Upotoshwaji wa taarifa kuhusu wanafunzi watanzania wa shahada ya uzamili nchini Algeria

wanafunzi wahanga

New Member
Feb 20, 2016
3
1
Barua ya wazi kwa mheshimiwa waziri, wizara ya elimu, sayansi, ufundi na teknolojia

YAH: UPOTOSHWAJI WA TAARIFA KUHUSU WANAFUNZI WATANZANIA WA SHAHADA YA UZAMILI NCHINI ALGERIA
Tafadhali rejea kichwa cha barua hapo juu. Sisi wanafunzi watanzania wa shahada ya uzamili nchini Algeria tumehuzunishwa na upotoshaji wa taarifa zetu na watendaji wa wizara ya elimu akiwemo mkurugenzi wa elimu ya juu. Pamoja na uwepo wa mheshimiwa Johari Chikira kutoka bodi ya mikopo hapa nchini Algeria, tumeonelea tuandike barua hii kutokana na taarifa yako kwa vyombo vya habari ya mnamo tarehe 16 ya mwezi februari mwaka huu.

Mnamo mwaka 2012 tuliwafahamisha wizara juu ya mabadiliko ya mfumo wa elimu nchini Algeria, kutoka mfumo uitwao «Classique» ambao shahada ya kwanza inasomwa kwa miaka mine kwenda mfumo mpya maarufu kwa jina la «LMD» huku «L» ikimaanisha «Licence» au shahada ya kwanza, «M» ikimaanisha «Master» au shahada ya uzamili na «D» ikimaanisha «Doctorat» au shahada ya uzamivu. Mfumo huu mpya umeondoa ulazima wa mwanafunzi kuwa na uzoefu wa kazi katika kuendelea na shahada za uzamili na uzamivu na umeweka msisitizo wa mwanafunzi kufika japo shahada ya uzamili. Chini ya haya mabadiliko ya mfumo wa elimu, wanafunzi wa kigeni (Wasio waalgeria) tumepewa ruhusa ya kuendelea na shahada za uzamili na uzamivu tofauti na mfumo wa awali (Classique) ambapo wanafunzi wa kigeni hatukuwa na ruhusa hiyo. Pamoja na wizara kuwa na taarifa hizo, haikuzifanyia kazi wala kutupa taarifa yeyote. Maafisa kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB) na wizara ya elimu akiwemo katibu mkuu aliyepita, walielezwa juu ya suala hilo walipotembelea nchini Algeria na walisema watalishughulikia lakini kwa masikitiko makubwa hawakutoa taarifa yeyote walipofika nyumbani Tanzania.

Pia mnamo mwezi disemba mwaka 2015 na mwezi januari mwaka huu tumetuma barua zaidi ya moja kwenda wizara ya elimu kuelezea suala hili na tunahofia kwamba barua hizo zote hazijakufikia.

Tunaomba ufahamu kwamba kitendo cha maafisa wa wizara ya elimu kuelezea suala hili kama jipya na wasilo na taarifa nalo si cha ukweli na inatuhuzunisha sana kuona maofisa hao ambao tunawategemea kama walezi wetu wakubwa wamefikia hatua ya kupindisha ukweli.

Haya ni matokeo ya wizara kupitia watendaji wake muhimu akiwemo mkurugenzi wa elimu ya juu kujiweka mbali na matatizo yanayowakabili wanafunzi watanzania nchini Algeria.

Tunaomba ufahamu kwamba maafisa wa wizara ya elimu wamekuwa na tabia ya kupuuza taarifa tunazowatumia hata ziwe na umuhimu mkubwa na pia imekuwa kwamba wanafunzi tukishafika hapa nchini Algeria basi tunakuwa kama tumetelekezwa. Mfano mkubwa wa haya ni suala hili la shahada ya uzamili.

Mheshimiwa waziri, Tunakuomba uliangalie hili suala upya maana uamuzi wa kutunyima mkopo wa masomo kwa mwaka 2015/2016 utakuwa umeathiri maendeleo yetu kielimu kwa kiwango kikubwa kwani tulilazimika kuendelea na shahada ya uzamili kwa sababu ambazo ni za msingi na zipo nje ya uwezo wetu.

Mheshimiwa waziri, sisi wanafunzi tupo katika hali ngumu kimaisha na kisaikolojia maana tupo nchi ya ugenini na hatuna njia nyingine ya kujikimu zaidi ya mkopo tuliokuwa tukiutegemea ukizingatia kwamba sheria za Algeria haziruhusu mwanafunzi wa kigeni kufanya kazi yeyote na ukiukaji wa sheria hiyo unaweza kupelekea kifungo na baada ya hapo kurudishwa nyumbani.

Tunatumaini kwamba utalipatia ufumbuzi tatizo linalotukabili na kutupatia mwongozo maana tumekata tamaa kimaisha na hatujui nini cha kufanya.
 
Tafuteni namba ya waziri pia e-mail uake mumjulishe huku jf tutawapa pole tu. Na hyo nchi ukikiuka sheria waweza pigwa mawe had ufe....polen sana
 
Bonjour mes amis, tuna imani waziri atasikia na atafanyia kazi ila ninavyojua mimi ni kuwa mkataba wa mkopo ulikuwa ni wa degree ya kwanza tu na sio masters hivyo nyie kuruhusiwa huko haina maana ni lazima bodi iendelee kuwapa mkopo tu na pia mjue kuna wengine waliendelea kupata mkopo hata baada ya kumaliza na kurudi nyumbani kwa kisingizio hicho cha kuendelea na masters na ndio waziri lilimuudhi sana hivyo inaweza ikawa ngumu kwenu kidogo kwenye hili la mkopo. niwashauri nyie wote ambao mpo bado vyuoni mjiorodheshe na documents zenu zote ili wizara iwatambue kuwa bado mpo mnasoma na pia ni vyema mkitumia chance hii kueleza matatizo yenu yote na sio mkopo tu. Hata ubalozi pia ni vyema mkigusia kama mnaona kuna umuhimu ninavyojua mimi mnatumia ubalozi wa Tanzania ufaransa ambapo ni mbali kidogo.

All the best, c'est votre ami Malcolm05.
 
Tulilazimika kuendelea na masters kutakana na mabadiliko ya mfumo wa elimu ambao ulimgusa kila mwanafunzi wa elimu ya juu nchini Algeria. Tumetuma matokeo yetu tangu mwishoni mwa mwezi wa kumi mwaka jana. Tunaomba ifahamike kwamba tuliwapatia wizara taarifa na wakasema watalishughulikia. Kingine pamoja na kwamba mkopo wa wanafunzi wa masters ni tofauti na ule wa undergraduate na sisi tulitoa taarifa ili tuendelee kusoma kwa mkopo wa undergraduate.
Kwa mheshimiwa Saint Ivuga, elimu nchini Algeria inaendeshwa kwa lugha ya kifaransa na kila mwanafunzi anayetoka nchi isiyoongea kifaransa analazimika kusoma lugha kwa mwaka mzima baada ya hapo ni kozi ambayo kwa utaratibu huu mpya wa kuunganisha degree ya kwanza na masters inachukua miaka mitano.
 
Back
Top Bottom