Upuuzi huu usiovumilika na uliovuka Kiwango unapatikana katika Soka la Tanzania tu duniani kote

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Kaimu Kocha wa Simba SC Selemani Matola mara baada ya Michuano ya Mapinduzi Cup alipohojiwa na Press alisema kuwa amewapa Wachezaji likizo mpaka Ijumaa ya Wiki hii (22 January 2021) kisha watarejea Mazoezini upesi sana ili kujiandaa kikamilifu kabisa na Michezo Klabu Bingwa ambayo inaanza mapema tu Mwezi February.

Cha Kushangaza Kaimu Kocha huyo huyo Matola akijua Simba SC haina Kocha yoyote juzi ameenda Kuungana na Timu ya Taifa (Taifa Stars) na kuiacha Simba SC bila Kocha. Sasa naanza Kumuelewa Rais JPM pamoja na Wadau wengine wa Soka nchini Tanzania kuwa Timu mbili hizi Kongwe na Kubwa nchini Tanzania zimejaa Uhuni, Usanii na Upuuzi huku zikituchelewesha Kimaendeleo.

Hivi ni lazima tu Kocha Matola aende huko Cameroon? Kwani hakuna Makocha wengine? Hizi 10% za TFF na huu Usimba na Uyanga utatugharimu.
 
ha ha nacheka tu. mleta umetoa povu kama nini. sijui ni utopolo unakusumbua. Kocha wa AS VITA yupo huko na wanashiriki club bingwa. kujifanya tunajua kila kitu wakati ni zero.
Hamjamwelewa jamaa. Point yake ni kwamba Simba haina kocha mkuu hivyo kuondoka kwa Matola maanake kaiacha Simba ikiendesha programu za mazoezi pasipokuwepo kwa kocha iwe mkuu ama msaidizi. Hao Mazembe na As Vita, timu zimebakia na makocha wasaidizi
 
Hivi kati ya Simba na Taifa stars nini kinatakiwa kitangulie? Taifa likimchagua kocha kutoka Simba anatakiwa akatae aseme siwezi kuja sababu niko mwenyewe kwenye timu yangu sasa hivi? Au TFF kabla ya kumchagua inatakiwa iangalie mazingira yake hata kama wanaamini ni mzuri na ni msaada kwa Taifa?

Nauliza tu
 
Eti kwa Simba hii iwapige Al ahal?nimempenda Sven jumba bovu lisimwangukie, na bado mtateseka tu
 
Hamjamwelewa jamaa. Point yake ni kwamba Simba haina kocha mkuu hivyo kuondoka kwa Matola maanake kaiacha Simba ikiendesha programu za mazoezi pasipokuwepo kwa kocha iwe mkuu ama msaidizi. Hao Mazembe na As Vita, timu zimebakia na makocha wasaidizi
Sasa program gani za mazoezi na ameandika mwenyewe timu ipo likizo mpk trh 22 Mm yanga sio simba lkn Sometime wabongo tuache ujuaji sana.

Ndo mana wazee km kilomoni na yule babu wa marehemu wa yanga AKILIMARI walikuwa wanaharibu soka la hivi vilabu
Yaan timu yenye mamilioni ya mashabiki unataka iende unavyotaka wewe mtu 1.

Sasa Matola anaweza kwenda huko bira ruhusa ya uongozi wa juu? Vitu vingine muwe mnafikiliaga kwanza kabla ya kuandika
Hii inawaponza hata mashabiki wengne wa SIMBA waonekane vilaza

Nyie NYAU FC vipi banaaaa
 
Hamjamwelewa jamaa. Point yake ni kwamba Simba haina kocha mkuu hivyo kuondoka kwa Matola maanake kaiacha Simba ikiendesha programu za mazoezi pasipokuwepo kwa kocha iwe mkuu ama msaidizi. Hao Mazembe na As Vita, timu zimebakia na makocha wasaidizi
Ye mwenyewe kasema wachezaji wamepewa likizo kwa hiyo wako mapumziko. kama mpaka ijumaa ataona team wanafanya mazoezi wenyewe ndio angeleta huu Uzi. Viongozi wanatoa mamilioni kuendesha team sidhani wanaweza kuwa wazembe hivyo.
 
Hamjamwelewa jamaa. Point yake ni kwamba Simba haina kocha mkuu hivyo kuondoka kwa Matola maanake kaiacha Simba ikiendesha programu za mazoezi pasipokuwepo kwa kocha iwe mkuu ama msaidizi. Hao Mazembe na As Vita, timu zimebakia na makocha wasaidizi
wachezaji wako likizo hadi tarehe 22, kocha takuwa keshakuja shida nini? nadhani uongozi ni wajinga?hata huko alipo matola kuna wachezaji 6 wa simba
 
Ulichotakiwa kufahamu ni kwamba Matola ni kocha msaidizi wa Timu ya Taifa.

Alikuwa Zanzibar kwa ruhusa maalum kwenda kuisaidia Simba kwenye kombe la Mapinduzi baada ya kocha mkuu kusepa gafla.

Simba ina mapumziko hadi tar 22. Ungesubiri hadi tarehe hiyo ndio uporomoshe povu, labda ijumaa na yeye Matola atakuwa anarudi toka Cameroon
 
ha ha nacheka tu. mleta umetoa povu kama nini. sijui ni utopolo unakusumbua. Kocha wa AS VITA yupo huko na wanashiriki club bingwa. kujifanya tunajua kila kitu wakati ni zero.
Halafu akikosolewa anatukana, utopolo wana shida sana.
 
Mbona kocha wa Mazembe na Vita(Club Kubwa Congo) ndio makocha wa Timu ya Taifa Congo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umemuuliza swali zuri, na mbona wachezaji wa hizo club wameenda timu za taifa. Tatizo la watanzania ni kujifanya wachambuzi kwa mambo ambayo hawana ujuzi nayo. Utakuta mtu anachambua mpira oooh na bla bla kibao ila ukimpa timu aifundishe au yeye acheze ni zeroo.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom