Upotoshaji wa wanasiasa kuhusu demokrasia,uongozi na majukumu yao. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upotoshaji wa wanasiasa kuhusu demokrasia,uongozi na majukumu yao.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ndusty, Jan 1, 2012.

 1. N

  Ndusty JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Waheshimiwa(Great Thinkers) wasomaji na wapenzi wa hii blog ya JF,nawasalimu wote na kuwatakia heri na fanaka za mwaka mpya 2012.nikiamini kwamba MUNGU ataendelea kuwa nanyi kwa kuwabariki na kuwasaidia kila mmoja kwa kadiri mlivyo muomba.Pia napenda kuwashukuru waanzilishi wa hii blog(JF) popote walipo kwa kuweza kuwa na upeo wa kufikiria na kufikia maamuzi ya kuanzisha hii blog.sio kazi ndogo wala rahisi.kwa kupitia JF wananchi wengi wamefanikiwa kufikisha mawazo,maoni,maonyo na mengine mengi kwa watanzania(viongozi na wananchi).MUNGU azidi kuwabariki na kuwapa moyo wa ujasiri zaidi waanzilishi wa JF.Naomba sisi members tuendelee kutoa hoja na maoni ambayo kweli yanawakilisha maana halisi ya JF(great thinkers) sanasana kwenye hii forum ya jukwaa la siasa.tujue kabisa maoni,hoja au ujumbe tunaotoa au kuchangia unaimpact kubwa sana kwa wasomaji wengine na wananchi wa tanzania kwa ujumla.tunapoongelea masuala ya Raisi wetu,mawaziri,wabunge au viongozi wengine lazima tuwe tunatoa mada ambazo zinalenga kuwakilisha au kutetea maslahi ya watanzania wote kwa ujumla.tuwajudge viongozi wetu kwa kuangalia utendaji wao wa kazi na jinsi gani wameweza kusimamia,kutetea,kulinda na kuliletea maendelea Taifa na wanachi wa Tanzania kwa kupitia nafasi zao za uongozi.Tutoe hoja ambazo ni za kujenga na sio hoja ambazo zitatutenga kwa itikadi za vyama vya siasa,kabila au dini.tujadili mambo kwa itikadi ya UTANZANIA,penye ukweli basi tuwe wakweli na sio kudanganyana na kupotoshana kwa maslahi binafsi.Kiongozi yeyote mwenye makosa tumseme na kumkemea na mwenye kufanya vizuri tumpe sifa zake na kumzidishia moyo zaidi.tusipende kuweka issues ambazo ni personal.hazita tusaidia chochote sisi wasomaji na wananchi kwa ujumla.pia zinazidi kupoteza hadhi ya JF na wachangiaji wote wenye kutoa hoja za msingi.Mfano kusupport mada kuhusu labda, ruzuku za CHADEMA zinafanya kazi gani,au kuhusu mtoto wa malecela kutaka kugombea ubunge,au kwanini kafulila kafukuzwa NCCR,au kwanini Nape Nnauye kawa katibu mwenezi wa CCM,au kwanini CCM hawamfukuzi Lowassa na issues nyingine nyingi ambazo hazitujengi wala kutusaidia chochote kwenye kuleta maendeleo.
  Sasa Waheshimiwa naomba nirudi kwenye mada kuhusu hawa wanasiasa wetu na jinsi wanavyo tuchanganya akili zetu na kutufanya kama watoto.
  Tumeona na kusikia matatizo ya migongano,kudharauliana ,chuki ,vita na kupingana kimaneno zaidi kwa baadhi ya wanasiasa.wanasiasa ambao wanatoka chama kimoja na sio vyama tofauti.sasa naomba tujaribu kuangalia hii migongano ya viongozi wetu kwenye kila chama na pia tuangalie sababu zake.
  CCM: Migongano kati ya Mheshimiwa Raisi ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama na Mh.Lowassa.Pia kati ya Mh Lowassa na Mh Sitta na waheshimiwa wengine wengi tu.tukiangalia kiini haswa cha haya matatizo tutagundua kwamba ni suala la kuwania madaraka ( Uraisi).Nafasi ambayo itapatikana baada ya miaka minne ijayo tayari watu wameshaanza kupigana, kudanganya, kutishia amani ya nchi na kuwagawa viongozi na wananchi kwenye makundi.
  NCCR: Migongano kati ya Mh Mbatia(Mwenyekiti wa chama) na Kafulila(Mbunge).ukiangalia kiini cha hili tatizo pia ni kuwania madaraka.
  CUF: Migongano kati ya Mh Seif Sherrif(Makamo wa wa raisi na katibu mkuu wa chama) na Hamad Rashid(Mbunge).tatizo ni Mh Hamad kutoa maneno ya kashfa na shutuma kwa Mh Seif.Pia kutangaza nia yake ya kugombea ukatibu mkuu.Kiini cha tatizo ni madaraka.
  CHADEMA(Kipindi cha nyuma kidogo):Mh Mbowe(Mwenyekiti na Kiongozi wa upinzani bungeni) na Mh Zitto.Zitto kupingana mara nyingi na Mwenyekiti wake pia na chama chake kwenye maoni na misimamo yao.Mfano kwenye suala la ununuzi wa ile mitambo ya dowans nakadhalika.Mwisho Zitto kujaza fomu za kugombea uwenyekiti na baadae kujitoa.Kiini cha tatizo pia ni Madaraka.

  Wakuu kuna mifano mingi mnoo ya migogoro inayotokea kwenye vyama vyetu vya siasa na kama tukiangalia kwa makini pasipo ushabiki tutagundua kwamba ni tamaa ya madaraka.Viongozi wamekuwa wanaleta migogoro kwenye vyama vyao kwa kujali maslahi yao wenyewe na kutumia neno DEMOKRASIA kama kigezo.Wakuu,hawa viongozi walipata madaraka waliyonayo kwa ridhaa yetu wananchi na ridhaa ya vyama vyao vya siasa.pasipo hivyo vyama wasingeweza kuwepo hapo walipo sasahivi.kila chama kina kanuni,sheria na taratibu zake kwa wanachama wake.sheria hizi zinatofautiana kwenye kila chama.kwahiyo kila mwanachama ambaye ameamua kujiunga na chama fulani ni wajibu wake kufuata kanuni na taratibu za hicho chama.sidhani kama kuna chama ambacho kina sheria ambayo inakataza wanachama wake kukosoana au kuwa na mtazamo tofauti.ila naamini kila chama kina utaratibu wake kwa wanachama kuwakilisha mawazo,matatizo au maoni yao.Sidhani kama ni sahihi wananchi wengine kuingilia maamuzi ya vyama pale ambapo vinajaribu kutatua au kurekebisha vyama vyao kwa misingi ambayo walijiwekewa wenyewe.ni ukweli usiopingika kwamba sisi watanzania tunakasumba ya kuchagua mgombea wa nafasi fulani kwa kuangalia chama anachotokea.kwamfano mtu hawezi kugombea ubunge pasipo kupitia chama.sasa kama alikubali kujiunga na chama fulani lazima akubaliane na taratibu za hicho chama.hakuna taasisi au kikundi cha watu wenye kukubaliana kufuata njia moja halafu pasiwe na sheria.vyama vya siasa vingekuwa vinaendeshwa bila utaratibu,sheria na mipaka sidhani kama kungekuwa na chama ambacho kipo hai mpaka leo.DEMOKRASIA ni haki ya kila mwananchi lakini kuna mipaka yake kutokana na sehemu na taratibu ambazo kila chama,taasisi nakadhalika wamejiwekea.Kiongozi hawezi kuvunja utaratibu wa chama ambacho kimempa nafasi aliyonayo halafu akakimbilia kwa wananchi na kulalamika huku akutudanganya ni Demokrasia.sisi wananchi tuna uwezo wa kusema chochote kuhusu viongozi wetu kwa kutumia mwamvuli wa demokrasia kwasababu hatujafungwa na kanuni au sheria za chama chochote,lakini viongozi wetu wamefungwa na sheria za vyama vyao hivyo wajaribu kuheshimu hizo sheria na mipaka waliyokubaliana nayo wakati wanajiunga na hivyo vyama.
  Wakuu,ukiangalia kwenye CCM ni kwamba kila kiongozi shida yake ni kuwa raisi.badala ya kumsaidia Raisi aliyopo madarakani kwa sasa ili kwa pamoja watuletee maendelleo sisi wananchi,wao wanajaribu kumfanya ashindwe kuongoza kwa kwenda against nae.kwanini viongozi wetu wanaleta persona issues kwenye masuala ambayo yana affect watu zaidi ya milioni 40?sisi wananchi hatukuwachagua ili wakagombee uraisi,sisi tuliwachagua ili wakatusaidie kutatua matatizo yetu mengi ambayo yanatukabili wakishirikiana na Mh Raisi.
  Kafulila hakuchaguliwa na wananchi wa jimbo lake ili aende kukosoa uongozi wa chama chama.kungolewa kwa Mbatia au kiongozi mwingine yoyote hakutatatua matatizo mengi waliyonayo wananchi wa jimbo lake ambao ndio waliomchagua.kila siku baadhi ya viongozi kugombana na kupingana na viongozi wao(wenyeviti) kwa kujidai ni demokrasia hakuwasaidii au kuwaletea maendeleo wananchi.kwanini viongozi wamekuwa kwa makusudi wanasahau majukumu yao na badala yake wana changanya wananchi kwa kesi zisizokwisha ambazo hazina maslahi kwa wananchi isipokuwa kwa maslahi yao wenyewe.kesi au matatizo ya ruzuku au madaraka tunaomba muyamalizie hukohuko kwenye vyama vyenu na sio kuyatangaza kwa wananchi kwasababu hayana manufaa kwao.Hamad Rashid,Kafulila,Zitto au kiongozi mwingine yeyote ambaye anajaribu kutaka madaraka zaidi kwa kukashifu,kutukana au kuzozana na wakubwa zake kwa kigezo cha demokrasia pasipo kufuata kanuni,sheria,mipaka na utaratibu wa vyama vyao tunawaomba mjirekebishe tafadhali.msiwaonee wananchi kwasababu hawajui hizo sheria za vyama vyenu.msikimbilie magazetini ili kuchochea chuki kati ya viongozi wengine na sisi wananchi.Tumuogope MUNGU jamani.cheo ni dhamana jamani,na hamna mtu mwenye guarantee na maisha.Msiwe na roho za ubinafsi tafadhani.kuna mamilioni ya watanzania ambao wanawategemea kukomboa maisha yao.kazi zenu zisiwe ni kugombea madaraka na kuzozana kila siku.kumbukeni mlikotoka jamani na mumuogope MUNGU.
  Sijawahi kuona post hata moja hapa kwenye JF kutoka kwa viongozi wetu,wakiomba mchango wa members kusaidia kununua madawati,au kiujenga kisima,au kununua vitanda vya hospitalini au tatizo lolote,kila siku ni kuweka post za kusengenyana na kuzozona.tunapenda kuona mnakazana zaidi kutuma post za kusaidia wananchi wenu sio kukazana kulalamika tu.sidhani kwamba kiongozi lazima awe mwenyekiti au Raisi ili aweze kuwaletea wananchi maendeleo au kutatua matatizo yao.mnataka vyeo kwa ajili ya maslahi yenu wenyewe na familia zenu.Mbona hatuoni watu kama Dr Slaa au Ndesamburo,au viongozi wengine wengi walioko vyama vingine kwa muda mrefu wakigombana na wenyeviti wao?Ni kwasababu wanatambua wajibu wao.Tunaomba viongozi wote waliochaguliwa na wananchi wajaribu kutekeleza majukumu na ahadi walizowapa wananchi wao na sio kutafuta madaraka zaidi ili wajinufaishe wao zaidi.
  Mwisho napenda kuwashauri members wa JF hasahasa wanaofuatilia na kutoa maoni kwenye forum ya siasa tuwe makini sana.tusijifikirie sisi wenyewe.tufikirie pia na ndugu zetu wengine wengi ambao hawapati nafasi ya kutoa maoni kama sisi.ambao wanaishi gizani,hawana hata pesa ya kinunua mlo mmoja,hawajawahi kuona umeme maisha yao yote.tujaribu kuwakilisha maoni yenye kujumuisha watanzania wote na hali halisi.tusiwe wamimi kwa kujifikiria sisi tu.kuwa na access ya internet kusikufanye kuropoka mambo ambayo hayana msingi.tusichangie au kusupport au kutoa hoja zenye kuattack watu personal kwa chuki zisizo na faida kwetu.kuongelea kuhusu ruzuku ya chadema,au mtu fulani kugombea ubunge au issues nyingine ambazo hazina tija kwa taifa ni upumbavu.wenye issues kama hizo naomba waziweke kwenye forum ya udaku.
  Much blessings!
   
Loading...