Upo uwezekano wa CCM kufutwa pindi kitakaposhindwa uchaguzi wa Kitaifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upo uwezekano wa CCM kufutwa pindi kitakaposhindwa uchaguzi wa Kitaifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chesty, Oct 22, 2011.

 1. C

  Chesty JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,353
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Ndugu wanajamvi, nikiangalia miaka kadhaa inayokuja ni dhahiri kuwa CCM kitaangushwa kwenye uchaguzi wa nchi. Sababu za kuangushwa ni nyingi ila hiyo sio mada yangu kwa sasa. Kwa sasa naangalia nini kitatokea baada ya kuangushwa.

  Ninachoona ni kuwa kutakuwa na ulazima wa kukifuta chama hiki kwani kuna uwezekano baada ya tathmini ikagundulika kuwa hakikuwa na vigezo vya kuwa chama cha siasa. Baadhi ya mambo ambayo nadhani yanaweza kupelekea chama hiki kufutwa ni haya yafuatayo:

  1. Inaweza kugundulika kuwa kulikuwa na support kubwa ya dola ya kukiwezesha kushinda chaguzi za kisiasa

  2. Kwamba Viongozi wake wengi wa chama walihusika katika wizi mkubwa wa rasilimali za nchi hii na kuingia katika mikataba mibovu na isiyo na maslahi kwa nchi ya Tanzania.

  3. Kwamba ni chama ambacho pamoja na kukaa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 kimeshindwa kabisa kujenga taifa lenye uchumi mkubwa unaoweza kukaribiana na South Africa au Botswana kwa sababu rasilimali tulizonazo ni nyingi pengine kuliko za SA na Botswana.

  4. Ni chama ambacho kimeshindwa kujitofautisha kama ni dola au chama, kwa sababu viongozi wake hata kama kutakuwa na ushahidi kuwa wamehusika na uhujumu uchumi, vyombo vya dola haviwaulizi wala kuwachukulia hatua za kisheria; mfano ni sakata la Meremeta, Kagoda, Richmond, n.k.

  5. Ni chama ambacho japokuwa viongozi wake wanasafiri nchi za nje kila siku lakini wameshindwa kujifunza wenzetu wanawezaje kupiga hatua za kimaendeleo wakati sisi tunaendelea kudidimia il hali tuna rasilimali nyingi sana nchini.

  6. Ni chama ambacho kimekuwa kikiwalaghai wananchi wake kuwa kitafanya hivi na vile wakati wa chaguzi lakini mara wanaposhinda wanawasahau kabisa ingawa huu nao ni ujinga wa wale wanaoahidiwa year in year out na hakuna kinachofanyika lakini bado wanakipigia kura, hilo laweza kuwa si kosa la CCM ni kosa la wananchi wenyewe. Hata hivyo CCM itabanwa kuwa ilifanya ulaghai huku ikijua kuwa inafanya ulaghai.

  Ni mengi sana ambayo yanaweza kukifanya CCM kifutwe kwenye uso wa dunia ya Tanzania ila nimeona nisiwachoshe.

  Nawasilisha.
   
 2. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Kweli nakubaliana na wewe kuwa ccm kitafutwa sababu kubwa za kukifuta chama hicho itakuwa ni kukiondoa tu kisiwepo kwasababu uwepo wa ccm tu ni laana kwa watanzania. Chama cha wahuni chama cha wahamiaji haramu kama Bashe na Adeni Rage, pamoja na wahindi haramu waliojaa hapa nchini.
   
 3. p

  politiki JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Kufutwa kwao itakuwa zaidi ni swala la kisheria zaidi kuliko utashi wa mtu, kuingia mikataba mibovu kuwa na viongozi mafisadi pekee hakuwezi kufanya CCM ifutwe. kuna hatima mbili zitaitokea CCM endapo kikitoka madarakani nazo ni CCM kugeuka kuwa KANU ya Kenya kwa sababu watakosa vyeo na pesa za kuwaonga watu hivyo viongozi na wananchama wao wengi watasambaratika na hatima ya pili ni chama hicho kufutwa endapo kitathibitika kuwa kilivunja sheria za nchi kitu ambacho itakuwa rahisi sana kuthibitisha kwani hawatakuwa wana control ofisi ya mwanasheria mkuu na DCI na cha kuthibitisha ni kama CCM iliiba pesa hazina kwa kutumia kampuni ya KAGODA AGRICULTURAL LTD. kufanyia uchaguzi na kuwa matumizi ya pesa nyingi yaliyokuwa yakitumwa kwa msajili yalikuwa ni fake ukilinganisha na matumizi yao makubwa ya fedha wanayoyafanya kwenye kampeni. unakumbuka maneno ya msajili alipoulizwa kuakiki matumizi ya CCM kama kweli yanaendana na taarifa wanayopeleka kwake naye alijibu kuwa siyo kazi kuhakiki yeye anapokea tu na kutia kabatini.
   
 4. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CCM ni kundi la magaidi wa ndani kwani wanahusika na vifo vya watu, kwenye migodi, mauwaji ya Znz na Arusha, kuhamisha makazi ya watu, milipuko ya mabomu na mengi mengineyo hata leo sheria zikifuatwa wanafutwa
   
Loading...