KWELI Upo uwezekano mdogo wa Mwanamke kupata ujauzito akisafisha uke kwa taulo yenye Shahawa

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Ikatokea mwanaume amemwaga manii kwenye taulo ambalo muda mchache baadae mwanamke akalitumia kukaushia uke wake.

Kuna uwezekano akapata ujauzito kupitia taulo hilo?

motherlode-sperm-donor-towels-tmagArticle.jpg
 
Tunachokijua
Ujauzito hutokea baada ya kuungana kwa mbegu ya kiume na yai la mwanamke, tendo ambalo kitaalam huitwa urutubishaji (Fertilization). Tendo hili hutokea kwenye siku maalum katika mzunguko wa hedhi ya mwanamke.

Ili kufanikisha suala hili, Mbegu za kiume (shahawa) hupaswa kutengenezwa na kuhifadhiwa kwenye sehemu iliyo na joto dogo kuliko joto la kawaida la mwili.

Hii ndio sababu ya kwanini vifuko vya korodani (makende) hupatikana nje ya mwili, sehemu inayozalisha joto dogo kiasi kuliko lile linalopatikana kwenye sehemu za ndani ya mwili. Pia, ili mbegu za kiume ziweze kurutubisha yai hupaswa kuzalishwa na kutolewa kwa kiasi kikubwa, ziwe na maumbo mazuri na zinapaswa kuwa na kasi kubwa ya kuogelea.

Kwa upande mwingine, uke kama sehemu ya kiungo kinachopatikana kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke huwa na mazingira yenye asili ya asidi, kati ya 3.8-5.0 kwa kipimo cha pH. Haya sio mazingira rafiki kwa mbegu za kiume.

Kwa kurejea sifa tajwa, JamiiForums imebaini kuwa taulo iliyo na shahawa/mbegu za kiume ikitumika kukaushia uke huwa na uwezekano mdogo sana unaokaribia 0% kusababisha ujauzito.

Hoja yetu imejengwa kwenye misingi zifuatayo;
  1. Mazingira ya asidi yaliyopo ukeni sio rafiki kwa mbegu za kiume, huhatarisha uhai wake na kuzuia zisiogelee vizuri kuelekea kwenye mlango wa kizazi. Kwa maana hii, shahawa zilizopo kwenye taulo huwa na umbali mrefu wa kuogelea hivyo hushindwa kuvuka mlango wa kizazi ili ziingie kwenye mirija ya uzazi kutungisha ujauzito.
  2. Shahawa huwa na muda mfupi sana wa kuishi zinapokuwa nje ya mwili wa binadamu kama hazitahifadhiwa vizuri. Kwenye taulo zinaweza kuishi kwa muda usiozidi nusu saa pekee.
  3. Shahawa hupaswa kumwagwa sehemu iliyo karibu zaidi na mlango wa kizazi ili ujauzito uweze kutungwa. Mashavu ya uke na sehemu za ndani kidogo ya uke zinazosafishwa na taulo zipo umbali mrefu kutoka kwenye mlango wa kizazi hivyo kufanya zoezi hilo kuwa gumu.
Hata hivyo, ikiwa shahawa zitakuwa zimemwagwa nyingi sana na mwanamke aliye kwenye siku sahihi za kupata ujauzito akatumia taulo husika kujisafishia uke wake, uwezekano wa kuingia kwa baadhi ya mbegu za kiume ukeni upo, hivyo hatari ya kupata ujauzito ikiwa zitavuka mlango wa kizazi hutokea.

Pia, kwa kuwa taulo husaidiwa na vidole kujisafisha, upo uwezekano wa mbegu chache za kiume kusukumwa ndani ya tundu la uke na vidole vya mhusika. Hii pia hutoa mwanya mdogo wa kutungwa kwa ujauzito.

Kwa mujibu wa tafiti, mwanamke huwa na 20% ya kupata ujauzito akishiriki tendo la ndoa kwenye kipindi sahihi cha mzunguko wa hedhi yake.

Hii inaonesha kuwa, ikiwa njia sahihi ya kupata ujauzito huwa na uwezekano wa 20% pekee, kujifuta kwa kutumia taulo ni njia iliyo ngumu zaidi, pengine isiwe na uwezekano kabisa wa kutengeneza ujauzito.
Watafiti mbalimbali wamegundua mwanaume akimwaga mbegu zake kwenye maji anaweza kuwapa mimba wanawake wanaoogelea kwenye maji hayo.

Katika gazeti la independent la Leo. Lina ushahidi wa wanawake waliyo Pata mimba katika bwawa la kuogelea.
 

Attachments

  • Screenshot_20231025-092602.png
    Screenshot_20231025-092602.png
    161.7 KB · Views: 8
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom