Upinzani wawajibu chama Tawala.. ni lile sakata la Nape kudai amekuta nyaraka za Siri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upinzani wawajibu chama Tawala.. ni lile sakata la Nape kudai amekuta nyaraka za Siri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by palalisote, Jul 26, 2011.

 1. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Chadema yamjibu Nape kuhusu nyaraka[​IMG]
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye


  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezikana nyaraka za siri zilizodaiwa kunaswa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, kuwa si zake na hazikuandikwa na chama hicho.

  Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbroad Slaa, alitoa ufafanuzi huo alipokuwa akizungumza na NIPASHE kuhusiana na taarifa zilizoandikwa juzi na gazeti dada la NIPASHE JUMAPILI likimunukuu Nnauye kuwa amenasa nyaraka za Chadema zilizokuwa zikitoa maelekezo kwa viongozi wa chama hicho wa ngazi ya mikoa na majimbo.

  Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi, Nape alisema nyaraka alizonasa ni pamoja na barua yenye kumbukumbu namba CDM/DSM/HU/Vol 040/2011 ya Julai 20, 2011 iliyosambazwa kwa wenyeviti wa kila mkoa kuandaa maandamano nchi nzima baada ya Mkutano wa Bunge la bajeti.

  Alisema barua hiyo iliyokuwa imesainiwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, Erasto Tumbo, ilikuwa ikiwashinikiza wenyeviti kuandaa maandamano hayo kwa nia ya kuiabisha serikali kwa madai kwamba imeshindwa kutekeleza majukumu ya kuwaletea maendeleo wananchi.

  Aidha alisema kwamba aliinasa barua nyingine ya Chadema yenye kumbukumbu namba CDM/DSM/Vol.138/2011 ya Juni 30, 2011 iliyosainiwa na Tumbo kwenda kwa makatibu wa majimbo kutekeleza agizo la Dk. Slaa la kuwahamasisha wananchi wagomee shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

  Dk. Slaa alisema mfumo wa namba za kumbukumbu katika barua zote mbili zilizotolewa na Nnauye kwenye mkutano huo, haziendani na mfumo wa kuweka namba za kumbukumbu unaotumiwa na Chadema.

  "Mbali na dosari hiyo iliyoko kwenye barua za Nnauye, hata katika tarehe ambazo Nnauye anadai kwamba barua hizo ziliandikwa yaani, Julai 20, 2011 na Juni 30, 2011, hakuna barua yoyote iliyoandikwa toka au kuingia makao makuu ya Chadema," alisema.

  Dk. Slaa alisema yeye binafsi na Chadema kwa ujumla, wanafahamika na wananchi jinsi walivyomstari wa mbele kuhamasisha maendeleo ya wananchi, kwa hivyo haiwezekani wakashiriki kwa namna yoyote ile kuwazuia wananchi wasichangie maendeleo.

  Dk. Slaa alisema suala la maandamano kwa Chadema halihitaji kuandikiwa waraka wa siri hata siku moja kwa kuwa wao hutangaza hadharani wanapohitaji kufanya maandamano.

  "Chadema huwa tunatangaza maandamano yetu hadharani, mbele ya vyombo vya habari, kupitia kwenye mikutano tunayofanya. Tumeshasema kwamba tutaendelea kuandamana mpaka kieleweke na watu wote wanatambua hilo," alisema na kuongeza: "Sasa kwa nini tuandike barua ya siri? "

  Alisema bado wananchi wanakabiliwa na maisha magumu,ufisadi, tatizo la umeme nchini na bei ya vyakula kuendelea kupanda, Chadema wataendelea kuandamana na safari hii maandamano yao yatakuwa katika mikoa ya Dodoma, Singida, Morogoro, Manyara na Tabora.


  Chanzo: Nipashe
   
 2. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,364
  Trophy Points: 280
  nape ni kilaza siku zote tunasema,..anataka kuiga style dr.slaa ya kukamata nyaraka,.hawezi,.wameghushi barua lumumba ili ionekane nao wako makini,..asije akajisahau akawaonyesha waandishi wa habari nyaraka za kuanzishwa kwa CCJ!!!ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu nzuri,ipo siku nape atajisahau...
   
 3. m

  marembo JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni ajabu mtu waliemwona anafaa kushika wadhifa huu nyeti ni kijana lakini bado anafanya kazi na kuwaza kiuzee. Kwanza hata spidi yake ni kali na hana uangalifu. Mambo ya kudurusu (copying) ndiyo yaliyojaa CCM. Mara maandamano na mikutano haina tija wao sasa ndio wanaandamana. Mbona mambo ya CDM yako wazi na wananchi wanajua ndio wakombozi wao. Leo hii bila hata kupiga hesabu anakwenda kwenye ngome ya CDM Moshi na kuanza kuongea mambo ya kubuni. Kama alivyosema Dr wa kweli Slaa hata kipofu hapaswi kuelezwa kuhusu maandamano ya CDM. Kagushi karatasi aliyoandikiwa anasema waraka wa sir (ukifanya uchunguzi utagundua na hizo barua za siri wametoa pesa nyingi tu)i. Kweli safari hii CCM wamepatikana hakuna issue. Nasikia hata watu wachache waliophudhuria mkutano wake waliletwa na fuso kama ilivyo kawaida yao baada ya kugawa pesa. Halafu huyu kijana anamuwaza sana Dr Slaa maana kila aendako ooh Slaa anapata mshahara wa mil 7. Nadhani hata akiwa amelala anawaza huyu shujaa ambae ni mwiba kaw CCM. Mbona hagusii mailioni yaliyochangwa na Jairo kwa ajili ya kupenyeza bajeti bomu? Sasa tunawaelewa vizuri na hadanganywi mtu ni mapambano hadi kieleweke. Peoples's Power ndio jawabu.
   
 4. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Kama ni kweli Nape amegushi barua hizo ili kukichafua CDM, huo ndio utakuwa mwisho wake kisiasa. On the other hand, kufanya hivyo ndio asili ya CCM kwani waliweza kushindwa kuwakamata makada wao waliochapisha kadi feki za CCM na kugawa ili washinde kura za maoni!

  Looking on the positive side, CDM would not have faulted had they been planning for the said demonstrations. CCM and its government have failed miserably in bringing development to this country since independence. To add salt to a wound, its MPs in the current Bunge session are behaving like a herd of elephants following the matriach wherever she goes, even in a ditch. So, to me, it is in order for such demonstrations to take place.
   
 5. Queen Kyusa

  Queen Kyusa JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Nape hana kazi ya kufanya so anataka kupata umaarufu kupitia CDM watz hadudanganyiki tumeishajua janja ya Magamba. Hivi anavopita kila mkoa kunadi sera ya kujivua gamba bibi yangu kijijini inamsaidia nini wakati maisha yamepanda sana.yani mm nawachukia sana viongozi wetu aswa pale wanavyotufanya ss mazumbukuku hatuna akili hata moja.

  Wtz tunashida nyingi sana lakini cha ajabu ccm badala ya kutupa strategy ya jinsi ya kututatulia shida tulizo nazo wao wamekazana na mambo ya kujivua gama huu ni ukosefu wa akili ambao sijawahi kuuona mahali popote duniani.
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,745
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu Nape kujikoboa hivyo usoni anataka nini haswa?
   
 7. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Natamani siku moja kuwe na maandamano ya Chadema na ccm sehemu tofauti za mji mmoja. mfano Mbeya ccm waandamane kwenda Uwanja wa Sokoine na Chadema waandamane kwenda uwanja wa Dr. Slaa (Luanda Nzovwe). Nakumbuka ile ya ccm ya Mkapa na Cisco 1995 na NCCR mageuzi ya Mrema na Lamwai pale Temeke. CCm walikuwa Mwenbe yanga na NCCR walikuwa viwanja vya veterinary.
   
 8. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nape chama chako na wewe mwenyewe kinahitaji kupata politicla consultant ili kiweze kujua ni mambo gani muhimu yakufanya ili kirejee kwenye reli, hakika sasa wewe unapotea bila kujua, umepanda chombo ambacho kwa fikra zako unaona kitakufikisha lakini badala ya kufika ni kupotelea njiani ndugu yangu.

  Kama kweli mnataka kuirudisha ccm kwenye reli hakuna budi kufanya upembuzi yakinifu wa kilicho wasibu na kujua hatua za kuchukua, na hili linapaswa kufanywa kitaalamu sio uchakachuaji wa kina Mukama na wenzake ambao wamefumbia macho matatizo ya chama na kuleta porojo.
   
 9. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Nape anahitaji vipimo vya ubongo wake, sioni nyaraka za siri hapa, watu wanaandikiana barua za maandamano halafu unasema nyaraka za siri wakati maandamano yenyewe hayawi ya siri. Huku kutapa tapa na kutafuta umaarufu kwa njia isiyostahili ni uwendawazimu. Ningekuelewa ungekuwa umepata nyaraka za ufisadi ndani ya CHADEMA.
   
 10. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hizo Documents,kuna wataalam wameishakula hela hapo! Wamekwenda kwa pipa na staili za kuiga.Watu wakaona hapo na sehemu ya kutengeneza pesa....unachukua pesa na unawapa documents za UONGO! UMEMALIZA!
   
 11. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  nani kakwambia kuna ufisadi chadema!
   
 12. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Huyu kilaza ameanza uzushi,karibu siasa zitamshinda!!
   
 13. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  nape ni bora ya tambwe, ameishiwa hoja kabisa hata mkutano wa moshi juzi bado alikuwa akimponda dr slaa kwa kuishinikiza cdm imlipe mil 7 wkt mambo yalishawekwa hadharani siku nyingi na sijui ni mwananchi gani asiyefahamu
   
 14. M

  Mtoto Wa Bibi New Member

  #14
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siasa hizi zimepitwa na wakati bwana Nape,zilifanywa na Mahita na visu vyake vya kariakoo dhidi ya CUF so i wonder u comeup with the same old trick what we need are solutions of our problems not dirty politics u used to play in ur weak ccm!
   
 15. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nape hana upeo wa kuchambua mambo ya msingi
   
 16. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nape huna sera tena..,kwisa habari ndugu yangu angalia umeanza umbea sasa...utabakia na wambea wenzako lol...
   
 17. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  hilo jamaa ukilitazama tu hata sura yake linaonekana linafiki la kutupwa.....tumboni linakula ccm lakini akilini linawaza ccj....mijitu minafiki haiachi kutapatapa
   
 18. a

  amaniwakusoma Member

  #18
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Relyin on facts: kwan Dr. Slaa kulipwa 7mil inakuwaje hoja ya kuijadili kitaifa?
  Maandamano yakushinikiza serikal itende matakwa ya wananchi ndo kitu hoja yakumtoa mtu Dar kuja moshi kutueleza? By the way we r the supporters of demonstration!

  Vtu kama upunguf wa umeme, ufisadi, uvunjifu wa Haki za binadamu, n.k. Ndo vtu vya kuzungumzia! Co eti nimekamata barua inayoelekeza kuandaa maandamano nchi nzima!
  "RESISTANCE TO OPRESION IS OBIDIENT TO GOD"
   
 19. j

  jiccaman Member

  #19
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  may GOD almighty forgive him,very sad kuwa na watu kama hawa
   
 20. TinyMonster

  TinyMonster JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Hivi kuna siku inapita bila kumuongelea Nape humu? imetosha jamani tushamjua wote kuwa Bwana Mdogo ni wale ambao CCM wanwaita majeruhi wakisiasa, hakuna haja ya kuendelea kumpa attention hapa. Hakuna haja ya kuendelea kupambana na vidagaaa wakati bahari tunayokabiliana nayo imejaa papa na jerryfish wakali.
   
Loading...