UKWELIYAKINIFU
Member
- Oct 6, 2020
- 27
- 50
Katika siasa za ushindani kama ilivyo ushindani holela wa soko huria kumeibuka upotoshwaji mkubwa wa kutumia fikra za Mwalimu Nyerere nyingi na hapa nitajikita katika dhana ya “UHURU”.
Kwa makusudi katika mchakato wa kuwa makuhadi wa soko huria, na pengine pia wapinzani kutokuwa na falsafa , inayoongoza itakidi na baadaye kutengeneza miongozo kama vile ilivyokuwa kwa Azimio la Arusha na sera. Wapinzani kwa kuendekeza tamaa binafsi za kulinganisha juhudi za sasa za kujikomboa kiuchumi wamekuwa wasaliti kwa kukosa uzalendo wa kulinda matakwa ya wanyonge ambao ndio kwa muda mrefu wamekuwa wahanga wa ukoloni mamboleo unajivika gwanda la “Uhuru” wa mawazo.
Upinzani huu umeendeleza propaganda ucharwa za kulinganisha juhudi za sasa za kujenga uchumi wa kitaifa na jumuishi unamlenga mtu mnyonge kama vile ni sawa na mapambano ya kumng’oa ukoloni ulio kuwa na nia ovu ya kinyonyaji kwa manufaa ya chi za kipebari.
Dhana ya Mwalimu Nyerere juu ya Uhuru ilikuwa bayana ni Uhuru wa kitabaka ukimlenga mtu wa tabaka la wanyonge kuondokana na mfumo wa kibeberu uliondoa utu kwa minajiri ya kulimbikiza mali kwa njia unyonyaji wa nguvu kazi na rasilimali za nchi na kusafirishwa nchi za Magharibi.
Hata neno “mabeberu” ndio dhana kuu iliyotawala maono na mapambano ya Mwalimu ambayo kwa sasa wapinzani hawataki kuhisikia maana inawachoma na kubomoa genge lao la ukwapuaji na kunadi sera za kinyonjaji zinazopiginia Uhuru wa uliberali mambo leo wenye nia ile ile ya historia ya ukoloni iliyokuwa na lengo kubwa la kulimbikiza mali kwa kupitia ulaghai. Na ulaghai huu unachochochewa na askari hawa kukodi wanaosambaza dhana ya ukombozi wa kweli wa kujenga Uhuru wa kiuchumi na fikra zinazopiginia wanyonge.
Dhana ya Uhuru ya wapinzani inashadadia mgawanyiko wa kijamii unachochea mfalakano, lakini pia kutia dhana ya Uhuru mamboleo inafifisha juhudi za pamoja za taifa la kizalendo la wanyonge kukata minyororo ya unyonyaji.
Inasukuma kubomoa nguvu ya demokrasia ya umma; maana mabeberu wanaogopa nguvu ya umma wa wanyonge na dhana ya kiliberali ya kujenga Uhuru uliojikita kwa mtu mmoja ni mkakati wa kuua nguvu ya tabaka kupigania kubomoa mfumo wa kibepari unaokosa utu na haki kwa maslahi ya watu wachache wenye mitaji(mabepari).
Mwalimu Nyerere alipata msukosuko kutoka chi za Magharibi alipokuwa anapinga waziwazi kupitia hatua zake za kukemea na kuweka sera thabiti za kuwathibiti mabeberu. Kwa Mwalimu ubepari ndio ulikuwa adui wa Uhuru wa kweli. Kwa wapinzani neno kama “mabeberu, ubepari; matabaka nk. yenye fikra za kimapinduzi unafunikwa kapuni.
Ni jukumu la watanzania wenye nia njema kuendelea kuibua propaganda hizi ambazo zinaenezwa kwa kasi ili kufifisha nia ya kuleta ukombozi wa kweli wa kiuchumi na kifikra unajenga demokrasia ya kweli inayosimamia ugawanyaji wa rasilimali za Taifa kwa wote pasipo kutoa mwanya maslahi ya wachache ya wanyonyaji kututia upofu kwa maneno yaliyokolezwa na kulebwa “Uhuru wa mawazo”. Tujenga Uhuru wa mawazo unapinga unyonyaji na uzalendo wa kulinda masilahi mapana ya wanyonge.
Tukatae ulaghai wa walio uza utu wao na kupiginia ukoloni mamboleo kwa kisingizio cha kudai Uhuru!