Upotoshaji huu wa Gazeti la Jambo Leo ni mpaka lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upotoshaji huu wa Gazeti la Jambo Leo ni mpaka lini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngaliba Dume, Apr 16, 2012.

 1. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Leo ktk gazeti la Jambo Leo, ukurasa wa kwanza kuna kichwa cha habari kinachosema CHADEMA Inahusishwa na mashetani, na eti Dr.Slaa ana jini lake linalomsaidia mambo yake ya kisiasa, pia ktk dini hiyo kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Pope naye yumo.

  Mwandishi amekwenda mbali zaidi kwa kumuhusisha Marehemu Kanumba na hiyo dini ya mashetani. Katika kujenga hoja amewaonyesha viongozi mbalimbali wa Dunia kuwa ni waumini wa dini hyo ya kishetani.

  Nimesikitishwa na umbumbumbu wa mwandishi, ujengaji wake wa hoja na zaidi kuwadhalilisha watu bila ushahidi wa kimantiki..msingi wa hoja yake kuwa CHADEMA na Dr. Slaa ni wafuasi wa shetani ni aina ya salamu ya vidole viwili inayotumiwa na CHADEMA, kuwa ni salamu ya kishetani na hivo CHADEMA ni ya mashetani na Dr. Slaa ana jini linalomlinda.

  Kwa kweli huu ni upotoshaji mkubwa,haupaswi kuachwa,kulivamia pia kanisa kwa kumuhusisha kiongoz wao ni upotoshaji,ni kuuambia umma kuwa wote walio chini ya kiongozi huyo (Pope) nao ni waabudu sanamu!huu ni uzushi,uzandiki na ukomo wa uelewa wa mambo ya kidunia.

  MY TAKE:...Alama ya "V" inayotumiwa na CHADEMA haina uhusiano na mashetani. Miaka mingi iliyopita, Jemedari wa vita toka Urumi(Roma) Julius Caiser aliwavamia maadui zake na kuwapiga kwa kusafiri umbali mrefu, alipofika ktk himaya ya adui aliua na kuteketeza kila kilicho cha adui..kufikisha ujumbe kwa walio Rome na Senator J.Caiser alisema "Veni,Vidi,Vici" = "I came,I saw,I conquered".. Hii ndo ikawa alama ya ushindi,na J.Caiser alipopita mbele za watu alikunja vidole kwa alama ya V kama tafsiri ya ushindi, na askari wote waliopigana ktk vita hvyo waliwekewa alama ya "V" tatu ktk mabega yao kama alama ya ushujaa,na toka hapo V ikawa alama ya cheo ktk jeshi...

  Kumbe alama ya V kwa CHADEMA si ushetani, haina mahusiano na mashetani...ni alama ya "Victory"...mashabiki wa mpira hutmia, wachezaji na hata makocha wao (japo wengine hufikili kuwa wanamanisha watashnda goli mbili).,si CHADEMA peke yao! JAMBO LEO Lisigeuke kuwa udaku, lisidhalilishe dini na viongozi wa watu, wajiheshimu! Wasitumike..kuna mbinu nyingi za kuibana Chadema lakn si kwa mtindo huo! kweli CHADEMA imewabana na bado kidogo mtaachia...NAWASILISHA
   
 2. domo bwakubwaku

  domo bwakubwaku Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  magamba at work haya mambo wanaayaanzisha wenyewe mwisho yankulaga kwao hivi tukianza kuwataja waumini wa freemasons hapa mjini mbona magamba watakimbia
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Labda walikosa heading ya maana wakaon iyo itauza!
   
 4. qq.com

  qq.com JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 9, 2012
  Messages: 370
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nani mmiliki wa gazeti hili?
   
 5. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hii ni hatari, huyo mhariri aliyeidhinisha huo upuuzi uchapwe ni balaa kubwa zaidi! Sijui wanatumia nini kufikiri hawa majitu!
   
 6. M

  Mukalunyoisa Senior Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Basi hata mmlikiwa gazeti naye ni freemason
   
 7. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Vijana waliomkamata Ghadafi na kumuua kule Libya walikuwa wanashangilia kwa kuonyesha alama ya V... Je nao ni Freemasonry??
   
 8. B

  Babuu Rogger JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 80
  Hili gazeti linatumiwa sana na MAGAMBA baada ya kuona gazeti la Uhuru halisomwi tena.
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Dr Ridhiwani Kikwete LLB,LLM,LLD
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Juma Pinto
   
 11. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,175
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Na jeshini mtu mwenye cheo cha "vv" inamaanisha ana mashetani mawili...lol. CCM wapo katika wakati mgumu Watanzania tushirikiane kuikataa katakata CCM
   
 12. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Watu wanaposikia kuwa kuna hatua UKIMWI hushambulia mishipa ya fahamu, yaani mtu anakuwa na ''afya'' yake tu lakini kichwani anakuwa dakika tatu. Hali hii ikimpata mtu watu huwa hawaelewei hatua aliyopo mtu huishia tu kusema ''siku hizi fulani simuelewi ana mambo fulani ya ajabu sijui nini kimempata".
   
 13. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  V stand instead of VICTORY.wameishiwa propaganda
   
 14. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  TATIZO ni kwamba umesoma mwenyewe na kuchambua mwenyewe na kila mmoja anatakiwa ku-comment ulichoandika wewe!
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Aliyewakaribisha Freemason Tanzania ni Benjamin Mkapa.
  Kikwete na Sheikh Yahya, Kapuya, Membe, Mengi, Magufuli, Mkono, Mwale, Lowassa ni baadhi tu ya mamembers wa Freemason.
  Wana Lodge yao maeneo ya Ngaramtoni panaitwa Masonic Lodge.

  CHADEMA inawanyima usingizi magamba wamebaki wanahaha tu.

  Wao wana fedha za Freemason

  Sisi tuna Mungu tusiogope tutashinda!
   
 16. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hiki kijarida sijawahi kunkinunua hata kukisoma
   
 17. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Waandishi makanjanja,
  mnatumwa mumcha
  fue docta na chadema!
  Na mnamuweka na papa!
  Nyie hamna adabu.
  Mmetafuta mbinu nyingi
  za kumchafua lakini docta
  hachafukiki. Tena watakao
  soma watawaona ni
  makanjanja!
   
 18. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  ukiunganisha hizi dots zote huwezi kumuweka nje Sheikh Yahaya na kama unavyojua hawa jamaa kwenye mtandao huu hawaamini kitu kingine chochote mbali ya mashetani kuwa ndio chanzo cha mafanikio. Hivyo wakiona mtu yeyote anaelekea kufanikia katika jambo lolote ni lazima wayaongee mambo haya wazi wazi kudhiirisha wanachokiamini.

  Fanya mambo yako mengine, achana na hao. Kibaya pesa ilishaingia mikononi mwao!


   
 19. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hana uelewa na alichokiandika.
   
 20. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #20
  Apr 16, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,058
  Likes Received: 3,241
  Trophy Points: 280
  Mbona hata marehemu AA Karume alionyesha vidole hivyo? a-google aone na atuambia kama na yeye ni freemason.
   
Loading...