KITAULO
JF-Expert Member
- Apr 27, 2018
- 1,926
- 2,777
Wadau,
Ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya member/ wadau wakipotosha wenzentu (wanaoshi na VVU) kuhusiana na matumizi ya ARV au kwa jina lingine dawa za kufubaisha makali ya virusi vya Ukimwi. Kumekuwa na utaratibu wa kuanzisha mada ali maarufu kwa nyuzi ambazo kiuhalisia ni potofu au za kuhadaa kuwaasa au kushauri waathirika kuepuka/kupuuzia matumizi ya ARV.
Ukweli ni kwamba hizi dawa zimekuwa msaada mkubwa kwa wenzetu wenye maambukizi. Hebu tujaribu kuvuta kumbukumbu hali ilivyokuwa kwa kipindi kile cha miaka ya tisini (1990s) hali ilivyokuwa mbaya. Tulipoteza ndugu jamaa na marafiki wengi mno kwa vifo vya kudhalilika. Watu walikuwa wanaisha na kubaki mifupa mitupu, vidonda mwili mzima, kupungua uzito kupita maelezo.
Serikali kushirikia na wahisani wamekuja na suluhisho la kuokoa nguvu kazi kwa kugawa dawa za kusaidia watu waweze kufikia malengo yao hali kanakwamba wanamaambukizi na tumekuwa mashahidi kwa kuona watu wanaishi hata kwa zaidi ya miaka 35 baada ya kupata maambukizi na hata mwisho wa safari zao za maisha wakifa kifo chema kwa maana ya kutokuteseka ama kudhalilika kama hapo mwanzo, kama Ukimwi ungekuwa ni habari za kusadikika mpaka leo tungekuwa na msanii maarufu wa kundi la QUEEN BAND..FREDDIE MERCURY. Nadhani kwa wachache tumewahi kusikia habari za huyu nguli aliyefariki mwaka 1991 kutokana na Ukimwi akiwa ameishi miaka 6 tu tangu agundulike ni muathirika mwaka 1985. Huyu angekuwepo mapaka leo pengine kama ARV zingekuwepo.
Nakumbuka vizuri nikiwa kijana mdogo mwaka 1995 mama yangu aligundulika ni mwathirika hii ilitokana na baba baada ya kugundua kupoteza tumaini kabisa kilichopelekea kuchukua uhai wake kwa kunywa madawa mengi mwaka 1996. Mama aliikubali hali yake na kupambana mpaka mwaka 1998 safari yake ilipokomea ikiwa ni miaka mitatu tu baada ya kugundulika, Mama aliteseka sana na alikuwa kifo cha mateso na kudhalilika mno. Naamini kama hizi ARV zingekuwepo pengine mpaka leo tungekuwa naye. Sasa mtu anaponiambia ARV ni sumu simuelewi kabisa.
Mfano mwingine dada yangu (twin wangu) anaishi na VVU kwa karibu miaka 16 sasa tangu agundulike mwaka 2004,na hii ilitokana na kukubali hali yake na kuanza matibabu ya ARV punde alivyotakiwa kufanya hivyo na wataalamu wa afya. Mpaka leo anadunda na afya yake ipo sawa kabisa na mtu wala hauwezi kudhani kama ni mwathirika.
NB: Ndugu zangu naomba mpuuzie udhalimu na upotofu wa hawa ndugu zetu wanaowalaghai muache matumizi ya arv. Serikali na wataalamu wa afya wanajua umuhimu wa hizi dawa na kweli zinasaidia mno
Ukimwi upo na unaua kinga kwanza mengine baadae.