Upotoshaji: Napinga uzi unao sema Diamond kamfananisha yesu na mwanamke

crankshaft

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,411
3,374
Kuna uzi wa kupotosha umefunguliwa ukilenga kupotosha watu dhidi ya wimbo wa msanii Diamond uliotolewa hivi karibuni na naona unazidi kupata umaarufu mkubwa hapa jukwaani.

Na wachangiaji wake wengi wameonekana kusapoti uzi huu bila kuthibitisha hali inayosababisha kuchafua image ya Msanii Diamond mbele ya jamii bila sababu za msingi.

Mistari halisi ya wimbo wa Diamond inasema
"Wewe ndio wangu yesu mkombozi sa mbona petro unaniacha mwenyewe."
akifananisha kitendo cha yeye kuachwa sawa na yesu alivyo muacha petro
yaani main theme hapo ni kuachwa ndio maana katumia kisa kizima cha petro kuachwa na yesu na hajamtaja yesu kama mwanamke.

Ila mtoa mada kasema".... wewe ndio wangu yesu mkombozi sa mbona unaniacha mwenyewe..."
mtoa mada ameamua kutoa neno petro ili kuhalalisha upotoshaji na kumfarakanisha Diamond na jamii ya kikristo.

Hakuna kosa lolote hapo kifasihi zaidi tu tuseme kijana katumia ubunifu.

Wana jf tuwe makini tunapoanzisha na kuchangia uzi tusiwachafue watu mbele ya jamii bila sababu ya msingi.
 
Hata angemtukana atajipa laana mwenyewe
Ukristo umejengwa katika misingi ya waabuduo katika roho na kweli ndio wata urithi ufalme wa Mungu.
Hakuna mkiristo wa kweli ataanzisha vita ya kumtetea Kristo masiha maana Nguvu na uweza una yeye Kristo akiona kuna kosa diamond kafanya atajua nini amfanye!
Mungu wetu ni Mungu wa upendo kama Diamond kakosea amsamehe hajui atendalo.
 
Misukule bana😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Lini yesu alimuacha petro
That's wrong

Petro ndiye aliyemkana yesu

Usimtetee jamaa kazingua
 
Kama hukuwaelewa, wanachobishania ni hayo maneno 5 hapo
mi nimewaelewa,rudi tena ule uzi mtoa mada kasema
"..we ndio wangu yesu mkombozi sa mbona unaniacha mwenyewe..."
Ila Diamond kasema
"...we ndio wangu yesu mkombozi sa mbona petro unaniacha mwenyewe..."

Karuka neno petro ili kuhalalisha upotoshaji na kumchafua bwana mdogo.
Huoni utofauti mkubwa wa kimaudhui hapo???
Kama uzi utaachwa utembee,utamchafua bwana mdogo mbele ya jamii ya kikristo bila sababu ya msingi.
 
Hata angemtukana atajipa laana mwenyewe
Ukristo umejengwa katika misingi ya waabuduo katika roho na kweli ndio wata urithi ufalme wa Mungu.
Hakuna mkiristo wa kweli ataanzisha vita ya kumtetea Kristo masiha maana Nguvu na uweza una yeye Kristo akiona kuna kosa diamond kafanya atajua nini amfanye!
Mungu wetu ni Mungu wa upendo kama Diamond kakosea amsamehe hajui atendalo.
ndio nakwambia hajakosea. Kama umeelewa nilichosema, nadhani utafuta comment yako hapa.
 
Kuna uzi wa kupotosha umefunguliwa ukilenga kupotosha watu dhidi ya wimbo wa msanii Diamond uliotolewa hivi karibuni na naona unazidi kupata umaarufu mkubwa hapa jukwaani.
Na wachangiaji wake wengi wameonekana kusapoti uzi huu bila kuthibitisha hali inayosababisha kuchafua image ya Msanii Diamond mbele ya jamii bila sababu za msingi.

Mistari halisi ya wimbo wa Diamond inasema
"Wewe ndio wangu yesu mkombozi sa mbona petro unaniacha mwenyewe..."
akifananisha kitendo cha yeye kuachwa sawa na yesu alivyo muacha petro
yaani main theme hapo ni kuachwa.
Lakini mtoa mada ameamua kutoa neno petro ili kuhalalisha upotoshaji.

Hakuna kosa lolote hapo kifasihi zaidi tu tuseme kijana katumia ubunifu.

Wana jf tuwe makini tunapoanzisha na kuchangia uzi tusiwachafue watu mbele ya jamii bila sababu ya msingi.
Mpumbavu umekuja kumtetea mpumbavu mwenzio humu unadhani utapata huruma? Yesu afananishwe na demu wa diamond wa kufikirika halafu iwe sawa? Diamond ni Muislamu haya mafundisho ya Yesu na Petro kuyapeleka kwenye mapenzi amefundishwa na nani? Yesu na Petro walikuwa wapenzi?
Tena usituudhi kibaraka mchumia tumbo mkubwa. Kamwambie huyo fala mwenzio, Wakristo tunamuhitaji.
 
mi nimewaelewa,rudi tena ule uzi mtoa mada kasema
"..we ndio wangu yesu mkombozi sa mbona unaniacha mwenyewe..."
Ila Diamond kasema
"...we ndio wangu yesu mkombozi sa mbona petro unaniacha mwenyewe..."

Karuka neno petro ili kuhalalisha upotoshaji na kumchafua bwana mdogo.
Huoni utofauti mkubwa wa kimaudhui hapo???
Kama uzi utaachwa utembee,utamchafua bwana mdogo mbele ya jamii ya kikristo bila sababu ya msingi.
Hoja yao kwa nini atumie mfano wa Yesu?
Wangetaka aseme "We ndio mama dangote wangu mkombozi...."
kitu kama hicho!
 
"... wewe ndio wangu yesu mkombozi sa mbona petro unaniacha mwenyewe..."
Hebu niambie umeelewa nini hapo??? Ndio maana Diamond hakuishia kusema
"... wewendio wangu yesu mkombozi."
Halafu pia kama alimaanisha hivyo mtoa mada, kwa nini aliruka neno petro??? Ule ni uchonganishi bro.
 
Tunakubaliana hapo kwenye huo mfano wa Yesu anazungumzia pisi. Kwa kwenye kichupa hiyo pisi inaweza kuwa nusu uchi...Anyway, acha wenyewe watetee hoja zao
 
Dhamira kuu: kuachwa
Matumizi ya lugha: lugha ya ufananisho
Kama vile yesu alivyo muacha petro wakati anaondoka kwenda mbinguni ndivyo mtunzi naye ameachwa. Ndio maana ametumia kisa kizima cha yesu kupaa kikimuhusisha petro.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom