G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,874
Kwa jinsi mambo yanavyoenda na huko tulipotoka, naamini kuwa upo uwezekano mkubwa wa Rais Magufuli kutokuivusha Tanzania salama.
Nimeona vihashiria kuwa sasa wananchi wanaonyesha kuchoshwa kweli na mwenendo wa siasa za kibabe za nchi yetu. Hili ni jambo la hatari.
Ni kweli kuwa kwa muda wa miaka minne na nusu iliyopita, Tanzania imepitia majaribu makubwa na naamini sasa kwenye majaribu hayo ndiyo tuanelekea zaidi kwenye makali.
Unaweza usinielewe kwa sasa kutokana na mtazamo ulio nao, ila inahitaji maombi ya "kufa mtu" ili kuivusha nchi salama na hili wimbi. Inavyoonekana ni kama tumeamua wenyewe kujipeleka huko kutokana na kiburi chetu na kujisahau kuwa sisi tupo duniani na tumezungukwa na ardhi, siyo maji.
Kila kona sasa ni vurugu mechi, mambo ya kuzuia moto kwa nguo wala hayana maana. Kufunika pembe la ng'ombe kwa kiganja huku ukiamini kuwa umelizuia kuchomoza, ni ujinga. Kama nchi tunaelekea kufumbwa macho ili mengine yatokee!
Nani atamfunga paka kengele?