upinzani wenye ukinzani na maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

upinzani wenye ukinzani na maendeleo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng`wanakidiku, Oct 28, 2012.

 1. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimekaa na kufikiri juu ya mstakabali wa siasa zetu na maendeleo ya Tanzania yetu.
  Ni dhahiri kuwa tangu2005 Mh. Dr Jakaya Kikwete alipo pochanguliwa kuwa rais, amekuwa akipambana na wapinzani toka ndani ya chama na nje ya chama.
  Kwa mwaka 2005-2010 alipambana zaidi na upinzani ndani ya chama wakati huo wapinzani nje ya chama walikuwa wanajiimarisha.
  Na sasa 2010-2015 anapambana na upinzani ndani ya chama na nje ya chama. Na tena wapinzani wa nje ya chama wamekomaa kwelikweli, na walianza tu tangu matokeo ya urais yalipotoka 2010. Na upinzani ndani ya chama nao umeongezeka ukilinganisha na 2005-2010.

  1. Je kwa mtindo huu nchi inaweza kuendelea kweli?
  2. Je nini chanzo cha haya yote?
  3. Je ni nani aliyeasili matatizo ya hii migogoro?
  4. Je tutafika kweli kwenye neema ya maisha bora kwa kila mtanzania?
   
 2. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Tutafika kama hatufuati mkumbo na kuacha kushabikia masuala ambyo hayaleti maendeleo. Sidhani kama siasa ndiyo pekee inayoweza kuleta maendeleo. Hivi unaelewa kuwa hata katika matatizo makubwa ya kuyumba kwa uchumi duniani na mgogoro wa fedha duniani siyo wote ni loosers wapo ambao wamekuwa matajiri kutokana na hali iliyvyokuwa na iliyopo, suala ni kwamba unacheza vipi karata yako. Je unakubali kwenda kupiga porojo za siasa za kuchuki ambazo ni adui wa maendelea au unatumia akili yako kujipanga katika kuinua kipato chako. Kumbuka siasa haiwezi kukuleta maendeleo kama siasa yenyewe. Hivi unajiuliza kwa nini wanachama wa vyama tofauti wanapigana hadi kuuana na baada ya muda wale wanaowaongoza katika kufanya fujo wanakuja kukaa meza moja na kugawana madaraka? na sisi walala hoi kubaki na makovu na majeraha bila kujua tulikuwa tunapigania nini?

  Ni vyema kuelewa kuwa mwanasiasa anapokuwa jukwaani kuhubiri chuki ni kwamba yupo kazini na anajitengeneza maisha yake na kipato chake (kwa maana nyingine anafanya investment au marketing ya bidhaa yake ambayo ni maneno yatakayokufanya wewe umpigie kura). Wewe unayeacha kazi yako na kufuatilia hayo unaacha kazi na kutumia muda wako vizuri ndiyo looser.

  Wanaoelewa mchezo huo vizuri wanazidi kujineemesha na kujiimarisha kibishara ili hata kama mfumo ukibadilika waweze kukubalika na mfumo mpya kutokana na umuhimu wa mchango wao kwa maendeleo ya nchi kwa maana watakuwa ndiyo matajiri.

  Iangalie siasa kama biashara yako au kazi yako ndiyo ujuwe namna ya kufit in na kunufaika na hali ilivyo. Nitafurahi kueleimishwa siasa inaletaje maendeleo?
   
 3. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kweli, sema sasa watanzania wengi tumegeuka kuwa wanaharakati badala ya kuangalia maendeleo. Ila umoja na mshikamano ndiyo maana ile sensi of unity ni muhimu.
   
 4. c

  chayowa1981 JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 218
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Nimeipenda hii, japo wakija wale ambao wanahisi kuwa maneno haya yanawalenga watu fulani ambao ni role models wao wataanza kutukana.
  In reality kuna watu washaamua "kupack magari" wakisubiri 2015, ili wayapige start, wakitarajia ya kuwa kutatokea mabadiliko.
  My take; Hata mabadiliko yakija itakuwa kwa wale ambao wanaendesha, kama walikuwa spidi 30 then itakuwa 60. while kwako uliyepack mpaka ukiwasha gari it will be tooo late.
  Nawasilisha
   
Loading...