Upuuzaji wa mambo muhimu na ujinga ni chanzo cha matatizo

contask

JF-Expert Member
Jan 3, 2021
800
1,640

Upuuzi na ujinga ni chanzo cha matatizo​


Habari wakuu,

Tuende moja kwa moja kwenye kichwa cha uzi kwamba ujinga ni chanzo cha matatizo. Watu wengi katika jamii zetu tumekua ni watu wa kupuuzia mambo madogo madogo ambayo mwishowe yanakuja kutugharimu katika maisha yetu binafsi pia familia na jamii kwa ujumla na wengi wetu tukafanya mambo hayo aidha kwa kua na uelewa mdogo wa athari wa mambo hayo au kufanya kwa kupuuzia kwa kuamini kwamba hayawezi kutuletea athari katika maisha yetu.

Leo nitazungumzia baadhi ya sababu ndogo ndogo ambazo tunanidharau zinapelekea kwenda jela au kuingia katika matatizo makubwa ambayo yanaweza kuathiri mfumo mzima wa maisha yako kijamii lakini pia kiuchumi,mfano wa sababu hizo ni kama zifuatazo

📌kununua simu used
Hapa namaanisha kununua zile simu za mkononi almaarufu kama simu za mtumba.

Mwaka huu mnamo mwezi wa 3 nilienda polisi kwa kosa la kuhisiwa kwa kununua simu ya wizi,ambapo mtu ambae alifungua kesi hiyo alidai kua aliibiwa simu ya samsung note 10 plus na iphone 12 pro max.Lakini mwishowe mungu ni mwema maana simu aliifananisha haikua iyo ambayo anihisi ilikua yake kwa maana kwamba nilifanikiwa kunusurika kuingia kwenye mtego wa kulipa samsung note 10 plus yenye gharama ya 450000 na iphone 12 pro max yenye gharama ya 1500000 ambao mwishowe ungeniathiri kiuchumi lakini pia kijamii kwa kupunguza uaminifu kwa watu wa karibu
Pia mwaka huu mwezi wa 3 kuna mtu amehukumiwa kifungo cha miaka 30 ambacho kilisababishwa na kununua simu ya wizi kwa mtu ambae hafahamiani nae.

📌kumuazima simu mtu ambae humfahamu
Kwatu wa rika moja mukikutana hasa vijana pale tunapokutana vijiweni kupiga soga bila hata ya kufahamia ,kuna ile tabia mtu anauliza kama unadakika umuazime simu kuna mtu anataka kumpigia bila kujua anaongea na nani na anaongea nini unampatia simu yako mwishowe anafanya mawasiliano ya kiuhalifu ,hali ambayo inapelekea kipindi cha upelelezi we unaweza kuchukuliwa na kuhisiwa ndie muhusika mkuu wa tukio la uhalifu kama vile mauaji ambayo kesi yake ni kubwa na unaweza ukasota kipindi kirefu mahabusu bila mafanikio na kupelekea kuanguka kwa shughuri za kiuchumi na ukienda mbali zaidi unaweza kuozea jela

📌kuazima simu ya mtu ambaye humfahamu
Hii mara kwa mara hutokea unapoazima simu ya mtu ambae humfahamu na kuweka line yako kwa nia ya kukamilisha mawasiliano pindi simu yako imekumbwa na changamoto kama vile chaji au hitirafu ya mfumo. Kitendo cha kuweka line kwenye simu ya mtu ambae humfahamu ni kitendo hatari ambacho kinaweza kuingia kwenye mkumbo wa wahalifu kama kifaa hicho kilifanya tukio au kama ni cha wizi hasa hasa hizi simu epuka kuweka line kwwnye simu za wtu pia hata kama unawafahamu jitahidi kujizui

📌kukaa kwenye vijiwe ambavyo havieleweki
Haoa namaa nisha vijiwe vya walevi na wavutaji kwa maana vijiwe hivi ni washukiwa wa tukio moja kwa moja pindi litakapotokea tukio la kiuhalifu pia baadhi ya vijiwe ni vichaka vya wahalifu
ongezea mengine mkuu kwa faida ya wana jf🙏
 
Back
Top Bottom