'Uponyaji wa majeraha' uanze na Objective journalism

afroPianist

Member
Nov 3, 2010
86
0
Kinyang'anyiro cha uchaguzi 2010 kimehitimishwa rasmi(ukiacha majimbo machache yasiyofanya uchaguzi). Mengi yamesemwa na kufanywa na mambo ya kutishia mustakabali wa umoja wetu yenye kutugawa kwa misingi ya dini yamejitokeza.

Ingawaje propaganda hizo zilianza na viongozi wa kisiasa na wa kidini,waandishi wa habari wamechangia sana kugongelea misumari ya moto kwenye majeraha hayo kwa kushindwa kwao kuwa objective. Hili limejitokeza hasa katika vyombo vya habari vya serikali,vyombo vya vyama vya siasa na vyombo vinavyomilikiwa na makada.

Kikwete amekiri kwenye hotuba yake ya kuapishwa leo kuwa 'walifanya mengi ya kuwagawa watu kwa udini,ukabila,u maeneo' na kutaka majeraha yaponywe.

Rai yangu ni pamoja na kumuasa Kikwete na wenzake kuacha kuchezea mambo nyeti ilimradi tu washinde uchaguzi na kutegemea 'wataponya' majeraha baadae, vyombo vya habari pia vianze kujirekebisha na kuacha kuyaongelea mambo nyeti kama dini zetu kwa mchezomchezo na uchochezi na pia kuwa objective kwenye kureport na kuandika makala. Hapa ndipo pa kuanzia!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom