Nimeenda mradi wa maji mmoja tunaoutekeleza hapa nchini kwetu kwa kutumia mkopo wa mabilioni kutoka "EUROPEAN INVESTMENT BANK" pamoja na AFD.
Mabilioni haya tuliyakopa tunatekeleza mradi huo kwa kutumia kampuni ya kichina.
Kampuni imeajiri wahandisi watanzania wanne na anayelipwa fedha nyingi ni milioni 3.5 lakini kampuni imeajiri wachina kibao ikiwemo wafungwa huko kwao. mfungwa wa kichina ambaye hata elimu yake hajafikia engineer analipwa milioni 6 anapofanya kazi kwenye mradi huu.
Bado mimi najiuliza inakuwaje tunaruhusu mgeni anakuja kwetu analipa mfungwa wa huko kwao kuliko mhandisi wa kwetu?
Halafu wahandisi hawa wameajiriwa wanafanya kazi ambazo si za saiti, kazi za saiti zote wanafanya wachina wenyewe.
Kwa maoni yangu tunalo jukumu kama taifa kuhakikisha tunapokopa, kuhakikisha tunaingiza wataalamu wa kutosha katika miradi miradi hii ambayo tumekopa na baadae tutalipa na kuhakikisha hata watu wetu wanalipwa fedha nzuri kwenye miradi hii.
Nakumbuka mwaka 213 serikali ilipitisha sheria ya wafanyakazi wote wanaofanya kazi kwenye construction kulipwa sio chini ya 10,000 kwa siku. Sheria hii ilileta mapinduzi makubwa kwa vibarua katika makampuni ya ujenzi kwani vibarua walikuwa wanalipwa mpaka elfu 3 kwa siku.
Sasa tunalo eneo jingine la kutazama jinsi gani wataalamu wetu tunaowasomesha wanaingizwa katika miradi hii tuliyokopea fedha kwanza kutengeneza ajira na pili kubakiza sehemu ya pesa hiyo katika jamii yetu.
Upo ubaguzi mkubwa sana katika makampuni mengi yanayotekeleza miradi hii baina ya wazawa na wageni kana kwamba nchi yetu bado hatujapata uhuru na tunayo matabaka bado ya wageni kuwa first class na wenyeji kuwa third class.
Usisahau kukomenti na kunipia kura ili tushirikiane kutokomeza ubaguzi katika jamii yetu ambao una sura ya ajira