kukumweupe
JF-Expert Member
- Apr 18, 2020
- 439
- 599
Wapotoshaji Horuba ya ofisi ya waziri mkuu bungeni kuhusu ajira hii hapa
Mheshimiwa Spika, mafanikio haya katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uboreshaji wa huduma za jamii yameenda sambamba na uzalishaji wa ajira zipatazo milioni 12.6 zikiwemo ajira za moja kwa moja milioni 11.7 kwenye sekta mbalimbali nchini.
Kwa mfano:
Sekta za Afya, Elimu na Utawala zimetoa ajira za kudumu kwa kuajiri watumishi 28,403 katika mamlaka za Serikali za Mitaa;
Mradi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa umewezesha kuzalishwa ajira zipatazo 13,177 za kitaalam na zisizo za kitalaam. Kati ya hizo, ajira za kitaalam kwa wazawa ni asilimia 46.5. Pia kupitia mradi huu kumekuwa na utoaji wa zabuni zenye thamani ya Shilingi bilioni 664.7 kwa wazabuni na wakandarasi wa ndani 640;
Mradi wa umeme wa mwalimu Nyerere kupitia maporomoko ya mto Rufiji umezalisha jumla ya ajira 3,897 ikiwemo ajira za wazawa 3,422;
Ufufuaji wa shirika la ndege la Tanzania (ATCL) pamoja na kuboresha viwanja vya ndege jumla ya ajira 2,970;
Ujenzi wa Viwanda nchini jumla ya ajira zilizozalishwa ni 41,900;
Ujenzi na uboreshaji wa miundombinu mbalimbali ikiwemo Hospitali za Wilaya, vituo vya afya, Zahanati, Madarasa, Nyumba na majengo maeneo mapya ya utawala, Miradi ya barabara chini ya TARURA kwa kutumia Force Account jumla ya mafundi 845,348 walipata ajira za mikataba na muda.