Upinzani wakihudhuria wanadharirishwa, wanapotezewa, wasipokuwepo wanafitinishwa. Wafanyeje?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
Habari wadau!

Naona ndo sera ya chama tawala hasa kwa awamu hii nitaelezea baadhi ya matukio ya kitaifa na tushauriane hapa kipi kifanyike tuondoa mzizi wa fitna na ubaguzi unaoshamili kwa sasa.

1. Mbunge wa Lindi alihudhuria shughuri ya rais lakini aliambulia fedhea toka kwa mkuu wa msafara kwa kuambiwa hawajali wananchi wake kwa kushindwa kuchangia fedha. Na kunyimwa nafasi ya kujieleza baada kugundua mkubwa huyo kateleza.
2. Uzinduzi wa Fly over za dar yakajirudia tena kwa upinzani kupotezewa kabisaaa.
3. Kwa Rwakatale Bukoba alijibiwa majibu ya ajabu sana hasa yaliwalenga walio mchagua mbunge kwamba kwa kuwa mmechagua mpinzani mtakoma.
4. Ufunguzi wa hostel za udsm mbunge hakwenda huku nyuma bwana mkubwa akamtafuta kwenye kadamnasi na kusema angekuwepo angempa chochote aombacho.
5. Moshi Mbunge, Meya wa jiji wakazuiwa kuzungumza na viongozi wa dini alipoenda kwenye mei mosi.
6. Kesho yake meya, mbunge na Mwenyekiti wa CDM wakahudhuria sherehe hizo hakuwakaribisha ila aliwaita woooote wa nguo za kijani kusalimia kwa miamvuli ya spika, mwenyekiti wa kamati bungeni na wengineo wa ccm.
7. Leo kwenye kuaga miili wamepotezewa kuanzia meya hadi mbunge wa mji husika.

8. Na mengine mengi.....

Sasa tushairiane hapa ni kukata ushirikiano kabisa na hawa au tufanyeje waone umuhimu na waache ubaguzi kama wa mkaburu?
 
Kwenye hili la Arusha nadhani Mungu ndiye anayesikiliza maombi zaidi na pole.

Hivyo tusilalamike kama tulidhamiria kutoka moyoni zaidi pasi na kufikiria maonesho au watu watasemaje/kuonaje.
 
Hivyo naona kama ni vitu vidogovidogo wakati mwingine. Mtu mwenye malengo makubwa ya kukamata mamlaka kihalali hayo hayawezi kumtoa kwenye mstari. Kung'ang'ania hiyo kama agenda kuu ni kutaka kututangazia kuwa hakuna kikubwa mnacholenga. Hudhurieni Kila mnapotakiwa kuhudhuria....
 
Mm si mwanachama wa chama chochote ila sipendi tabia ya wanasiasa kupenda kudandia matukio yasiyowahusu japo yako maeneo yao kwa mgongo wa eti wenyeji ila wakiwa na azma ya kuingiza siasa zao

Kwa mf kwa kwenye msiba uliotokea Arusha kilinishangaza kitendo cha baadhi ya makada na wengine viongozi kuvaa sare za vyama vyao vya siasa wakati
wananchi tuko kwenye maombolezo, nikawa najiuliza hawa wanasiasa wana akili timamu kweli?

Mara gwanda za kadi mara za kijani nikahisi tuko kwenye kampeni, kama hiyo haitoshi wengine wakaanza na kulalamika eti hawakupewa nafasi (mic) kutoa pole.

Wote waliofika wafiwa tunaamini mlikuwa na moyo mwema hivyo hakuna sababu ya kila mtu kulalamika hakupewa mic.

Pia tunawashukuru watz wote kwa sala zenu ktk kipindi hiki kigumu cha maombolezo ila tafadhali msiingize siasa maana mnawaumiza wafiwa tu
 
Mm huwa na amini dawa ya moto ni moto.
Uwe ni mwendo wa kudhalarishana tu.

Mtu anakurupuka eti Halmashauri ya Hai imelipwa bilioni 1.3 za barabara wakati Halmashauri imepokea millioni 300 tu!!! Huoni anakuchonganisha na wananchi. Iwe ni mwendo wa kudhalarishana wote kila mmoja kwa nafasi yake. Najua siku akidhalarishwa mkuu na chizi atakae jitoa akili heshima itarudi tu. Hiki ni kizazi cha Bangi... wao waendelee na Ujinga wao.
Oneday watakopsa pa kuificha aibu kuu!!
 
Dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana itatafuna sana nchi kwa hii miaka mitano. Tulitegemea vijana wanajielewa kumbe vilaza sijui tzd unaenda wapi! Upinzani sio dhambi jamani no fikra mbadala tu ya kuiletea nchi yetu Maendeleo.
 
Back
Top Bottom