Upotoshaji kuhusu mizimu

badison

JF-Expert Member
May 29, 2015
593
1,000
Yes ulichoandika n sahihi kwa .Mana jamii zote diniani Zina Mila zao za kuwakimbuka marehemu wao .Nakupa mfano unaweza zaa mtoto mtoto ukamuita jina flani lakini akalikataa hadi umpe lile la asili ndo anakua vzr.Pia ni haohao mizimu ndo wanatulinda ambao mnandangnywa na wazungu eti n malaika.Umeongea up kweli Shukurani Sana.

Asante kwa kuelewa
 

badison

JF-Expert Member
May 29, 2015
593
1,000
Binafsi baada ya kusoma na kupata ukweli kwanini dini ziliumbwa na wazungu na waarab, kwa kweli sina hamu tena na hizi 'Abrahamic' religions kwani zote ni man made na hazina umungu wowote. Yes, nasema hazina Umungu wowote, zimetungwa kwa ajili ya kutawala binadamu tu, matokeo yake people don't think na kuwa watumwa wa fikra tu. Dini ya ukweli nimebaini ni kuabudu mizimu na Mungu tu.

Hizi dini ni uongo na ukiwa unaomba baraka haziji kwako zinaenda kwao wenye mungu wao ndo mana watu weusi tuna makanisa na misikiti mingi maendeleo hakuna.
 

badison

JF-Expert Member
May 29, 2015
593
1,000
Huu ndio ukweli unaotusumbua watu weusi, Wazungu wana dini yao, Waarabu wana dini yao, Wahindi wana dini yao, Wachina wana dini yao, na wanaziishi dini zao, ila cc waafrika tulizikataa dini zetu.

Upo sahihi ila kinacho waumiza watu weusi ni kwamba hawataki kukataa uongo na kukubali ukweli kuwa hizi dini hatukuzitaka kwa hiari bali tulilazimishwa kwa nguvu kuzikubali.
 

Mancobra

Member
May 31, 2021
54
125
Sina haja ya kutoa salam. Kwani najua wengi hampo salama.

Nimeamua kuleta mada hii tata ili kuwafumbua macho walio wengi. Kwanza nakiri kwamba ukweli unashangaza sana. Truth is stranger tha finction. Asilimia 75% ya watu weusi ni watumwa.

Mizimu ni roho za watu ambao ni ndugu zetu waliokufa ambao wamekuwa trapped in 4th dimension na binadamu wa kawaida tupo third dimension. Wao ndio viumbe wa karibu na sisi sana ukizingatia kuna nine dimensions ulimwenguni. Wote sisi ni wasafiri. Na mwisho wa safari yetu ni tisa.

Wengi wa watu weusi wana laana ya asili kwa sababu ya utumwa wa fikra. Lakini silazimishi mtu akiamini kile nachotoa hapa. Kwani wengi wamekuwa trapped by by the matrix system.

Kila jamii zilizo tuzunguka zina miungu yao. Mfano wayahudi (waisraeli) wana mungu wao wa musa aliyetajwa kitabu cha mwazo. Wanasema ni mungu wa haki. Amesemwa ni mngu wa haki kwani ameweka sheria na adhabu kali kwa mwanadamu. Na mungu wa waisraeli ni mungu wa Time (muda) ambaye ameumba vitu. Sikatai.

Pili kuna mungu wa agano jipya chini ya yesu ambaye ni mungu wa upendo. Mungu huyu yupo na anaabudiwa na warumi( warumi ndio wazungu wa sasa hivi au roman empire)

Mungu wa waisraeli, warumi na waarabu ni mungu wa muda hata ukisoma vitabu vyao kila saa wanajisifu wao ndio wana control time.

Kila jamii za kidunia zina miungu yao mfano wahindi wana mungu brahma, kali, vishu na krishna nk., wachina wana budha pamoja na wajapani na watu wote wenye asili ya macho madogo mungu wao ni sanamu lenye tumbo kubwa linaitwa budha.

Waarabu mungu wao ni allah ambaye anawakiliswa na jiwe lipo maka linaitwa black stone jiwe jeusi ambalo lipo al kaba jiwe hilo lilishuka duniani toka kipindi cha adamu na hawa na watu wakienda kuhiji wanalibusu na kusujudia jiwe hilo kwa kulizunguka mara saba. Jiwe hilo linaitwa hajr al aswad.

Ni ibada ya kuabudu sanamu lakini waislamu wengi hawajui ukweli huu. Ndo mana wanipagana vita na kuwauwa watu weusi wenzao kwa makundi kama boko haramu na al shabab. Ni sawa na mawe yanayotumiwa kuchonga sanamu la yesu wa wakrito wakaliabudu. Haina tofauti wote waislamu na wakristo wote wanamuabudu Saturn au Kronos ndo mana waslamu wanaamini biblia ni kitabu cha mungu ambaye ni saturn katika nguzo zao za imani. Nasisitiza mungu wa wakristo ni Saturn pamoja na waislamu ili ujuwe huu ukweli lazima uwe INITIATE. Kawa wewe sio INITIATE utaishi kutoa sadaka na sijda.

Kronos Ndio mungu wa waislamu na wakristo. Na nguvu zake sio kamili kwani mungu halisi hatoi adhabu wala hataki kunyenyekewa ni mungu wa upendo haijalishi unafanya mabaya au hapana yeye yupo tuu wala hawezi kuhukumu kitu. Duniani tupo kwaajili ya kujifunza hivyo hakuna zuri wala baya. Inategemeana na tafsiri ya kile unachokiona nikzuri kwako kinaweza kuwa kibaya kwa mwenzako.

Kwa sasa kuna mawakala wengi sana makanisani na kisikitini wakiwaaminisha kuwa mizimu ni roho chafu za kuzimu ilihali wakijuwa wao wamepokea shahada za ki freemason ambazo ni ibqda za wazungu na hii ipo katika historia ya mqmbabu zao kwamba ndio asili yao wazungu. Wanawatoa watu weusi wenzao katika ukweli ili kulinda maslahi yao ya kidunia.

Wanachofanya hawa watu wazungu ni kututoa katika asili yetu na sisi kufata mambo yao.

Mzimu ni baba au mama yako aliyekufa je baada mzazi wako akifa utamchukia au utamkumbuka kwa wema aliokufanyia kwa malezi mpaka hapo ulipo fika.? Baba na mama yako nao wana wazazi wao ambao nao walisha tangulia mbele za haki mlolongo unaendela hivo. Lengo la ibada ya mizimu ni kutoa shukrani kwa walio tutangukia kwani wao wanatuona ila sisi hawatuoni ila sio kuwa abudu. Kuna tofauti ya kutoa shukranu na kuabudu mfano kujenga kaburi la ndugu au jamaa ni kuonyeaha shukrani fulani.

Wanachofanya watu wa dini mfano wakristo na waslamu kupiga vita mizimu hasara yake hutaiona hapa duniani na pindi utakapo kufa utawakuta ndugu zako na ma bibi na mababu zako ila hawata kupokea kama sehemu yao kwani wakati upo duniani uliwadhihaki na kuwa adui kwao.

Mizimu wanachotaka ni kuwa na hisia za kibinadamu kutowa sadaka mbali mbali kwao ikiwamo za wanyama kwani huwa wametuzunguka na mkikutana kama ukoo huwa wapo na hupenda.

Mizimu inapenda pombe maji au wanyama wanaochunjwa kwa hesma yao kwani ndio life style ya mwanadamu toka enzi watu wanakunywa pombe. Kwa vitu hivo unatengeza conection ya mafanikio yako hapa duniani na ukifa utakuwa na watu watakao kupokea. Ukifa unaenda sehemu ya ugenini lazima uwe na wenyeji walio kutangulia.

Kama ulivyo zaliwa hapa duniani ukapokewa na wazazi wako na ndugu zako na pia utakapo kufa jua kuna wenyeji ambao walisha kutangulia ambao watakupokea. Je hao wenyeji uliwafanyia jambo gani la maana kuonyesha heshima kwao. Wakati bila wao wewe usinge weza kuzaliwa. Kumbuka marehemu babu yako na bibi yako ndio walizaa wazazi wako ambao unawapenda. Na wazazi wako wana wazazi wao ambao wana wapenda na kuwakumbuka cheni ni ndefu sana kurudi nyuma mpaka wewe ukawepo hapo ulipo daganywa na stori za biblia ya warumi na kurani ya waarabu.

Dini zote ambazo mnaziabudu zote zililetwa na watesi wetu na kuwachukua babu na bibi zetu kama watumwa na wameua watu weusi wengi sana. Alafu leo unajifanya mlokole au mkristi safi au muslam safi jua unajidanganya na unaungana na maadui za wazee wetu na kusahau mila.

Ukoo hauishi, kama ulivyo pokelewa hapa duniani na wazazi wako utapokelewa na ahera na mizimu ya waliokutangulia kama ulikuwa unawatoa katika jina la yesu ndonutajua sasa utakapo ishia na mtu akifa kinachobakiwa nae ni kumbukumbu za maisha yake.

Watu weusi ni watumwa wa fikra za historia ipo wazi kuwa tulijishusha chini na kupokea tamaduni za watu wengine hasa waarabu na wazungu. Ili tufanikiwe gundueni tatizo lipo wapi kwanini tuna mali zote lqkini hatuna baraka tupo katika lindi la umaskini na kusalitiana?

Mfano wa wazi ni filamu ya vikings ambapo ragnar alisahau mizumi ya asili kwao kwa kupokea ukristo na mizimu ikamsahau. Ile filamu ni kwaajili ya kutoa fundisho usisahau ulipo toka.

Mimi siabudu mizimu ila natoa shukrani kwa wazee wangu wote waliotangulia mbele za haki ambao bila wao nisinge weza kuzaliwa na baba na mama yangu kwa kutia sadaka ya denge au maji au chochote nachotaka. Kuna mahali nimwekea alter maalumu ila hakuna anaye ishi hapo porini. Ila kwakuwa najua mizimu ipo na mimi inajua nachofanya.

Ombi langu kwako usigombane na mizimu ya watangulizi wako kwani huwezi jua kama wao ni mizimu huenda na wewe ukawa mzimu pia ila ukiwa mzimu wenye maaadui upande wa pili itakuwa ngumu kwako.

Heshimuni tamaduni zenu tukutane mwezi 12 nyumbani. Kuwa kwako mkristo autimatiki unaona waslamu wanaenda motoni wahindi wanaenda matoni na wayahudi pamoja na watoa shukrani kwa mizimu hii ndo mentality wa matrix wana kuwa na Ego kwamba wao dini yao ndo ya haki na wengine wapo dini ya uongo kumbe wote wamepotea.

Wewe unapokesha kumsifia mungu wa waisraeli usije kudhani eti baraka zinakujua kwako hapana zinaenda kwa waisrael na vilevile unavyo msalia mtume na allah baraka zote zinaenda kwa waarabu ndo mana mtu mweusi ni maskini wa mali akili na fikra.

Elimu hii sio ya ku google ni urithi wangu niliopewa. hivo usije kuniambia uislamu au ukristo ni dini ya haki nikikuomba ushahidi ukaniletea maneno kwa biblia imesema au qurani imesema wewe ulikuwepo au wewe ni mwarabu au mrumi.? Pita hivi.
Africans ni viumbe pekee dunian tunaotapatapa kwenye kila sekta, hii yote inasababishwa na kuikana asili yetu yani saiv hakuna utumwa wa nguvu tupo kwenye utumwa wa kifkra; leo hii africans tunakana majina yetu kwa kisingizio Cha din(ubatizo), tunakana lugha zetu kwa kisingizio Cha kuelimika, tunakana teknolojia zetu kwa kisingizio Cha kuitwa uchawi, mifano ni mingi....ila yote kwa yote africans Kama tunataka maendeleo ni lazma tuwe huru kifkra, kuanzia dini mpk teknolojia. Ukiangalia madhara ya kuiga iga tamaduni za watu ni umaskini tulionao. Leo hii ukimwangalia mzungu utaona anaishi lifestyle tofaut kabsa na ya mchina, mhindi n.k....lakn ukija africa watu tumegawanywa kuna waliomfata mzungu,mwarabu n.k...
Africans lazma tujitambue kwa kusoma history tujue hizi din na vitu tunavyoviona vipo kwa sababu gani?
 

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
5,131
2,000
uzi wako ni mzuri bt bado unahitajika kujifunza zaidi kuhusu haya mambo, mizimu hiyo hiyo inatumiwa na wachawi katika kufanikisha mission zao za kuuwa/kuwatupia uchawi watu.

nikiwa shule nimewahi pitia matatizo ya kuumwa kichwa na kutoona vizuri nikatumia dawa wapi... nikaambiwa kwa sababu natumia jina la babu basi mizimu wananitaka ninunue mazaga yao nikafanya hivo bt matatizo ndo yakazidi, nikafanyiwa hadi matambiko lakini wapi, kilichofuata nikachoma kila kitu na kutoamini tena upuuzi huo ndipo hali ikawa sawa nikaendelea na shule, mambo ya mizimu ni mambo ya kipumbavu sana.

kitu pekee ulichopatia katika uzi wako ni "mungu halisi hatoi adhabu wala hahitaji kunyenyekewa"
 

Master Arcade

JF-Expert Member
Apr 21, 2021
242
500
Hizi dini ni uongo na ukiwa unaomba baraka haziji kwako zinaenda kwao wenye mungu wao ndo mana watu weusi tuna makanisa na misikiti mingi maendeleo hakuna.
Ni kwa sababu maendeleo hayatokani na sala Bali kufanya kazi kwa bidii na kuyatawala vyema mazingira yako.
 

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,241
2,000
MUNGU AKUPE REHEMA YA KUJUA KWELI, By the way hata yao wazungu nao hufa..so nao pia wanakuwa mizimu sio!? So nao wanawaabudu Kama unavyotuambia hapa kuhusu africans tuitunze mizimu!?

Mzee..kilichokufa kimekufa..ni sawa na mwembe uliokauka..usitarajie mwembe yataota juu yake.
 

Mzimu wa Kolelo

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
1,604
2,000
Mizimu ni MAJINNI yaliokaa sehemu sehemu tangu enzi za mwanzo wa dunia
Na kufahamu mila tamaduni za eneo husika na kuzirithisha kutoka kizazi hadi kizazi nawe ukiwafatilia basi utawarithisha
Watoto wako

MTOTO
"mama jana nimelala nimeota mtu mweusi ana madevu na shuka jeupe kashika kirungu akakaa pembezoni mwa kitanda akawa ananiongelesha mimi sikumuelewa"
MAMA
"Huo ni mzimu wa babu yako kesho twende kwenye MZIMU kule kweye mbuyu tukatambike
Inabiki apatikane kuku mweusi na mtama robo mchele robo uwele robo
Na kaniki 1"

Kesho hao wanachukuzana kupanda milima na mabonde wanajichosha kutembea kufata mzimu msituni huko

Kumbe yule alomtokea ni JINNI alojivika sura ya marehemu babu yake
Nia na dhumuni kuwahadaa tu wanadamu walokosa mahalifa sahihi
 

badison

JF-Expert Member
May 29, 2015
593
1,000
Mizimu ni MAJINNI yaliokaa sehemu sehemu tangu enzi za mwanzo wa dunia
Na kufahamu mila tamaduni za eneo husika na kuzirithisha kutoka kizazi hadi kizazi nawe ukiwafatilia basi utawarithisha
Watoto wako

MTOTO
"mama jana nimelala nimeota mtu mweusi ana madevu na shuka jeupe kashika kirungu akakaa pembezoni mwa kitanda akawa ananiongelesha mimi sikumuelewa"
MAMA
"Huo ni mzimu wa babu yako kesho twende kwenye MZIMU kule kweye mbuyu tukatambike
Inabiki apatikane kuku mweusi na mtama robo mchele robo uwele robo
Na kaniki 1"

Kesho hao wanachukuzana kupanda milima na mabonde wanajichosha kutembea kufata mzimu msituni huko

Kumbe yule alomtokea ni JINNI alojivika sura ya marehemu babu yake
Nia na dhumuni kuwahadaa tu wanadamu walokosa mahalifa sahihi

Hiyo ni hatua ya kwanza ya kufahamu mambo
 

Luggy

JF-Expert Member
Aug 6, 2012
3,049
2,000
Mbona Wazungu nao walipelekewa Injili kama sisi lakini wameendelea.Maana ukweli ni kwamba nao walikuwa na dini zao,walipelekewa Injili wakaachana na dini zao za asili,...tusihalalishe kutokuendea kwetu kwa sababu nyepesi.
 

badison

JF-Expert Member
May 29, 2015
593
1,000
Mbona Wazungu nao walipelekewa Injili kama sisi lakini wameendelea.Maana ukweli ni kwamba nao walikuwa na dini zao,walipelekewa Injili wakaachana na dini zao za asili,...tusihalalishe kutokuendea kwetu kwa sababu nyepesi.

Wazungu hawakupelekewa injili yoyote wazungu ndo Roman Empire wao ndio waanzilishi wa hiyo injili Soma mqmbo ya First Council of Nicaea. Mkutano Uliitishwa na kusimamiwa na kaisari Konstantino Mkuu, aliyehofia mabishano kati ya raia wake Wakristo kuhusu Yesu Kristo, ambayo yalihatarisha umoja na usalama wa Dola la Roma lililoanza kuelekea kusambaratika. Yeye aliwaalika maaskofu wote wa dola, waliokuwa kama 1000 mashariki na kama 800 magharibi. Hapo ndu ukristo ulipoanzishwa
 

Luggy

JF-Expert Member
Aug 6, 2012
3,049
2,000
Wazungu hawakupelekewa injili yoyote wazungu ndo Roman Empire wao ndio waanzilishi wa hiyo injili Soma mqmbo ya First Council of Nicaea. Mkutano Uliitishwa na kusimamiwa na kaisari Konstantino Mkuu, aliyehofia mabishano kati ya raia wake Wakristo kuhusu Yesu Kristo, ambayo yalihatarisha umoja na usalama wa Dola la Roma lililoanza kuelekea kusambaratika. Yeye aliwaalika maaskofu wote wa dola, waliokuwa kama 1000 mashariki na kama 800 magharibi. Hapo ndu ukristo ulipoanzishwa
Okay...hivo ndo umeelewa ww,lkn ukisoma Kitabu cha Matendo ya Watume utaelewa jinsi Injili ilivoenezwa kutoka Uyahudi kwenda Asia,Ulaya na maeneo mengine.Hao Rumi hawakuwa Wakristo hapo kwanza,walikuwa na miungu yao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom