Upo umuhimu wa Tanzania kuendelea kushirikiana na MABEBERU?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Tanzania tuna kila kitu kuanzia rasilimali watu (60M+ population), rasilimali fedha na natural resources zakutosha kujiendesha wenyewe bila kutegemea mtu,nchi au shirika la nje.

Aidha, tunaamini na ndivyo ilivyo kwenye nadharia kwamba nchi jirani zaidi ya nane zinatuhitaji sisi ziweze kujiendesha kuliko sisi tunavyowahitaji tujiendeshe.

Kwa haya machache, kwanini sisi tusiamue kuachana kabisa kushirikiana na MABEBERU ambao wameonyesha wazi kuimezea mate Tanzania? Wameleta kila uovu yakiwemo magonjwa, tukiamua kutoshirikiana nao tutapata madhara gani?
 
Huku unategemea utalii wa nje huku mikopo na misaada unalamba huku unatafuta masood ta madini nje yaani huku unaota njozi
 
Tanzania tuna kila kitu kuanzia rasilimali watu (60M+ population), rasilimali fedha na natural resources zakutosha kujiendesha wenyewe bila kutegemea mtu,nchi au shirika la nje.

Aidha, tunaamini na ndivyo ilivyo kwenye nadharia kwamba nchi jirani zaidi ya nane zinatuhitaji sisi ziweze kujiendesha kuliko sisi tunavyowahitaji tujiendeshe.

Kwa haya machache, kwanini sisi tusiamue kuachana kabisa kushirikiana na MABEBERU ambao wameonyesha wazi kuimezea mate Tanzania? Wameleta kila uovu yakiwemo magonjwa, tukiamua kutoshirikiana nao tutapata madhara gani?
Mkuu asilimia 90 ya madawa yanayotumika hospitali na vipimo vyote vinatoka ulaya, pia watalii wanatoka ulaya, madini asilimia 100 yanaenda ulaya au kama mnavowaita mabeberu , hata hizi ARV wanatumia watu zinatoka huko , asilimia kubwa ya vitu tunavyotumia hapa bongo hata Hiyo Sim au computer unayotumia inatoka huko vitu vingi bongo ni made in China, India , Korea n.k hadi magari tunayotumia yanatoka huko , na vitu vingi tu vinatoka huko, sasa sijui unaanzaje kuwakwepa hawa watu.

Hebu fikiria upya usikurupuke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fedha sio rasilimali,na kama zingekuwepo fedha za kutosha serikali isengeendelea kukopa kutoka kwa hao mabeberu.
 
Tanzania tuna kila kitu kuanzia rasilimali watu (60M+ population), rasilimali fedha na natural resources zakutosha kujiendesha wenyewe bila kutegemea mtu,nchi au shirika la nje.

Aidha, tunaamini na ndivyo ilivyo kwenye nadharia kwamba nchi jirani zaidi ya nane zinatuhitaji sisi ziweze kujiendesha kuliko sisi tunavyowahitaji tujiendeshe.

Kwa haya machache, kwanini sisi tusiamue kuachana kabisa kushirikiana na MABEBERU ambao wameonyesha wazi kuimezea mate Tanzania? Wameleta kila uovu yakiwemo magonjwa, tukiamua kutoshirikiana nao tutapata madhara gani?
Haiwezekani kwani hata Marekani anategemea nchi nyingine tajiri hata zile maskini ili mambo yake yawe sawa.
 
Back
Top Bottom