Upopo Wetu Unaliangamiza Taifa!!

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Sisi watu wa ajabu kweli.
Kama wewe ni mgeni jitahidi sana kutuzoe!


Ukitutazama kama mabepari lakini eti ni wajamaa!

Wenye bidii ya kuizomea rushwa ya hadharani ilihali moyoni tunaishangilia!

Tunang'ang'ania kiswahili pasipo kukiacha kingereza.

Tunazuia bunge live; ila wakati fulani tunalionesha!

Hatutaki misaada vinywani lakini ukitupa mkononi tunachukua!

Hatufurahii mawazo mbadala lakini yakikosekana tunalalamika!

Tunalisusia bunge lakini ikiwa ni Lugumi tunaweza kutotoka!

Tunawalaumu viongozi wapole lakini wakija wakali hatuwashangilii.

Tunauchukia ufisadi wa wakubwa lakini wetu wadogo tunaupenda!

Tunapenda kula sana lakini kilimo kwetu kwetu ni ushamba!
 
...tunalilia demokrasia serikalini wakati kwenye vyama vyetu kumejaa udikteta na ubabe.
 
Tumewaimba mafisadi miaka nane lakini wakati chaguzi tuwafanya wagombea wetu pamoja na kuwadekia barabara.
 
Kipindi kile tuliponyimwa misaada na MCC kuna watu walikuja na ngonjera nyingi za hatutaki misaada na taifa limefika wakati wa kujitegemea, ajabu ni kuwa misaada inazidi kumiminika hadi sasa na wale wazalendo wa kujitegemea siwaoni wakiipinga......ama kweli kupigania tumbo inabidi akili uzitie mfukoni.
 
Back
Top Bottom