Upofu wa Mwandishi huyu dhidi ya Mkoa wa Kagera. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upofu wa Mwandishi huyu dhidi ya Mkoa wa Kagera.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kenge (Eng), Jul 28, 2010.

 1. K

  Kenge (Eng) JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2010
  Joined: Dec 7, 2006
  Messages: 502
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Wednesday, 12 May 2010 05:13
  Na Reuben Kagaruki

  HIVI Karibuni nilikuwa mkoani Kagera ambapo nilipata fursa ya kuzungukia maeneo mbalimbali hasa yale ya mpakani. Kuna mambo ambayo mgeni yeyote yule akitembelea mkoa huo ni lazima yatamshangaza.

  Kwa wenyeji wao wanaona mambo hayo ni jambo la kawaida, kiasi kwamba hata waandishi wa habari waliopo mkoani humo hawawezi kunyanyua kalamu zao na kuyapigia kelele.

  Kwa mgeni kama ilivyokuwa mimi ni lazima atashangaa. Mfano leo hii mtu akitembelea maeneo ya mkoa huo kabla hata ya kusogelea mpakani anaweza kuhisi kuwa ameishangia nchi za jirani kama vile Uganda.

  Katika mkoa huo bidhaa zinazozalishwa nchini Uganda zinazouzwa upande wa Tanzania ni nyingi kiasi kwamba hauwezi kuamini kama nchi yetu nayo huwa ina viwanda.

  Hali ni mbaya zaidi maeneo ya mipakani. mfano mtu akifika maeneo ya Kyaka ataweza kujionea jinsi bidhaa za Uganda zinavyouzwa kwa wingi upande wa Tanzania.

  Utafiti mdogo nilioufanya ulibaini kuwa bidhaa za Tanzania ambazo zinauzwa kwa wingi maeneo ya Kyaka na Mtukula ni sigara na bia,baada ya hapo karibu kila kitu ambacho utapenda kugusa kimetengenezwa Uganda.

  Ukitaka kununua kiberiti, maji ya kunywa, mafuta ya kula, sukari, saruji, chumvi, wembe, vitana na vitu vingine vingi basi utauziwa vilivyotengenezwa Uganda.

  Hata ukitaka kununua pombe isiyokidhi viwango nayo pia inatoka Uganda. Anayekataa hili basi akaulize wakazi wa mkoani Kagera viroba vya konyagi aina ya Empire vinatengenezwa wapi? Viroba hivyo pamoja na kupigwa marufuku kutokana na kutokdhi viwango vya ubora ndivyo vinaonekana kuwainua vijana wengi wa mkoa huo kiuchumi.

  Ni kweli maeneo ya mpakani kunakuwa na mwingiliano wa bidhaa, lakini iweje upande wa Uganda kusiwe na bidhaa nyingi zinazouzwa Tanzania?

  Hii inaonesha kuwa ile tabia ya Watanzania kutodhamini vitu vyao na kuwa watumwa kwa vile vya kigeni inazidi kuongezeka. Siyo kwenye bidhaa tu, bali utumwa huo umegusa hata sekta nyeti ya elimu.

  Katika eneo hili nilitamani kutokwa na machozi baada ya kukutana na mzazi mmoja akipeleka watoto wake watatu wenye umri kati ya miaka sita hadi 10 kwenda kusoma Uganda.

  Baada ya kukutaka na mzazi huyo akisubiri basi maeneo ya Kyaka nilimfuata nikijifanya mgeni. Nilimwambia nina mpango wa kupeleka watoto wangu kusoma Uganda, hivyo niliomba anisaidie ilipo shule nzuri.

  Swali hilo halikuonekana gumu kwake kwa kujiaminialijibu kuwa; "Mbona Uganda kila shule ni nzuri, ndani ya miaka miwili watoto wanakuwa wanazungumza kiingereza vizuri." Baadhi ya watu waliosikiliza mazungumzo yangu na mzazi huyo waliungana naye kubeza elimu inayotolewa Tanzania.

  Hali hiyo ilinifanya niwaulize wananchi hao nikitaka kujua wale wasomi maarufu kwa jina la nshomile wa mkoani Kagera waliopo Dar es Salaam kama nao walisoma Uganda.

  Jibu lao lilikuwa hapana na walichokisisitiza wao ni kuwa elimu ya Tanzania kwa sasa ni tofauti na ile ya zamani. Nilianza kujiuliza ni kitu gani kinafanya elimu ya Tanzania inadharaulike kiasi hicho. Niliwauliza kama shule za serikali hazifundishi vizuri ni kwa nini wasiandikishe watoto wao kwenye shule binafsi zinazofundisha kwa kwa mitaala ya kiingereza?

  Bado wananchi hao walionekana kutokuwa na imani na shule hizo, badala yake waliendelea kusisitiza kuwa shule za Uganda zinafundisha vizuri. Hivi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi anafahamu kuwa elimu ya Tanzania inadharaulika kiasi hicho.

  Pamoja na Tanzania kusifika kama kisiwa cha amani ulimwenguni, hakuna mzazi yeyote wa nchi za jirani anayetamani kumleta mtoto wake kuja kusoma nchini. Leo hii imefikia hatua wazazi wengine wanatamani kwenda kusomesha watoto wao kwenye nchi za Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

  Kwa nini hatukai chini na kutafakari ni kitu gani kinafanya bidhaa na elimu ya Tanzania inadharauliwa? Leo hii tukizunguka katika mikoa ya Tanzania inayopakana na nchi jirani kama vile Burundi, Rwanda, DRC, Malawi, Msumbiji, Kenya na Uganda hauwezi kukutana na mtoto anayetoka kwenye nchi hizo anayeletwa kusoma Tanzania hasa kwenye shule zinazomilikiwa na serikali.

  Lakini sisi tukienda kwenye nchi zao vitoto vyetu vichanga vinapelekwa huko kusoma. Hivi kweli Tanzania inastahili kuzidiwa kwenye maendeleo ya taaluma na nchi ambazo tulizitangulia kupata uhuru.

  Kama ndiyo hivyo basi, kulikuwa na haja gani ya kudai uhuru mapema? binafsi naamini dhamira ya Baba wa Taifa Mwalimu Juliusi Nyerere kudai uhuru ilikuwa nzuri lakini kinachoharibu nchi hii ni kukosa viongozi wa zalendo.

  Mfano leo Waziri anaweza kwenda Marekani au Uingereza badala ya kujifunza jinsi wenzao walivyofanikiwa ili na sisi tujifunze kutoka kwao, hafanyi hivyo badala yake anatanguliza ubinafsi.

  Wapo mawaziri wanaondoka nchini hapa wakilipiwa nauli na posho za walipa kodi badala ya kutekeleza majukumu ya kitaifa yaliyoyapeleka, wanaaza kufanya mambo yao. Wengine wanaanza kuzunguka katika miji mbalimbali wakiuliza zilipo shule nzuri ili baadaye wapeleke kusoma watoto wao nchini humo.

  Wabinafsi wa aina hiyo ndiyo wanaochochea kila kitu kinachozalishwa Tanzania kuonekana hakifai. Viongozi ambao watoto wao hawasomi kwenye shule zetu ambazo zinadharauliwa ndiyo maana hawana machungu na yanayotukuta.

  Wakati umefika wa Rais Jakaya Kikwete kuwabana wasaidizi wake ili waoneshe uzalendo. Kama wasaidizi wake wanakimbia elimu ya Tanzania kuna haja gani ya kuwakumbatia ili waendelee kuongoza Watanzania wakati hawana uchungu nao?

  Uongozi inabidi uwe wa mfano kama ilivyo kwa mheshimiwa rais ambaye watoto wake wanasoma shule za hapa nchini. Hata kama shule wanaposoma watoto wake siyo Watanzania wote wanaweza kumudu ada yake, lakini ameonesha uzalendo wa hali ya juu.

  Wakati umefika sasa wakuwa na viongozi wenye uchungu na Watanzania. Niliyojionea mkoani Kagera yawe fundisho kwa viongozi wetu.


  NINA MASHAKA NA UPEO WA UELEWAJI!!! MKOA WA KAGERA UPO ZAIDI UPANDE WA UGANDA KULIKO MWANZA AU DAR AMBAPO VITU VINGI VINAPATIKANA KAMA NI VIWANDA UGANDA NI KARIBU KULIKO MWANZA AU SEHEMU NYINGINE ZA NCHI. SHULE ZA SERIKALI MPAKA WACHAPWE VIBOKO NDIPO WAFUNDISHE ZA BINAFSI BADO NI CHACHE NA NI GHALI KULINGANISHA NA UGANDA HATA ASILIMIA 70% YA WALIMU WANATOKA UGANDA. GHARAMA ZA USAFIRI WA BIDHAA ZA TANZANIA MPAKA MKOA WA KAGERA NI KUBWA NA KUSABABISHA BEI KUWA JUU. KWA NINI MWANANCHI AKIMBILIE UCHUNGU WA TAIFA NA HASIWE NA UCHUNGU WA GHARAMA. MWANDISHI AMKA KUMEKUCHA SIO KAGERA TU NENDA MIPAKA YOTE YA NCHI . TUNDUMA , SIRARI, NAMANGA, RUSUMO, NK. UONE MAMBO YAKOJE NA UONE WTU WA MIPAKANI WANATUMIA CURRENCY GANI, TEMBEA UTOE UPOFU HUU.​
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mwandishi wa makala ajifunze vile vile kuwa hata wakulima wanajua sana scales of economy.Mtu hawezi kununua kitu cha Tanzania wakati kitu kile kile kinauzwa karibu na bure mpakani.
   
 3. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Lole, your argument is faulty. Mpaka unatenganisha nchi mbili. Sasa kwa nini nchi moja (yaani upande mmoja wa mpaka) iwe mzalishaji na nchi nyingine (upande wa pili wa mpaka) iwe mnunuzi tu? Hilo ndilo analohoji Kagaruki. Kwa nini katika mipaka yote Tanzania iwe mpokeaji na si mtoaji? Kuna tatizo kubwa hapo. Kwa mfano bidhaa nyingi za Uganda zinazalishwa Kampala. Umbali wa kutoka Bukoba kwenda Kampala karibu ni sawa na ule wa kutoka Bukoba kwenda Mwanza. Kama bidhaa mbadala za Kitanzania zingekuwepo, kwa ubora na bei nafuu au sawa wafanyabiashara wangezifuata Mwanza. Tatizo ni kwamba Tanzania hatuna bidhaa na zilizopo ni mbovu na aghali. Jambo la pili ni udhaifu wa wazalishai wa Kitanzania. Mbali na watengeneza pombe na makampuni ya simu wazalishaji wengine hawafanyi jitaihada za kuwashawishi walaji kunua bidhaa za Tanzania. La tatu ni uzamani wa sera na watawala katika mikoa kama Kagera. Pale Kyaka kwenye barabara ya kwenda Uganda' baada ya kuvuka mto Kagera kuna kituo cha TRA. Kwa uzoefu wangu kile kituo kazi yake ni kuzuia biashara badala ya kuwa facilitator wa biashara. Mfanyabiashara anayefika pale na magunia, tuseme ishirini ya mchele na analo duka pale Bunazi au mpakani Mutukula anazuiwa eti ana nia ya kuyavusha kwenda Uganda. Polisi nao ni kawaida yao kufukuzana na watu wanaosafirisha bidhaa, hasa kahawa, kwenda Uganda. Mara nyingi wanachotafuta ni rushwa tu. Lakini wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa kutoka Uganda hawafanyiwi hivyo. Sijui kama kuna mtu pale TRA, Polisi na serikali ya Wilaya ya Missenyi anayeelewa concept ya balance of trade. Tanzania ni soko la kila mtu bila sisi kudai na wao wanunue kutoka kwetu. Huenda mzee aliyesema kuwa elimu ya Tanzania ni mbovu alikuwa na maana yake. Kama anaona hali kama hiyo niliyoieleza ikiendekezwa na watu waliosoma kwa nini asihoji kama kweli elimu yao inatosha?
   
Loading...