Elections 2010 Upinzani waziteka ngome za CCM mijini

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Miezi kadha iliyopita, Mzee Mwanakijiji aliweka thread humu JF ikisema ngome za upinzani zimedorora katika miji mikuu hapa nchini. Thread hiyi iliibua post nyingi, nikiwa mmojawapo na nilisema upinzani upo, lakini tu labda siyo organized na kukosa strong leadership.

Uchaguzi wa safari hii umeniprove right -- ngome ya CCM imesambaratishwa katika miji ya Dar, Moshi, Arusha, Musoma, Mwanza, Shinyanga, Iringa na Mbeya.

Soma habari hii kuhusu hapa Dar:









Chadema yatikisa ngome ya CCM Dar

Na Ramadhan Semtawa

TOFAUTI na muongo mmoja uliopita ambao CCM imeweza kuwa na ngome imara ya kisiasa mkoani Dar es Salaam, safari hii kambi ya upinzani imeweza kuiteka baada ya kupata kura za ubunge 395,157 ikilinganishwa na 345,101 za chama tawala.

Pigo hilo la ngome ya CCM limekwenda sambamba na ushindi wa upinzani kwa kupata viti viwili vya ubunge majimbo ya Kawe na Ubungo.

Kwa mujibu wa mchanganuo wa kura za ubunge zilizotangazwa rasmi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), zinaonyesha jimbo la Kinondoni CCM ililinda ngome yake, lakini kwa ushindi mdogo wa kura 51,372 sawa na asilimia 50 dhidi ya 51,150 za Chadema huku jumla ya kura zikiwa ni 102,522.

Jimbo hilo limekuwa likiongozwa na Iddi Azzan wa CCM limeweza kuangukia tena mikononi mwa chama hicho kikongwe barani Afrika.

Katika Jimbo la Ukonga, CCM pia iliweza kutetea ngome yake kwa kura 28,000 sawa na asilimia 40 dhidi ya 18,819 za Chadema na jumla ya kura zilikuwa 46,891, jimbo hilo pia limeangukia mikononi mwa chama tawala.

Hata hivyo, katika Jimbo la Kawe ngome ya CCM ilitikiswa baada ya Chadema kupata kura 65,619 sawa na asilimia 66 dhidi ya 34,412 za CCM, jumla ya kura ni 100,031.

Jimbo la Ubungo, ngome ya CCM ilitikiswa tena baada ya Chadema kupata kura 81,346 sawa na asilimia 62, ikilinganishwa na kura 50,544, huku jumla ya kura zikiwa ni 131,890.

Kwa mara ya kwanza baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, jimbo hilo lilichukuliwa mwaka 1995 na Dk Masumbuko Lamwai kipindi hicho akiwa NCCR-Mageuzi, lakini mahakama ilibatilisha ushindi huo na CCM kupitia kwa Venance Ngulla ikalinyakua tena.

CCM pamoja na kwamba iliweza kushinda Jimbo la Segerea, lakini iliweza kupata upinzani mkubwa baada ya kushinda kwa kura 43,5557 sawa na asilimia 57 dhidi ya 39,150 za Chadema na 18,737 za CUF.

Temeke, jimbo hilo ambalo liliwahi kunyakuliwa na Augustine Mrema akiwa NCRR-Mageuzi, limeangukia tena CCM lakini kwa ushindi mwembamba wa kura 59,886 sawa na asilimia 51 dhidi ya kura 58,339.

Katika jimbo la Kigamboni, CCM pia iliweza kutetea ngome yake lakini kwa nguvu kubwa baada ya kushinda kwa kura 53,389 sawa na asilimia 49 dhidi ya kura 51,370 za Chadema, huku jumla ya kura 104,759.

Hata hivyo, katika Jimbo la Ilala, CCM imeweza kutetea ngome yake kwa kishindo baada ya kupata kura 25,490 sawa na asilimia 26 dhidi ya kura 9,008 katika kura jumla 34,498.

Chanzo: Mwananchi
 
HATA VIJIJINI UPINZANI UPO LAKINI LEVEL YA UCHAKACHUAJI NI KUBWA SANA NA WANANCHI HAWANA MBINU ZA KULINDSA KURA ZAO KUTOKANA NA MAzingira
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom