GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,518
- 108,793
Baba mmoja nchini Kenya amemshtaki mahakamani mwanae wa kiume akitaka asilimia 20 ya mshahara wa mtoto huyo ili kukidhi mahitaji yake ya kila mwezi na kudai kuwa aliuza mali zake nyingi ili kumsomesha lakini mtoto huyo hampi msaada.
Chanzo: ITV Tanzania
Hivi Wazazi wa Kiafrika mnapotaka Watoto zenu tuje Kuwalea 'Kilazima' kuna Mtu aliwalazimisheni mtuzae kwa Starehe zenu?
Hivi Wazazi wa Kiafrika ni nani aliwadanganya kuwa Kuzaa Watoto, Kuwakuza mpaka Kuwasomesha basi wao Kuwatunzeni ni lazima na siyo Hisani tu?
Hivi Wazazi wa Kiafrika kwani wakati mnatuzaa na bado mna Nguvu zenu na Mali nyingi pia mlishindwa Kuzipangilia vyema ili zije ziwatunzeni mkiwa Wazee na muache Kuwatafutia lawama Watoto zenu huku wengine mkifikia hata hatua za Kuwatishia Kuwalaani japo wapo pia ambao mnawalaani Kweli?
Kuna Mzazi Mmoja aliwahi kusema Yeye hata kama amejinyima ili Kusomesha Watoto zake na Wamefanikiwa Kimaisha ila hatopenda alazimishe Fadhila zao kwani Kuwazaa na Kuwakuza ni Jukumu lake na Yeye Furaha yake ni Kuwaona hao Wanae wakizilea pia Familia zao na Kusaidia na Watu wengine pia kwakuwa kuna Watu hapa duniani wana Shida kuliko hata Yeye Baba yao.
Mzazi muda wote ukiwa na Kazi yako Wewe Kutwa tu ni Kuzunguka na 'Mimalaya' hapa Mjini, Kuzaa hovyo, Kuhonga sana huku ukifululiza kwenda kwa Waganga wa Kienyeji ambako wamekulia mno Pesa zako halafu umekuwa Mzee na Maisha yamekuendea 'alijojo' unaanza kutaka kutupa Lawama kwa Wanao kuwa hawakutunzi wakati huenda hao hao Wanao walikushauri sana ubadilike na utunze Pesa zako ukawa Unawadharau.
Wazazi wa Kiafrika mna matatizo sana.