Fahamu makundi ya tabia za wanadamu

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,678
106,786
Hello..
Lately I’ve been writing random topics centered on personality traits, this Topic will be serving as a sequel of those Topic. Will focus on other perspective of personalities

Personalities ni nini?
Kwanza kabisa hakuna definition maalumu ya personality hivyo basi ma Guru wa saikolojia kila mmoja anaielezea kadri alivyoilewa, ila mwanasaikolojia Raymond cattel anasema kwamba Personalities ni sifa fulani ambazo zinaweza kubashiri au kumuelezea mtu fulani yukoje. Aina za personalities zimegawanywa katika makundi mawili ambayo ni Personality traits na personality types. Katika personality traits ndipo tunapata makundi mawili maarufu ambayo ni Extroverts na Introverts, humu jamvini kuna mada nyingi zinaelezea makundi haya ya introverts na extroverts. Leo ningependa tuone sifa za kundi la personality types.

Zifuatazo ni ni makundi mawili ya personality types

Type A personality

Hili ni kundi la watu ambao hupenda kuwa wa na haraka, wasio na subira, wenye tahadhari kupita kiasi, na wenye hasira. watu waliopo kundi hili wanakua na tabia zifuatazo.​
  • Wanapenda kutoka sio wa kukaa sehemu moja​
  • Wana shauku na tamaa ya kufanikisha jambo​
  • Wanapenda kufanya vitu kwa mpangilio​
  • Wanajali sana muda​
  • Hupenda kuwa watawala au kuwa viongozi wa mambo​
  • Hawana subira katika kufanya jambo​
  • Wanapenda kujituma sana katika kazi zao (workholics)​
  • Hawapendi ubabaishaji katika mambo​
  • Hupenda kujipa matarajio makubwa zaidi na wanapenda wao ndio wawe mbele katika kutimiza jambo Fulani​
  • Wanafunzi wenye aina hii ya Personality hua wanapata alama za juu (wazee wa kushusha mabanda)​
  • Hupenda kusumbuliwa na magonjwa ya moyo ajili ya kua na shauka na kutokua na subira​
  • Wanatamaa sana ya mafanikio​

Kwa Tanzania baadhi ya watu waliopo kundi hili ni Nyerere, Magufuli,Sokoine

Type B personality

Hili ni kundi ambalo sifa zake zipo kinyume na watu wa kundi A, mara nyingi watu wa kundi hili hutumia mwuda mwingi kujifunza kua na tabia za watu wa kundi A. sifa zao ni…​
  • Huwa wana kiwango kidogo cha stress​
  • Huwa hawajali wala kuwaza pindi wanaposhindwa kutimiza matakwa yao​
  • Pindi wanapokuwa kwenye ushindani wa kushinda au kushindwa mara nyingi hujichukulia kua watashindwa, wanatarajia mabaya wakati wanasubiria mazuri. They prefer to be underdog​

Watu walio kwenye kundi hili hupenda shughli na kazi zinazohusu masuala ya ubunifu maana asili yao hupenda kuchambua mawazo na nadhariaza ya vitu mabalimbali, kazi wazipendazo ni kama vile​
  • Uigizaji​
  • Uandishi​
  • Kutoa ushauri​
  • Therapy​

Kwakua watu wa kundi hili kwa asili yao wana subira na uvumilivu wa mambo hivyo inawafanya wanakua wanauwezo mkubwa wa kufanya maamuzi bora, kuona vitu katika mtazamo mpana pia huweza kuhamasisha utendaji kazi wa pamoja.

Kama unazifahamu characteristics za Extroverts unaweza kudhani kwamba watu wenye Type A ni Extroverts na type B ni Intoverts, Hapana si hivyo. Unaweza kua introverts na ukawa Type A na ukawa Extroverts ukawa type b. Mfano nyerere was a Typical Introvert ila alikua ni Type A na mgufuli alikua Extrovert ila alikua type A pia.

Scorched Earth.

Obsessive –compulsive Disorder (OCD)
ni ugonjwa wa akili na kitabia ambapo mtu mwenye hali hii hua anajisikia uhitaji wa kufanya jambo Fulani mara nyingi kwa kurudia rudia. Watu wenye tatizo hili hua na tabia zifuatazo​
  • Kuogopa kufanya ngono​
  • Kuogopa kupoteza vitu​
  • Kupenda kuosha mikono mara kwa mara​
  • Kuwa mkali kwa watu wengine ajili ya tabia zao​
  • Kujihisi kutokupendwa na kukataliwa​
  • Uoga (anxiety)​
  • Kupenda kupangilia vitu katika mtindo Fulani​
  • Kuhifadhi viyu vya zamani hata kama havina umuhimu (eg. Makaratasi)​
  • Kupenda kutafuta uthibitisho wa kitu, kama kafunga mlango atarudi kutizama tena kama mlango kafunga kweli​
Kwakua OCD inaendana na hali ya mtu kua obsessed na kitu kimoja na kukirudia rudia hali hii inafanya watu wenye tatizo hili kuzama kabisa kwenye the so called Mapenzi. Akiwa nawe atataka uwe nae muda wote, muda wote ataruadia rudia kukwambia anakupend…unaweza kumuona msumbufu lakini sio yeye ni thali tu aliyonayo ndio inamfanya apende kusema hivo. Ukitaka kujua kwamba hujui jichanganye uwe na mahusiano na mtu ambe ni Introvet, ana type A personality na ana OCD na pia awe na
Low latent Inhibition (LLI) utaipata pata. Mwigizaji James Spader ni moja kati ya watu wenye tatizo hili la OCD, anasema kwamba maisha yake ya mahusiano yamekua na changamoto sana kwakua hali hii inamfanya kua kinganganizi kwa mwenzie na kuonekana msumbufu

James Spader

images (16).jpeg

-Vinjii​
 
Scorched earth ni Sera inayotumika jeshini ambapo kama ikitokea vita sehemu, tuseme ikigundulika kwamba waasi wa msumbiji watakuja Tanzania kwa kupitia mtwara basi jeshi linaweza kuondoa watu hapo mtwara na Kuharibu miundombinu yote kama madaraja, majengo, umeme, barabara nk ili waasi wakifika hapo wasivitumie vitu hivyo kwa faida yao (ya kivita)
 
Kwanini??
Yaani unajikuta tu kutokana na kuwa na wasi wasi wa kitu fulani basi akili yako inakulazimisha kufanya jambo fulani kuliko hali ya kawaida ili tu kulikwepa lile unaloliogopa. Unaweza ona ni kawaida ila sio kawaida ni ugonjwa. Maana mpaka kufikia kuitwa OCD basi ni kuwa hyo hali tayari inaathiri maisha yako kwenye mahusiano au hata kiuchumi.
 
Scorched earth ni Sera inayotumika jeshini ambapo kama ikitokea vita sehemu, tuseme ikigundulika kwamba waasi wa msumbiji watakuja Tanzania kwa kupitia mtwara basi jeshi linaweza kuondoa watu hapo mtwara na Kuharibu miundombinu yote kama madaraja, majengo, umeme, barabara nk ili waasi wakifika hapo wasivitumie vitu hivyo kwa faida yao (ya kivita)

Hii ndio mbinu waliyotumia USA kwa wale wavaa kobazi wa Afghanstan
 
Ikiwa una ugonjwa wa obsessive-compulsive (OCD), unajua kwamba dalili zako mara nyingi zinaweza kukuzuia kuanzisha na kudumisha mahusiano ya kimapenzi. Hakika, watu wengi walio na OCD ni waseja, na wale ambao wako kwenye uhusiano mara nyingi huripoti kiwango kikubwa cha mkazo wa uhusiano
 
WANA SIFA NYINGI ZINGINE NI;

1. Wanapata shida kuelezea hisia zao.

2. Wana ugumu wa kuunda na kudumisha uhusiano wa karibu na wengine.

3. Wanafanya kazi kwa bidii, lakini tamaa yao ya ukamilifu inaweza kuwafanya wasiwe na ufanisi.

4. Mara nyingi wanahisi kuwa waadilifu, wenye hasira, na wenye hasira.

5. Mara nyingi wanakabiliwa na kutengwa kwa kijamii.

6. Wanaweza kupata wasiwasi unaotokea na unyogovu.
 
Ila kama ilivyo kwa magonjwa mengine ya akili, OCD hutokea kwa sababu maalum. Huenda kuna jambo liliwahi kukuathiri na ikawa ndyo chanzo cha yote.
Hili jambo binafsi linanitesa sana. Kuna Vitu na watu natamani niwapoteze ila nashindwa..
 
Kwa kweli kuna mambo mingi sana binadamu anatami kuwa nayo au kufanya lakini kutokana na uwezo wa fedha ndio hapo anashidwa kufanya .Ujana nao ni balaa kubwa katika maisha yako usipojitambua basi utafeli kimaisha ,binadamu tumeumbwa na tamaa so usivunjike moyo kwani maisha yote ni tamaa mbele mauti nyuma.
 
Kwa kweli kuna mambo mingi sana binadamu anatami kuwa nayo au kufanya lakini kutokana na uwezo wa fedha ndio hapo anashidwa kufanya .Ujana nao ni balaa kubwa katika maisha yako usipojitambua basi utafeli kimaisha ,binadamu tumeumbwa na tamaa so usivunjike moyo kwani maisha yote ni tamaa mbele mauti nyuma.
Maisha yakishachanganya mtu hujali tena habari za mauti baada ya tamaa
 
Back
Top Bottom