadhali sawa?
Unajifanya jeuri hebu soma ulivoanza ww kunitusi Mimi afu unakimbilia kusemelea ukianzisha vagi siku nyingine jaribu kulimaliza mwenyewe sio unaishia kulia lia
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,382
2,000
Kwani wapi ulipotukanwa acha kulia lia mwanaume mzma biti nyingiiii msuli sisimizi

Ni kweli hakuna mahala uliponitukana na nitawaachia Moderators waweze kunisaidia Kutafsi kama ' post ' yako # 15 ni Tusi au ni neno la Baraka.
 

monopoly inc

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
3,215
2,000
Nadhani nimeshamalizana na Wewe na sasa nangojea wale ambao umesema ' nawalilia ' na ' nimekusemea ' Kwao watende Haki. Nakuruhusu uendelee Kunitusi ila baada ya ' post ' hii sitojibizana nawe tena kwani tayari nimeshajua unachokitafuta Kwangu. Nimemaliza.
Namm siwez kuendelea kubishana na wewe jaribu kuwatishia wanyonge wenzio unaowatukana kila siku wanakuangalia tu, be careful sio kila mtu ni mnyonge Kama unavodhania
 

koboG

JF-Expert Member
Apr 3, 2016
1,224
2,000
Iache simba ichanje mbuga bn or iyo drug Gentamycine inakupa hallucination
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom